Kashfa Ktk NDOA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kashfa Ktk NDOA

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Bazazi, May 30, 2010.

 1. Bazazi

  Bazazi JF-Expert Member

  #1
  May 30, 2010
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 2,029
  Likes Received: 560
  Trophy Points: 280
  Tafadhalini sikieni hiki kisa!!!!!!!!!!

  Mama alikuwa na watoto watatu na hana MUME (single parent). Mtoto wa kwanza ni wa kiume na ana baba yake, wadogo wawili ni wa kike na wana baba yao. Mama kawasomesha watoto wake vizuri kwani wote wana shahada za uzamili (Master Degrees) ktk fani tofauti-tofauti.

  Kaka alioa mdada BONGO FLAVOUR na mapenzi yao yalikuwa mazuri sana hadi pale walipogombana na mke kuamua kumkashfu (labda kumweleza ukweli), kashfa aliyodhani kuwa itamuumiza mwenzake hadi kumoyo na maini. Mke alimwambia mume "tatizzo la watu ambao hawakulelewa na kina BABA wanaoeleweka hawajui mapenzi kabisa, hata uwafanyie nini hawawezi ku-appriciate.

  Mume kusikia hivyo aliamua kutofanya lolote zaidi ya;
  -Kumuachia gari la kuendea kazini ya yeye kuanza kupanda dalala.
  -Kula chakula nje ya nyumba yao ingawa nyumbani wanapika
  -Hela ya chakula na matumizi ya nyumbani inaachwa kama kawaida
  -Hakuna maongezi wa mama yake maongezi
  -Wanalala kitanda kimoja lakini hakuna mawasiliano yeyote
  -Mke haruhusiwi kumfanyia mume vitu ambavyo katika hali ya kawaida anatakiwa kuwa anamfanyia kama kufua na kupiga pasi. Mume alikuwa akifanya mwenyewe au kwa dobi na vitu kama hivyo.

  Mke alianza kupungua kwa mawazo na kujaribu kumrai mume wake amsamehe lakini mume alikuwa mara zote akigoma. Mambo yalipochacha mke alijifunga kibwebwe na kumvaa mama-mkwe na kumuelezea kila kitu. Bahati mbaya mamamkwe naye akija juu kwa kutukanwa kuwa ni malaya na hivyo kumfukuza na kutomsaidia mkamwana wake.

  Mke aliamua kufunga safari kwenda Dodoma kwa Mjomba mtu aliyekuwa anasimama kama Baba na alimuaga mume wake na kupatiwa nauli ya kwenda huko. Ashukuriwe Mungu kwani Mjomba alikuw mwelewa na kukubali kumsaidia mkamwana wake. Mjomba aliongea na dadaye na kuyaweka sawa kabla ya kumvaa mume mtu.

  Wanandoa hao kwasasa amani imerejea ktk nyumba. Tatizo ni kuwa haijulikani kama kweli amani hiyo ina upendo ule wa awali. UPENDO ILHALI WEWE NI MWANAHARAMU?

  NB: Hamna kitu kibaya ktk ndoa kama kashfa; bahati mbaya dada zetu sababu ya kujua kuongea kuliko waume zao wamekuwa na kauli chafu na bila kuzifanyia kwanza uchambuzi kujua athari zake.

  Wana-JF tuchangie mada hiyo ili tujaribu kuwekana sawa ktk tasnia nzima ya ndoa na mahusiano kwa ujumla.

  NAwasilisha.
  Bazazi wa Mbazazi ktk Ubazazi
   
 2. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #2
  May 30, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  nimeipenda sana hii maada, so i'll be back as soon as possible,
  asnte sana mkuu, haya ndiyo mambo muhimu yanayotunguka kama jamii
  hivyo ni muhimu mno kuyadadavua
   
 3. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #3
  May 30, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Pengine mzee usidhnai kashfa zipo kwa upande wa wake zetu tu. Hata sie wanaume mzee tunaongoza kwa kashfa hususan pale ugomvi unapokuwa hauna kichwa wala shingo katika familia.

