KASHFA KWENYE BAJETI 2010/11: Shilingi Bilioni 500 zimeenda wapi?

KASHFA KWENYE BAJETI 2010/11: Shilingi Bilioni 500 zimeenda wapi?

Kabisa Masa, kuna haja ya Dr kufuatilia utata huu ili tujuwe kulikoni maana huyo Mkulo simuamini hata kidogo anafanya madudu karibu kila leo. Kama utakumbuka aliwahi kutamka pesa za EPA si za Serikali baada ya kubanwa sana ndiyo akasalimu amri.

Mkulo na Zakia Megji sawa tu no difference.
Dr Slaa na Zitto wanaweza tupa majibu ya kweli hapa kwenye mkanganyiko huu kama ni kweli.
 

Rais Kikwete hajui bajeti ya serikali yake mwenyewe?

JUNE 10, 2010

Kwenye website ya Wizara ya Fedha, hotuba iliyowekwa inasema hivi:

"Mheshimiwa Spika, Serikali imepanga kutumia jumla ya shilingi 11,609.557 bilioni (trilioni 11.6) katika mwaka 2010/11 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na ya maendeleo. Matumizi haya yatagharamiwa na mapato ya ndani, mikopo ya ndani na nje, pamoja na misaada na mikopo kutoka kwa washirika wa maendeleo." -- Ukurasa wa 70 wa hotuba ya bajeti ya Mkulo.

(http://www.mof.go.tz/mofdocs/msemaji...%202010-11.pdf)

Hotuba ya bajeti waliyogawiwa wabunge June 10 siku ya bajeti na kutoka kama tangazo kwenye magazeti siku inayofuata (June 11) hapo kwenye hiyo qoute hapo juu figure inayotajwa ilikuwa ni 11.1 trilion shillings (ninayo nakala).

JUNE 21, 2O1O

Kwenye hotuba yake Dodoma wakati wa kuchukua fomu za kugombea tena Urais kupitia CCM, Rais Kikwete alisema (nanukuu):

"Uchumi wa taifa, pato la taifa na pato la Mtanzania limeendelea kuongezeka na kuwa kubwa zaidi kuliko ilivyokuwa mwaka 2005 na idadi ya Watanzania wanaoishi katika umaskini uliokithiri imepungua, ingawa sio kwa kasi tuliyotarajia. Bajeti ya Serikali nayo imeongezeka sana kutoka shilingi trilioni 4.8 mwaka 2005/2006 hadi shilingi trilioni 11.1 mwaka 2010/2011. Tumezidi kupunguza utegemezi wa misaada kutoka nje katika bajeti yetu. Mafanikio ni mengi sana, na itakapofika wakati wa kampeni tutayaeleza yote kwa kina."

Hapa ina maana Rais wa nchi hajui kuwa serikali yake imepanga kutumia 11.6 trillion/- au bajeti halisi ni hiyo 11.1 trillion/-? Je, hizo shilingi bilioni 500 zimeenda wapi?

Fumbuka, this is a serious matter...

inatia shaka na kusikitisha sana kwamba viongozi wetu wengi hawasomi taarifa na wanakosa muda wa kujipanga kabla ya public address. waTz hatupendi statistics lakini huwa tunataka tuzitumie kutukweza.

Kwenye hili nadhani tatizo liko kwa rais na wasaidizi wake zaidi kwani walitakiwa wapitie atakachosoma.....

SERIOUSNESS NI KITU AMBACHO HAKIPO KWA WENGI WA WATENDAJI NA VIONGOZI WETU
 
Kwanini watu wawili tena wenye nafasi nyeti kama Rais na Waziri wa Fedha wakosee kutamka figure sahihi tena figure zao zifanane (11.1)? It is too much of a coincidence.


Ndugu usijaribu kutunga na ku-sensationalize mambo wakati simple reasoning inakwambia kuna tofauti kati ya kilichosemwa na kilichoandikwa kwa wino.

Hiyo bajeti ya trilllioni 11.1 ushahidi wake unadai ni "Mkulo kasema" au "Kikwete kasema" wakati ile ya trillioni 11.6 ndiyo imeandikwa kwenye nyaraka zilizopo tovuti za MoF ( http://www.mof.go.tz/mofdocs/msemaji... 2010-11.pdf)
na Bunge ( http://www.parliament.go.tz/bunge/docs/budget2010.pdf ).

