KARUME yuko LONDON kisiri siri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

KARUME yuko LONDON kisiri siri

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Game Theory, Apr 30, 2008.

 1. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #1
  Apr 30, 2008
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Ujumbe wake mzio ulijaa kwenye BA iliyoingia jana hapa London. Tatizo ni kuwa sielewi kaja kufanya nini na kwa manufaa yanani

  au

  Inawezekana kaja kufanya medical check up maan watawala wetu hawaiamini Muhimbili
   
 2. MwanaHabari

  MwanaHabari JF-Expert Member

  #2
  Apr 30, 2008
  Joined: Nov 9, 2006
  Messages: 444
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  huyu ameanza kuwa kama muungwana....hawamwambii mtu sikuhizi
   
 3. N

  Nyerererist JF-Expert Member

  #3
  May 1, 2008
  Joined: Oct 1, 2007
  Messages: 443
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  mie nadhani amekuja kuhamishia hela zake Swansea maana kisiwa cha Jersey kimeshafahamika na sasa wengi wanahaha huzihamisha pesa zao kabla umma hauja waumbua....au amekuja shoping M&S? kazi ipo
   
 4. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #4
  May 1, 2008
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,918
  Likes Received: 219
  Trophy Points: 160
  Wataiamini vipi wakati wanajua ukweli wote kuhusu Hospitali zetu kuwa fedha za kununulia vifaa zilikwenda kwa Mhe. Fulani na madawa yanayoingizwa nchini yamenunuliwa kwa bei nafuu baada ya kuisha muda wake. Pia wanajua kuwa Madaktari wetu hawakawii kuconfuse na kukupasua kichwa wakati una tatizo la mguu na yote inasababishwa na ukata unaowachanganya akili kwa kulipwa mishahara midogo na kufanyisha kazi katika mazingira yasiyoridhisha huku wachache wakiifaidi nchi.

  Huo ndiyo ukweli Mr. GT, Muhimbili wanakwenda wale wasio na uwezo wa kusafiri kutibiwa nje.
   
 5. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #5
  May 1, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Umetonesha kidonda!

  Dunia ilishangaa, na kuna watu hatujamsamehe, Julius Nyerere kwa kufia London!

  Angekufa Mwaisela kusiko na vitanda, Bugando japo sio hospitali kwa sababu hakuna waganga wala dawa. Kwa utashi wa Taifa, angefia juu ya sakafu, bila chandarua, kwa sababu ndivyo watu wake walivyo kufa leo hii KCMC Moshi. Wamelazwa kwa maumivu ya kichwa wakafa kwa Malaria waliyo ipata hospitali.

  Tungemwita Gandhi. Tungemwita Mandela, tena angemzidi Mandela aliyesifiwa na wazungu kwa sababu tu hakuwawashia moto alipo pata Urais. Na wengine wangemwita Mtakatifu!

  Baba wa Taifa, uliye pinga kutegemea mabeberu, ukawakatalia Wajerumani walipotaka kununua Zanzibar kwa misaada ya Umeme! Kwa nini ufie London? Kwa nini Baba?
   
 6. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #6
  May 1, 2008
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  kaja kisirisiri ama amekuja tu. umepiga simu State House ZNZ ukadanganywa au kukataliwa kuambiwa alipo...LOL
   
 7. MwanaHabari

  MwanaHabari JF-Expert Member

  #7
  May 1, 2008
  Joined: Nov 9, 2006
  Messages: 444
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  siyo kosa lake kutibiwa huko kwani specialists wa lukemia walikuwa huko (hakulipia yeye mwenyewe) halafu kumbuka Mwalimu aliondoka Urais 1985 -----thats 23 yrs ago, kusema watu wanakufa kcmc leo ni kumuonea...kama sisi wenyewe tumeshindwa kujiendeleza miaka 23 mpaka leo, tujilaumu wenyewe
   
 8. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #8
  May 1, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,607
  Likes Received: 82,181
  Trophy Points: 280
  Mwalimu Nyerere, Mwenyezi Mungu amlaze mahali pema peponi~AMEN kwa jinsi alivyoitumikia Tanzania kwa mapenzi ya kweli bila kufanya ufisadi na kujilimbikizia utajiri alikuwa na haki ya kutibiwa katika hospitali yoyote ile duniani yenye mabingwa wa kuweza kumponya na Watanzania wengi hatutalalamika kwa hilo, lakini hawa mafisadi hatutakuwa tayari kuona fedha za walipa kodi zinatumika kwa matibabu yao
   
 9. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #9
  May 1, 2008
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  angekufa Mnazi mmoja kama alivyokufa Rais wa kwanza wa Zanzibar, na Mh I drissa Abdul wakil
   
 10. MwanaHabari

  MwanaHabari JF-Expert Member

  #10
  May 1, 2008
  Joined: Nov 9, 2006
  Messages: 444
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ili iweje, hao walikuwa wanaumwa same conditions kama mwalimu?
   
