Kashfa Bandarini Dar: Rais Magufuli amsimamisha kazi Kamishna Mkuu wa TRA, Rished Bade

Mkuu nimekuelewa vizuri sana, lakini kwanini toka alipoingia madarakani mpaka sasa yeye kama kiongozi ameshindwa kutumia madaraka yake na kufanya maamuzi magumu ya kufukuza wale wazembe wala rushwa na kukata mirija yote inayoitia nchi hasara? Pia kuonyesha kwamba kweli yeye ni tofauti na waliomtangulia? Lakini kama kashindwa kufanya hayo na madudu ya huko tra yanajulika kwa muda mrefu sana basi anapaswa kutimuliwa.

Kilichopo, inawezekana ndugu Bade aliona ubadhirifu, pengine angeweza kumfukuza kazi mtu wa chini yake. Lakini issue inakuja uliyemfukuza kazi akishinda mahakamani unatakiwa umlipe fidia. Kwa ujumla kuchangia humu mitandaoni ni rahisi lakini maamuzi ya kumsimamisha au kumfuta kazi muajiriwa kufanywa kwa level ya Kamishna inatakiwa umakini wa hali ya juu. Mfukuzwa kazi akishinda kesi mahakamani ukimlipa itatajwa umeisababishia hasara serikali. Kwa wakuu kama Rais na Waziri Mkuu ni rahisi kutoa amri na ukasimamishwa mara moja. Kwa hilo la Bade kushindwa kumuwajibisha mtumishi wa chini yake siyo jepesi sana. Labda tuseme ni ule uzembe wa kutojua idadi kamili ya Makontena yaliyopotea nalo ni uzembe wake kwa sababu idadi aliyoitaja Mh Waziri Mkuu ni kubwa kuliko Takwimu za Bade
 
Huyu mtu ulikuwa ni mpango wa Mungu kulikomboa taifa letu,hii mijizi imefilisi taifa huku walala hoi wakiteseka na wengine wakipoteza maisha kwa kukosa panado.
Kwa spidi hii anaweza funika hata uongozi wa nyerere tunakuombea mr.pombe Mungu akupe ujasiri na moyo wa huruma kwa sisi vidudu mtu tunaoteseka ndani ya inchi yetu na ikiwezekana wengine uwatangurize kwetu pazuri wakaisome namba kule maana ni mizigo ktk taifa hili lenye kila kitu lkn masikini la kutupwa.
 
Mashirika ya UMMA yanalipa vizuri Sana ndo maana vigogo wengi Wa serikali ya awamu ya nne wamejaza watoto na ndg zao huko. Bila kimemo cha mtu mkubwa hulambi kazi huko utaishia kusindikiza kwa kufanya written interview. Wengi wamejaa TRA, NSSF, LAPF, PSPF Tanesco, NHIF nk. Ukimkuta mtoto wa kigogo kwenye mashirika Kama ya USAID, UN basi Huyo hata kichwani yupo vizuri
 
Jitahidi mzee isiwe ni nguvu ya soda,bado tunakuangalia..
Maliasili na utalii nako kumeoza balaa vamia pale!!
 
Ben kaja na uchaga we umekuja na udini! Huu mtandao wa Minywele lazima ufyonzwe ndio uliompa kiburi, Uislam sio kichaka cha ufisadi, ya wachaga namuachia ben!