Ni wazi bajeti iliyopitishwa itakuwa ile iliyoandikwa kwenye hizo docs na siyo ile iliyotoka vinywani mwa Kikwete na Mkullo.
 
Ninyi mtasema typing error kumbe wanataka peleka izo 500 kwa kampeni za CCM.
Hii ndo danganyika bwana!
 
Please don't keep this thing on this forum alone. This is big. Let us blow it up. Let as many Tanzanians as possible know about it. Let us not entrust it to Dr. Slaa alone. Let us help him. As for Zitto Kabwe, I think he is about to decamp. Don't bank on him.
 
Kuna mtu kasema raisi kapotoshwa, siyo kweli, sahihi ni kwamba raisi ndiye aliyeagiza yafanywe hayo...
 
Lakini inakuwaje Wabunge wote wawe hawajaliona hili? Yani woooote? Haishangazi hata hivyo, maana wanatoroka sana sessions wako busy wanajiandaa na kura za maoni....
Tunahitaji maelezo, na mabadiliko yafanyike. Hakuna utani hapa

Sema hivi: Inakuwaje Mh Dr Slaa hajaliona hilo? Nashauri hivyo kwa sababu siyo tabia ya wabunge kufuatilia yaliyoandikwa na yale yanayosemwa. Fahamu kwamba sehemu kubwa ya majibu yanayotolewa na mawaziri/serikali kwa maswali yao huwa hayana ukweli wowote na baada ya hapo kila Mheshimiwa husahau.
 
I really don't understand where is the problem!!!...

Zikikubaliana idadi manake nini? say wote wanasema ni trilioni 11.1 au trilioni 11.6 .. Ina maana gani?
 
I really don't understand where is the problem!!!...

Zikikubaliana idadi manake nini? say wote wanasema ni trilioni 11.1 au trilioni 11.6 .. Ina maana gani?

Respect, Mwanakijiji, Ni vizuri tujue bajeti yetu ni TSh ngapi, sioni kama kuna ubaya wowote. Halafu nchi yetu tumechezewa mazingaombwe sana na watendaji wetu, ndio maana watu wanafuatilia kila neno linalotamkwa na viongozi wetu!
 
Kichuguu,

Kiingereza na Kiswahili katka mfumo wa budget tofauti yake ni 500bn Tshs - Kumbuka kuna nakala ya Budget kwa aili ya "wafadhili" na kuna nakala ya Budget kwa ajili ya watanzania!
 
Kichuguu,

Kiingereza na Kiswahili katka mfumo wa budget tofauti yake ni 500mil Tshs - Kumbuka kuna nakala ya Budget kwa aili ya "wafadhili" na kuna nakala ya Budget kwa ajili ya watanzania!

Mkuu,

Hapana, tofauti iliyopo ni TShs bilioni (siyo million) 497.138. Nakala ya kiingereza inayokwenda kwa wafadhili iaonyesha kuwa tutamuia Tsh 11,112.419 bilion, lakini kiasi kilichoombwa kiidhinishwe bungeni kwa kiswahili Tsh 11,609.557 billioni; kwa hiyo bunge liliidhinisha zaidi ya bajeti halisi, hizo za ziada hatujui zinakwenda wapi.
 
Duuh, hapo hakuna cha typing error wala mtoto wake, kwani maandishi yamerudiwa mara mbilimbili. I wonder kama bajeti zilizopita hazikuwa na kosa kama hilo hilo.

Ina shangaza sana kuona kosa kubwa namna hiyo limepitishwa - wabunge wa CCM wote wakisema NDIYOOO!! Hamna aliyeondoa shillingi. Do they ever read??

Lakini kwa upande mwingine napenda kuuliza; kwanini ile ya wafadhili ndiyo iwe yenye pesa pungufu na ile kwenye nakala ya walalahoi iwe na ziada??! Mimi nilitegemea kinyume chake.
 