 11. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #11
  May 1, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Umekosa pointi yangu. Watu wake walikuwa hawapati hao specialists. Au yeye alituendeleza sisi tukarudi nyuma?. Na hata siku aliyo kufa miaka 14 baada ya utawala wake wa miaka 24 bado nchi ilikuwa iko reeling from his leadership. Kumbuka Nyerere ndio Muasisi wa nchi yetu na yanayo tokea leo baadhi yake yana mizizi ya uasisi wake. Huwezi ukamtenganisha nayo. But that’s besides the point. Pointi yangu ilikuwa sio kuhusu ufanisi wa Nyerere.

  Na mimi nasema AMEN. Na uadilifu wa Mwalimu hauswalishiki. Na wala haujaswalishwa hapa, kwa hiyo sio ishu. Na hata ingekuwa ndio ishu, kuwa mwadilifu ndio wajibu wake. Tunapopima uongozi wake hatuwezi kumuweka Chenge na Lowassa kwenye upande mwingine wa mzani. Off course ataonekana Mtakatifu kwa sababu umesha lower the bar chini mno.

  Pointi ilikuwa kwamba, Nyerere alikuwa ni alama ya Kujitegemea, pamoja na Usawa wa Binadamu. Kufia hospitalini London kumepunguza hiyo stature kwa sababu watu alio kuwa anawaongoza hawapati hiyo bahati ya access to healthcare kama yeye aliyo ipata kama kiongozi siku alipo kufa. Ile alama ya kuwa “Mtu wa Watu’ inaharibika kidogo. Pili, yeye alisimama kama alama ya kukataa kuburuzwa na wenye nguvu kwa kigezo cha misaaada. Alihubiri kujitegemea, hivyo anapokufa kwenye mikono ya Madaktari wa ‘Mabeberu’ inapunguza hiyo stature yake. Ni kweli mtu yeyote ana haki ya kutibiwa mahali popote pale duniani, lakini Nyerere anapimwa na mizani tofauti, mizani iliyo kuwa more exacting, kutokana na Stature yake na vitu alivyo vihubiri. Ndio maana nikasema, angefia Tanzania tungemwita Gandhi, mvaa Khanga.

  Mwisho, Bubu unasema Watanzania hatumlaumu Nyerere kwa hilo. Hata mimi ni Mtanzania! Sababu ya kuwa na vast majority ya Watanzania kuto kumlaumu kwa hilo ni kwamba bado hatujapevuka katika uhuru wa kuwachambua waasisi wa nchi bila kuonekana unawapinga. Editorials nyingine duniani zili swalisha contradiction ya mazingira ya kile kifo and what Nyerere stood for. Bongo hakuna Editor wa kuchambua vitu kama hivyo. Ataonekana ana chuki binafsi na Nyerere, kama mnavyo dhani ndio kiini cha maoni yangu. I can tell kwa sababu mnaharakisha kumtetea katika vitu ambavyo sijavikosoa. Ahsante.
   
 12. Gamba la Nyoka

  Gamba la Nyoka JF-Expert Member

  #12
  May 1, 2008
  Joined: May 1, 2007
  Messages: 6,594
  Likes Received: 6,755
  Trophy Points: 280
  dah kuhani mkuu, hapana bwana, hii haikubaliki mzee. tiba ni tiba, mgonjwa ni mnyonge na ponyo ndo tumaini lake, huwezi kumlaumu mgonjwa kwa kuitafuta dawa kule iliko.
  Nimepata kukutana na watoto kwenye ndege wanapelekwa israel kufanyiwa matibabu ya moyo kwa gharama za serikali, je tuwalaumu waliopitisha sera hiyo ya kusaidia wagonjwa kutibiwa nje?,eti kwa vile hawajatosheleza hospitali za nyumbani?

