Kasheshe vituko na vitimbwi vya mimba

Naomba kuuliza wadau hivi ile story ya mwenzetu mmoja rafik yake alivozalishwa hospitalini na dokta wa kiume halafu akamzimia sana dokta hadi akawa analia kua anampenda sana na ilihali ana mme wake ...imekuwaje ??
Mh hii sijaisikia bado hebu nipe link yake
 
Mh hii sijaisikia bado hebu nipe link yake
Ngoja niitafute mkuu....huyo dada ambae ndo best yake huyo mwanamke hakurud kuttupa mrejesho kwamba ilikuwaje. Sasa sjui ndo hizi dalili kuna wakat through pregnancy na kuna zile baada ya kujifungua sjui wanaitaje kitaalamu.
 
Omba sana Mungu mimba ya shemeji isiangukie kwenye kupenda vitu kama hivi
1469169026359.jpg
1469169036056.jpg
1469169045866.jpg
1469169054615.jpg
utatoboa kibubu nakuapia, ikishanasa tu omba apende vitu vya chukuchuku na achukie nyama choma na roast na tuskeri barrrid sana . ...yani awe mpenzi wa bamia mlenda na ugali wa muhogo daily
 
Acha kabisa hii maneno
Kuteseka ni lazima kwa mama hata kwa baba pia
Huruma zaidi huja pale mimba inapomgeukia baba na kuwa kama yeye ndio kaibeba! Yaani vichefu chefu vyote yeye malimao mbilimbi na ubuyu ni yeye. .huwa inatia huruma mno

HII IMESHANITOKEA AUGUST 2010 - APRIL 2011, USIOMBE MWANAUME IKUPATE! NILIKUWA NATEMBEA NA NDIMU AU LIMAU KWENYE SURUALI.


-mkeo anaweza kupoteza hamu kabisa ya tendo la ndoa!

NDIYO MTIHANI WANGU WA SASA!

Nitaongeza uvumilivu!
 
Dhu! Jana nimetibuana na mke wangu na ni mjamzito. Kumbe kile kisirani na hasira yawezekana sio kile kiburi chake cha kila siku. Hata kabla ya mimba hua ana kiburi sana. Muda mwingi nashindwa kutofautisha kiburi chake cha asili na kile cha mimba. Nitaisoma namba mwaka huu.
 
Ah mie embe hapana nilikuwa napenda ubuyu..... Kipindi hicho ofisi iko karibu na imalaseko supermarket.....asubuh napitia ubuyu wangu....unaliwa mpaka nikitoka. Napitia pweza na supu yake....nikifika nyumbani barafu natafuna mpaka meno yanakufa ganzi......ila sasa haya yote siwezi kuyafanya....mimba kiboko.....
mimi nilidhani ubuyu wa instagram!
 
Mi mke wangu alikuwa ananipenda mimi kiasi kwamba hataki niende hata kazini. Na jioni nisiporudi mapema hari. Sku izi ameacha.
 
Mimba acheni tu.....me zinanipa kisirani na hasira za kufa mtu....pia nmetokea kuwachukia Sana wanaume na nnahasira nao balaaaa
 
Back
Top Bottom