Inaonekana suala hili la Waziri Mkullo kuandaa bajeti mbili zenye makadirio tofauti ni HALALI. In fact kulingana na habari aliyoandika mtoa mada Fumbuka Ng'wanakilala tarehe 12 Juni (google "Tanzania budget discrepancy 2010" amenukuu John Cheyo ambaye anajua kuwapo tofauti hii na kushangaa kwa nini Waziri Mkullo hajatoa maelezo yoyote hadi sasa ya hiyo tofauti.
 
Mkuu,

Hapana, tofauti iliyopo ni TShs bilioni (siyo million) 497.138. Nakala ya kiingereza inayokwenda kwa wafadhili iaonyesha kuwa tutamuia Tsh 11,112.419 bilion, lakini kiasi kilichoombwa kiidhinishwe bungeni kwa kiswahili Tsh 11,609.557 billioni; kwa hiyo bunge liliidhinisha zaidi ya bajeti halisi, hizo za ziada hatujui zinakwenda wapi.

Noted and corrected in my post.

Wabunge hawakuona tofauti kwa maana wengi hawa hesabu za "decimali" au "kiingereza"! Ndiyo maana hata ukipita pita mitaa ya nchi utasikia bajeti ya serikali mwaka 2010/11 ni "trilion 11" - nimewasikia wanasiasa, wasomi, e.t.c : wote hawataji 11 point xxxx!
 
I really don't understand where is the problem!!!...

Zikikubaliana idadi manake nini? say wote wanasema ni trilioni 11.1 au trilioni 11.6 .. Ina maana gani?
MKUU, much as we usually dont follow our mipango kazi... it is always important to satrt with balanced records.... and budget as pivot to our implementations must be balanced

UTAPIMAJE MATUMIZI, UTAKUAJE NA DATA MBILI ZA MAPATO HAYOHAYO? UTAKUAJE NA TABIA YA KUKOSEA BASIC MATHS YET UWE WAZIRI WA FEDHA NA UCHUMI????

INAKUJIA VIPI AKILINI NCHI INA WACHUMI WANAOSHINDWA HATA MAGAZIJUTO??

BUDGET BEING A MANAGEMENT TOOL, NEEDS TO BE RELIABLE, ACCURATE AND CONSISTENT WITH ITS INPUTS
 
[/SIZE] 81. Mr. Speaker, the budget frame takes into account the expected outcomes of the tax measures that I explained above. The following table summarizes the budget frame for 2010/2011.

BUDGET FRAME 2010/2011

Revenue
Shillings in Millions

A
Domestic Revenue

6,003,590

(i) Tax Revenue
5,652,580

(ii) Non Tax Revenue
351,000

B
LGAs Own Source

172,582

C
Foreign Loans and Grants- general Budget Support

821, 645

D
Foreign Loans and Grants- Basket and projects

2,452,908

(i) Project Loans and Grants - 1,975,120

(ii) Basket Loans and Grants - 477,788

E
External and Domestic Borrowing

1,331,212

F

Domestic Borrowing (Roll Over)

797,620

G

Privatization Proceeds

30,000



Total Revenue - 11,609,557

Total Expenditure

H

Recurrent Expenditure

7,790,506

(i) Public Debt
1,756,044


(ii)Ministries
4,155,768

(iii)Regions
119,580

(iv)Local Government Authorities
1,759,114

I
Development Expenditure

3,819,051

(i) Local

1,366,143

(ii)Foreign
2,452,908

Total Expenditure - 11,609,557


Wakuu labda tusaidiane, sifahamu kama mfumo unaotumika katika kuandaa hii bajeti ni tofauti na kujumlisha nambari. Kwa hizo figures zilizotolewa, najaribu kujumlisha sioni kama macho yangu yananipa jibu linalofanana kama si makosa katika kujumlisha labda kuna utaratibu mwingine tofauti ambapo yawezekana wengine hatuujui katika hili!!!!

Revenue
Shillings in Millions (A - G)

5,652,580

351,000

172,582

821,645

2,452,908

1,975,120

477,788

1,331,212

797,620

30,000
___________

19,244,400
______________

Total Expenditures (H-I)

7,790,506

1,756,044

4,155,768

119,580

1,759,114

3,819,051

1,366,143

2,452,908
__________

23,219,114
_____________
 
Back
Top Bottom