KASHFA KWENYE BAJETI 2010/11: Shilingi Bilioni 500 zimeenda wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

KASHFA KWENYE BAJETI 2010/11: Shilingi Bilioni 500 zimeenda wapi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Fumbuka, Jul 1, 2010.

 1. F

  Fumbuka New Member

  #1
  Jul 1, 2010
  Joined: Jul 1, 2010
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Natanguliza salaam kwa wana JF wote,

  Kuna jambo limekuwa linanitatiza labda wenzangu mnaweza kunisaidia kupata ufafanuzi. Kumekuwa na utata mkubwa kuhusu jumla ya pesa ambazo serikali imepanga kutumia kwenye bajeti yake mpya iliyopitishwa na Bunge hivi karibuni.


  Je, bajeti ya serikali kwa mwaka 2010/11 ni sh 11.1 trillion/- au sh 11.6 trillion/-?


  Kwenye hotuba yake ya bajeti, Waziri wa Fedha, Mustafa Mkullo, anatoa figure mbili tofauti -- yaani 11.1 trillion/- na 11.6 trillion/-. Tofauti ya figures hizi mbili ni 500 billion shillings! Pesa nyingi sana hii.


  This is a very serious matter. Inakuwaje kuwe na mkanganyiko kwenye figure namna hiyo, tena kwa kiwango kikubwa namna hiyo? Bajeti ni swala very sensitive ambapo ikishapitishwa na Bunge, serikali hairuhusiwi kufanya matumizi nje ya hapo unless inapata kibali maalum cha Wabunge.


  Sasa swali ninalojiuliza mimi ni kuwa Bunge imepitisha bajeti ya 11.1 trillion/- au 11.6 trillion/-?


  Alipo wasilisha mwelekeo wa bajeti kwenye kamati ya fedha ya Bunge jijini Dar es Salaam kabla ya kuanza kikao cha bajeti, Mkulo alisema matumizi ya serikali 2010/11 yatakuwa 11.1 trillion/-. Kwenye hotuba yake Bungeni akasema ni 11.1 trillion/- na 11.6 trillion/-.


  Juzi, kwenye hotuba yake wakati wa kuchukua fomu ya kugombea Urais tena kupitia CCM, Rais Jakaya Kikwete alisema kuwa bajeti imekuwa mpaka kufikia 11.1 trillion/- kwa mwaka 2010/11. Sasa ile bajeti ya 11.6 trilion/- iliyopitishwa na Bunge imekuaje?


  Rais Kikwete amepotoshwa kuhusu bajeti halisi ya serikali mwaka 2010/11? Je, hiyo tofauti ya bajeti ya shilingi bilioni 500 imeenda wapi? Au ni pesa za wakubwa za uchaguzi hizo?

  Naomba, majibu, maoni au maswali zaidi kwa wana JF wenzangu tafadhali.

  Zaidi, napendekeza soma hii post
   
 2. Questt

  Questt JF-Expert Member

  #2
  Jul 1, 2010
  Joined: Oct 8, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Sijakuelewa kabisa...inamaana bungeni ziliwasilishwa figure mbili tofauti???
   
 3. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #3
  Jul 1, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Dr Slaa hapa tunamwitaji aje atusaidie!
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Jul 1, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,811
  Likes Received: 83,208
  Trophy Points: 280
  Kabisa Masa, kuna haja ya Dr kufuatilia utata huu ili tujuwe kulikoni maana huyo Mkulo simuamini hata kidogo anafanya madudu karibu kila leo. Kama utakumbuka aliwahi kutamka pesa za EPA si za Serikali baada ya kubanwa sana ndiyo akasalimu amri.
   
 5. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #5
  Jul 1, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mkulo ni VUVUZELA tu!
   
 6. F

  Fumbuka New Member

  #6
  Jul 1, 2010
  Joined: Jul 1, 2010
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Rais Kikwete hajui bajeti ya serikali yake mwenyewe?