Haya yanahusikaje na maamuzi ya rais. Watanzania tuepuke sana hizi hisia au chuki za kidini, kikabila au ukanda. itafika mahali sasa kiongozi mkuu ashindwe kufanya maamuzi chanya kwa faida ya nchi kwasababu ya wananchi kuweka mbele hisia za kidini, kikanda au kikabila. Ndugu Muombe sana Mungu wako akusaidie kuepuka hisia za ubaguzi wa aina yoyote ndani yako. kama kuna mbegu ya ubaguzi wa aina yoyote ndani yako ninamuomba Mungu ninayemuamini aing'oe ndani yako apande mbegu ya UPENDO kwa watu wote na AMANI WATANZANIA NI WAMOJA NA KAMWE HATUTAGAWANYIKA KWA MISINGI YA UKABILA, UDINI AU UKANDA. MUNGU IBARIKI AFRIKA MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Kilichopo, inawezekana ndugu Bade aliona ubadhirifu, pengine angeweza kumfukuza kazi mtu wa chini yake. Lakini issue inakuja uliyemfukuza kazi akishinda mahakamani unatakiwa umlipe fidia. Kwa ujumla kuchangia humu mitandaoni ni rahisi lakini maamuzi ya kumsimamisha au kumfuta kazi muajiriwa kufanywa kwa level ya Kamishna inatakiwa umakini wa hali ya juu. Mfukuzwa kazi akishinda kesi mahakamani ukimlipa itatajwa umeisababishia hasara serikali. Kwa wakuu kama Rais na Waziri Mkuu ni rahisi kutoa amri na ukasimamishwa mara moja. Kwa hilo la Bade kushindwa kumuwajibisha mtumishi wa chini yake siyo jepesi sana. Labda tuseme ni ule uzembe wa kutojua idadi kamili ya Makontena yaliyopotea nalo ni uzembe wake kwa sababu idadi aliyoitaja Mh Waziri Mkuu ni kubwa kuliko Takwimu za Bade

Kwa hiyo inajenga hoja kwamba mtuhumiwa wa uzembe na kutowajibika asifukuzwe kazi kwa kuogopa huenda ataenda mahakamani na kushinda kesi!!!!!
 
Kwa hiyo inajenga hoja kwamba mtuhumiwa wa uzembe na kutowajibika asifukuzwe kazi kwa kuogopa huenda ataenda mahakamani na kushinda kesi!!!!!

Uteuzi wa rais au kutenguliwa kwa uteuzi wa rais hauhojiwi mahakamani. Nafasi zote za uteuzi zikitenguliwa huwezi kukimbilia Mahakamani.
 
Hapana! This is extremely wrong! For those of us who know Bade- this is wrong starter. Magufuli needs the kind of Bade for his crusade. Bade is being victimised for wrongs that he might not be part to them. Huyu ni mchapakazi, msomi mstarabu asiye na papara, mtaratibu. Amechukua TRA juzi juzi tu baada ya kustaafu Kitilya. Bandarini ndiko Customs na Bosi wa Customs ni Kamishna wa Forodha angeanza na huyo, na akamtumia Bade kusafisha uozo wa TRA.

Kumteua anayemjua Bade kwa ujuzi na weledi wake wa kazi ni kujenga mazingira ya hofu tu na utendaji wa kazi katika hofu bila kujiamini utatuletea shida. Please Your Excellency take heed! Usifanye hasira, twende taratibu Rais wangu upige vita ya kushinda sio ya kuviziana haitaisha!

Unasema unamjua bade lakini nina mashaka sana. Kwa mtu yeyote ambaye yupo kwenye sekta ya benki atajua kabisa kwamba bade ni chief non-performer. Wengi tulishangaa alivyopewa hiyo post ya commissioner-general wa TRA. Hivi hukumbuki alivyoboronga Barclays? Wakati akiwa pale zilipigwa hela mpaka benki ikataka kufungwa. Bade huyo ndio unamuita "mchapakazi"?
 
leo nilikuwa benki ya equity walikuwepo watu kama wa tatu hivi, watanashati kweli........wakiongelea speed hii ya mheshimiwa ,wakasema kwa speed hii, ni lazima wazee watamwita wamukanye, na asione hawajasema kitu, wako wanatunga sheria,,,,,,,,,,,,,,walionekana wazi kabisa hawana raha,,,,,,mmoja wao kasema,,,alaaaa haiwezekani watu uwazuie kwenda ulaya na wameishazoea kwenda.......nikajua hapa dawa imeanza kuwaingia kidogo kidogo.
 
Back
Top Bottom