  Ni sawa kuwa kina mama nyenzo yao kubwa katika ugomvi ni maneno na mara nyingi utumia yale ambayo yanaweza kukufanya upunguze kasi au kughazabike zaidi ili anonekane mshindi, lakini tukubaliane japo wengi wanaweza kupinga kuwa ugomvi wake na munme siku zote utawaliwa na "domination ya Mwanaume" kwenye kila kitu. Hii inaweza kujidhihirisha hata katika mada uliyoileta kuwa japo Mke alimtamkia Mumewe mijineno ya kashfa na dharau, laini aliendelea kutimiza wajibu wake kama kawaida, kupika, kumwandalia mumewe kila kitu lakini Mume hakuwa tayari kupokea hayo na kusahau mpaka mtu wa pembeni alipokuja kumshauri (mjomba).

  Huyo Mume kwa upande mwingine anaweza kuwa ni "dikteta" kwa mkewe kwani inaonekana alishindwa kupima maneno yaliyotolewa na mkewe kwenye ugomvi na yale ya kawaida ambayto yanaongelewa kila siku. Labda ingempasa pia kujua kuwa kile alichoambiwa ni hali halisi lakini na angetafuta wasaa wa kumtaka mkewe asibitishe kama alidhamiria kumtusi au ni hasira tu za ugomvi na sio kuzila kabisa kana kwamba hataki tena kuendelea na huyo mke. Maneno ya kqwenye ugomvi wa watu wawili ni nguvu kupima kwa akili ya kawaida, kwani yanasukumwa na hasira na ghazabu..pengine hata ya kuambiana ukweli ilimradi tu kujaribu kupunguza moto japo pengine ndo unauwasha zaidi..yote ni hasira na siku zote hasira ni kama ajali, haina kinga na ndio mana wakasema hasira hasara!!.

  Katika maisha ni vyema kujifunza kuwa watu huwa wanaona tofauti zilizo kwa wenzao kuliko zile walizonazo wao. Mtu mwenye mapungufu ukimwambia anamapungufu inaweza kuwa ndio mwanzo wa kukorofishana kuliko kumwambia ajaribu kurekebisha lile ambalo unaona halikuridhishi au haliendani na hali halisi (japo ukiwa una maanisha kitu kile kile kwa matamshi yaliyotofauti na kumkemea).

  Haifai sana kujenga kisasi cha jinsi hi kwa wanandoa hata kama umetukanwa. Cha msingi ikiwa mwenzio amejawa na kiburi na kinywa cha Kashfa, ukifahamu, ni heri kumkarisha chini na kumweleza kuwa hiyo tabia yake haikupendezi na kamwe haiwezi kuvumilika na mtu mwingine yeyote (Umkemee kwa nguvu aache hiyo tabia) na sio kuzila kabisa huduma zake au kuweka moyoni jambo kana kwamba hakuna tena uhusiano nae. Hakuna dhambi isiyo sameheka hapa duniani, ukiwa mtu wa kuzilazila hovyo, utakufa mapema na yeye kumwacha watu wakidunda nae.
   
 4. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #4
  May 31, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  icho ni moja ya vitu vibaya sana mtu anaweza kuongea...ni tusi kubwa sana kwa mamangu kama ndo mimi, na anakuwa ananionea kwasababu mimi kama mtoto sina hatia, nilijikuta nimezaliwa hivyohivyo, so inauma sana kwakweli. however, kila jambo hata kama linauma kiasi gani, tunatakiwa kusamehe, kwasababu kama hatutasamehe wenzetu na Mungu wetu hatotusamehe sisi makosa yetu...vilevile tunavyowaumiza wenzetu mioyo, tunamwumiza Mungu wetu kila siku zaidi ya hapo lakini yeye Mungu anatusamehe tukimrudia.