  JUNE 10, 2010

  Kwenye website ya Wizara ya Fedha, hotuba iliyowekwa inasema hivi:

  "Mheshimiwa Spika, Serikali imepanga kutumia jumla ya shilingi 11,609.557 bilioni (trilioni 11.6) katika mwaka 2010/11 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na ya maendeleo. Matumizi haya yatagharamiwa na mapato ya ndani, mikopo ya ndani na nje, pamoja na misaada na mikopo kutoka kwa washirika wa maendeleo." -- Ukurasa wa 70 wa hotuba ya bajeti ya Mkulo.

  (http://www.mof.go.tz/mofdocs/msemaji/HOTUBA%20%20YA%20BAJETI%20MWAKA%202010-11.pdf)

  Hotuba ya bajeti waliyogawiwa wabunge June 10 siku ya bajeti na kutoka kama tangazo kwenye magazeti siku inayofuata (June 11) hapo kwenye hiyo qoute hapo juu figure inayotajwa ilikuwa ni 11.1 trilion shillings (ninayo nakala).

  JUNE 21, 2O1O

  Kwenye hotuba yake Dodoma wakati wa kuchukua fomu za kugombea tena Urais kupitia CCM, Rais Kikwete alisema (nanukuu):

  "Uchumi wa taifa, pato la taifa na pato la Mtanzania limeendelea kuongezeka na kuwa kubwa zaidi kuliko ilivyokuwa mwaka 2005 na idadi ya Watanzania wanaoishi katika umaskini uliokithiri imepungua, ingawa sio kwa kasi tuliyotarajia. Bajeti ya Serikali nayo imeongezeka sana kutoka shilingi trilioni 4.8 mwaka 2005/2006 hadi shilingi trilioni 11.1 mwaka 2010/2011. Tumezidi kupunguza utegemezi wa misaada kutoka nje katika bajeti yetu. Mafanikio ni mengi sana, na itakapofika wakati wa kampeni tutayaeleza yote kwa kina."

  Hapa ina maana Rais wa nchi hajui kuwa serikali yake imepanga kutumia 11.6 trillion/- au bajeti halisi ni hiyo 11.1 trillion/-? Je, hizo shilingi bilioni 500 zimeenda wapi?
   
 7. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #7
  Jul 1, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Jibu jepesi ni makosa ya uchapishaji !

  Huyu raisi anapenda matani alikuwa labda anatania tu
   
 8. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #8
  Jul 1, 2010
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  I wouldn’t dare to quote our president. Najuwa ni mtu wa aina gani. Like our modern instrument, ”garbage in, garbage out.”

  Tatizo ni huyo waziri wake kwa nini ataje figure mbili tofauti. Yawezekana kasema siri maana hiyo ziada yaweza kuwa ni bajeti ya CCM. Always kuna bajeti ya CCM ndani ya Bajeti kuu.
   
 9. F

  Fanfa JF-Expert Member

  #9
  Jul 1, 2010
  Joined: Sep 25, 2009
  Messages: 538
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  WanaJF, hii hapa ni sehemu ya hotuba ya MKULO. Bajeti iliyotajwa kwenye jedwali hapo chini ni tofauti na maelezo kuanzia 78. Mr speaker, ......

  78. Mr Speaker, Government expenditure is planned to be Tshs11, 112.419 billion (Tshs 11.1 trillion) for both recurrent and development expenditure. Expenditure will be financed through domestic revenue, domestic loans and external grants and loans.

  79. Mr Speaker, our Development Partners are expected to provide Tshs3, 274.553 billion (Tshs 3.27 trillion) to support our 2010/11 budget. Of this amount, Tshs 821.654 billion will be for General Budget Support and Tshs2, 452.91 billion (Tshs 2.4 trillion) will be grants and loans for development projects.

  80. Mr. Speaker, the Government intends to borrow Tshs 2,128.832 billion (2.1 trillion) from both domestic and external commercial sources. Of this amount, Tshs 797.62 billion will be for rolling over maturing Government securities and the remaining amount of Tsh 1,331.2 billion (1.3 trillion) will be used to finance the development projects.

  81. Mr. Speaker, the budget frame takes into account the expected outcomes of the tax measures that I explained above. The following table summarizes the budget frame for 2010/2011.

  BUDGET FRAME 2010/2011


  Revenue

  Shillings in Millions


  A

  Domestic Revenue


  6,003,590

  (i) Tax Revenue
  5,652,580

  (ii) Non Tax Revenue
  351,000

  B

  LGAs Own Source


  172,582

  C

  Foreign Loans and Grants- general Budget Support

  821, 645

  D

  Foreign Loans and Grants- Basket and projects

  2,452,908

  (i) Project Loans and Grants - 1,975,120

  (ii) Basket Loans and Grants - 477,788

  E

  External and Domestic Borrowing


  1,331,212

  F


  Domestic Borrowing (Roll Over)


  797,620

  G


  Privatization Proceeds


  30,000  Total Revenue
  - 11,609,557

  Total Expenditure

  H

  Recurrent Expenditure


  7,790,506

  (i) Public Debt
  1,756,044


  (ii)Ministries
  4,155,768

  (iii)Regions
  119,580

  (iv)Local Government Authorities
  1,759,114

  I

  Development Expenditure


  3,819,051

  (i) Local

  1,366,143

  (ii)Foreign
  2,452,908

  Total Expenditure
  - 11,609,557
   
 10. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #10
  Jul 1, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160

  Mmmmmhh huyo ndiye mkwere raisi wa Jamhuri wa Muungano wa wadanganyika 2005-2015
   
 11. m

  magee Senior Member

  #11
  Jul 1, 2010
  Joined: Jun 3, 2009
  Messages: 126
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  hapana!!!!!!!nooooo.......ntajiua mimi aibu,aibu kubwa mno........sitashuhudia uovu tena ndani ya macho yangu!!!!
  Embu tuungane tubabilishe hii....ibaki japo 2005-2010!inauma,inauma sana hali zetu zazidi kuwa duni hakuna tunachonufaika nacho zaidi ya sera mbovu.....uchumi kudidimia,mali za taifa kuzidi kugeuzwa mali za watu binafsi,madini yetu yanavyozidi kumalizwa bila maendeleo hata,uhuru wetu unavozidi kuondolewa....democracy inavozidi kubinywa.....it makes me sick!!!!!!
  I have nothing to luz......naamua kupambana............
   
 12. T

  The Informer Senior Member

  #12
  Jul 1, 2010
  Joined: Jun 14, 2010
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Duh, hii ni scandal kubwa! Imekuwaje wabunge makini hawakuona hii changa la macho. Hotuba ya Mkullo kweli inataja bajeti kuwa ni shs 11.1 trilioni halafu sehemu nyingine inasema ni shs 11.6 trilioni.

  Kwa kuwa Rais Kikwete amesema mwenyewe juzi kuwa bajeti ni 11.1 trilioni, hiyo shs 500 bilioni ya ziada iliyopitishwa na Bunge kwenye shs 11.6 trilioni IMEIBWA!
  Dk. Slaa na Zitto tunawaomba tafadhali sana mtupe maelezo, kwani nyie ni miongoni mwa Wabunge mliokuwepo wakati bajeti inapitishwa!
   
 13. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #13
  Jul 1, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Nakupongeza sana Fumbuka kwa umakini wako mkubwa wa kuweza kunotice haya mambo.

  Ujue watanzania tulio wengi huwa hatuna muda wa kusoma na kufuatilia kwa karibu mambo kama haya, na hao wabunge ndo siyo tegemeo maana wengi wao wanakwenda kule kupiga usingizi, au wapo bungeni kimwili lakini moyoni wanawaza majimbo yao.

  Hii ndo Tanzania bwana. Hiyo itakuwa imeingia kwenye kampeni, na mbaya zaidi bajeti ilishapitishwa.
   
 14. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #14
  Jul 1, 2010
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,656
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Ndugu usijaribu kutunga na ku-sensationalize mambo wakati simple reasoning inakwambia kuna tofauti kati ya kilichosemwa na kilichoandikwa kwa wino.