  kwa kifupi, uyo kaka anatakiwa awe mwanaume mwenye kifua cha kutapikaa uovu, amsamehe kikwelikweli, kwasababu kama hata msamehe, hata maombi yake yeye hayatajibiwa mbele za Mungu...na yeye akimkosea Mungu dhambi basi Mungu hatamsamehe. kwa wanandoa wengine, naomba tuwe makini, tuwe na hekima, ukweli siku zote huwa unauma, so unapoongea jambo linalolenga kwenye ukweli bora kwenda kwa hekima na busara sana. sio kwenda kwa kawadia.
   
 5. doup

  doup JF-Expert Member

  #5
  May 31, 2010
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 1,172
  Likes Received: 335
  Trophy Points: 180
  Jamani tunaweza kupata list ndogo ya viji-kashfa; wengine wanaweza kuwa wanaongea maneno bila kujua kwamba ni kashfa na yanawakwaza wenzi wao
   
 6. Lisa

  Lisa JF-Expert Member

  #6
  May 31, 2010
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 1,568
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  :target: Heheheheheeheheeeeeeeeeeeee! Mkuki kwa nguruwe! Maana naona jamaa aliumia mpk maini yakatikisika . pole sana ila nyinyi wanaume huwa mnatukashfu sana wanawake na bado tunawavumilia na hatuwasusii na Sakalamenti Takatifu tukiwa madhabauni tunawapa. ila nyinyi mkusemwa kidogo tu mnanuna . Tena mnatoa makashfa sana. Mf wewe nn nimekukuta mteremko kama kwa sadala. lkn mtu unanyamaza na hununi ila yy kuambiwa mtoto HARAMU TU ANANUA. Poleeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee! Mwayaaaaaaaaaaaaaaaaaa!
   
 7. T

  Tall JF-Expert Member

  #7
  May 31, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  1.KATIKA NDOA...WAZAZI NI SENSITIVENOBS.HUGUSWA KWA UANGALIFU MKUBWA.
  2.ELEWA HISTORIA YOTE YA WAZAZI WA MWENZIO HILO SI KOSA.HISTORIA HIYO ITAKUSAIDIA KUISHI NA KUMWELEWA MWENZIO
  3.YALE UNAYOONA MAZURI SIFIA SANA.
  4.UNAYOONA HAYAJAKAA SAWA KAA KIMYA USITOE COMMENT YOYOTE IWE KIUTANI AU LA.
  5.KUMBUKA KWA KUSEMA NENO LOLOTE BAYA KUHUSU MZAZI WA MWENZIO WEWE KAMA MKWE NI TUSI
  6.SISI KWETU HAKUNA ANAEHESHIMIWA DUNIANI KAMA MKWE,EBO kakuletea mwenzi ati!!!!!!.
  7.Kama mzazi wa mwenzio angekuwa na tabia mbaya usingemfuata mtoto wake.Maana mtoto wake ulie nae ni yuleyule mzazi wake.
  8.Kumdharau au kumsema vibaya mzazi wa mwenzio ni kujitafutia laana ya bure.
  9.Huyu mke kafanya kosa kubwa sana sana,ni sawa jamaa alivyochuka hatua......
  nasema hivi? HATA SIKU MOJA ISIJETOKEA UKAMDHARAU,KASHIFU,KEJELI AU FANANISHA TABIA YOYOTE MBAYA YA MZAZI WA MWENZIO.HATA AKIFANYA/DHAMBI AU KOSA GANI.....WEWE NYAMAZA TU VINGINEVYO UTAHARIBIKIWA.
   
 8. Bazazi

  Bazazi JF-Expert Member

  #8
  May 31, 2010
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 2,029
  Likes Received: 560
  Trophy Points: 280
  He da'Lisa habari za Machame na Hai kwa ujumla, siye wazururaji hatujambo na tunatarajia kuzungukia maeneo hayo hivi karibuni.
   
Loading...