  Hiyo bajeti ya trilllioni 11.1 ushahidi wake unadai ni "Mkulo kasema" au "Kikwete kasema" wakati ile ya trillioni 11.6 ndiyo imeandikwa kwenye nyaraka zilizopo tovuti za MoF ( http://www.mof.go.tz/mofdocs/msemaji...%202010-11.pdf)
  na Bunge ( http://www.parliament.go.tz/bunge/docs/budget2010.pdf ).

  Ni wazi bajeti iliyopitishwa itakuwa ile iliyoandikwa kwenye hizo docs na siyo ile iliyotoka vinywani mwa Kikwete na Mkullo.
   
 15. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #15
  Jul 1, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Nasubiri ufafanuzi wa Dr Slaa na Zitto Zuberi Kabwe
   
 16. T

  The Informer Senior Member

  #16
  Jul 1, 2010
  Joined: Jun 14, 2010
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Acha kudanganya hapa.

  Wewe hauoni kuwa kuna utata mkubwa kuwa bajeti ya Mkulo kuna sehemu inasema ni 11.1 trilion/- na sehemu nyingine 11.6 trilion/-. Unataka kusema kuwa wananchi wapuuze kinachosemwa na kuandikwa na Rais kwenye hotuba yake kuwa bajeti ni 11.1 trilion/-. Nani mkubwa, Rais au Mkullo?

  Kama unapenda sana maandishi tafuta hotuba ya bajeti waliyogawiwa Wabunge June 10 na hotuba ya bajeti iliyochapishwa magazetini June 11 utaona bajeti inatajwa ni 11.1 trilion/-.

  Au wewe ni mmoja wa wale waliopewa mgao wa shs bilioni 500 zilizoibwa. Peleka huko sensation zako, ebo?!
   
 17. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #17
  Jul 2, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280

  Yaani na wewe ni mmoja wao. Swala siyo nani kasema nini, swala ni bejti ya serikali. serikali imetoa version mbili za hotuba ya bajeti. Version ya Kiswahili na version ya kiingereza. Ile ya Kiswahili inaonyesha hivi:

  [​IMG]
  [​IMG]

  Na ile version ya kiingereza inaonyesha hivi:

  [​IMG]
  [​IMG]
  Version zote mbili zimepitia bungeni kwa hiyo ni zote ni matamako rasmi ya serikali kuhusu bajeti ya mwaka 2010/11. Sasa maswali aliyotoa ndugu Fumbuka ni ya msingi kabisa, hiyo tafauti ya bilioni 500 imetokana na nini? Na matumizi halisi ya serikali yatakuwa ni yapi kati ya hizo takwimu mbjili?

  Ni jambo la ajabu sana kwa serikali yetu inavyoendesha mambo ya muhimu kama hili kienyeji enyeji namna hii. Siwezi kuamini kuwa serikali inaweza kufanya makosa ya kijinga namna hii. Inawezekana kuwa ni kosa la kupiga chapa lakini kama makosa ya namna hii yangekuwa kwenye mkataba na mwekezaji wa nje kuhusu kuchimba madini isingekuwa rahisi kuyasahihisha tena baada ya kutiliana sahihi.

  Serikali yetu haiko makini kabisa.
   
 18. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #18
  Jul 2, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Hivi mndhani tanzania kuna financial dicspline.
  Mpaka leo hatuna muundo stable ya wa serikali na wizara zake. Sitashangaa after october kuna wizara zitapunguzwa au kuongezwa.
   
 19. Questt

  Questt JF-Expert Member

  #19
  Jul 2, 2010
  Joined: Oct 8, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  They can come with typing error excuses on this saga......but yet still nobody is sure of which is the true value between the two...its election year and I dont trust these guys whenever it comes to Money......It shouldnt be EPA kind of thing........Otherwise this is too much
   
 20. C

  Chupaku JF-Expert Member

  #20
  Jul 2, 2010
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 1,045
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Lakini inakuwaje Wabunge wote wawe hawajaliona hili? Yani woooote? Haishangazi hata hivyo, maana wanatoroka sana sessions wako busy wanajiandaa na kura za maoni....
  Tunahitaji maelezo, na mabadiliko yafanyike. Hakuna utani hapa
   
Loading...