  Unathubutu kweli kuwaita wale waliojitolea kumtibu Mwalimu katika hospitali ya saint Thomas bure "mikononi mwa mabeberu".

  mimi sasa nashawishika kwamba huenda sera ya mwalimu ya usawa,ujamaa na kujitegemea huifahamu vizuri, mwalimu alikuwa anaamini hivi "Binadamu wote ni ndugu zangu na afrika ni moja".

  alikuwa tayari kupambana na Fisadi mweusi(mfano nduli Amini) na pia kupambana na fisadi mweupe(mfano kaburu) au rangi yoyote ile. na alikuwa tayari kuwa rafiki na yeyote yule ambaye ana misingi ya utu. sasa ndugu yangu unashangaa kweli mwalimu kufia ulaya?,
   
 13. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #13
  May 1, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Kamanda, hapo juu umemaliza mjadala wa Mwl.Nyerere!
   
 14. M

  Mwakilishi JF-Expert Member

  #14
  May 1, 2008
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 484
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Chonde chonde Kuhani Mkuu akikusikia Mzee Mwanakijiji unamsema Nyerere patakuwa hapatoshi hapa... :)
  Lakini on a serious note, I wouldn't fault Nyerere for seeking medical help and eventually dying huko kwa "mabeberu", I mean when it comes to survival, our basic instincts as humans(animals if you like) is to do all in our power to survive hata ikibidi kwenda kwa "beberu". No wonder tuna ile methali isemayo "baniani mbaya (lakini)kiatu chake dawa"!
   
 15. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #15
  May 1, 2008
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  mdabwado! huna jipya, bado mchovu kufikiri
   
 16. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #16
  May 1, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Tatizo lako una chuki binafsi, na huna hoja ya kutoa....
   
 17. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #17
  May 1, 2008
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,275
  Trophy Points: 280
  Kwa hio unamaanisha kwamba kama binadamu wote ni ndugu? Mbona kama ni hivo basi hata wale ambao ni MAFISADI kwa sababu ni ndugu basi tuendelee kuwachagua na wale maskini wa kutupwa waendelee kula mlo mmoja kwa siku na kutembeza godoro toka tandika mpaka Kariakoo na asipate mnunuzi huku wengine wakifaidi matunda ya uraia wa Tanzania?

  Hii yote ni siasa ndugu yangu. hayati Mwalimu alikuwa ni miongoni wa "elites" watu wenye uswahiba na mabepari lakini kwa mtindo wa aina yake ambapo mtu asiekuwamo humo hawezi kuelewa.

  Ukisoma kuhusu vita baridi iliyoanza mwishoni mwa miaka ya sitini mpaka mwanzoni mwa miaka ya themanini na kuilewa yote ndio utajua kuwa Afrika hatuna watu ambao wewe tunawaita ndugu na kwamba eti Afrika ni moja.

  Je unajua ni sababu zipi hasa zilimfanza Idi Amin amchokoze hayati Mwalimu? na ni nani walimsaidia Amin kuwa kiongozi wa Uganda? Nenda kasome tena na uchambue historia halafu utaniambia.

  Afrika sio moja kwa kuangalia mifano ya nchi kama za Botswana, Namibia, Mozambique zenye kuonesha kwamba zina uwezo wa kuajiri na kuwajali madaktari wa Tanzania.


  Lakini tutaendelea kuwa wajinga kwa kuendelea kufikiri kwamba viongozi tunaowachagua ni wale wenye nia njema za kuendeleza jamii ya watanzania kwa kuhakikisha tunafanza hata nusu ya hawa waliotangulia kimaendeleo kwa kuwa na hata hospitali moja yenye specialists wa kila ugonjwa na vifaa vya kisasa kama X-Rays, UltraScans na vingine.

  Kwa mfano Ultrascan inasaidia kujua ni sehemu gani katika mwili pana uvimbe au damu imevia kwa muda mfupi mno,na mengine ambapo ndio unaambiwa eti mzee kaenda kuangaliwa afya yake.

  Sasa kama hatuwezi kuwa na Ultrascan za kutosha katika nchi yetu ndio hivo tena tunabaki tukishangaa watu kwenda majuu kwa uchunguzi wa kiafya.

  Kwa hio nahitimisha kwa kusema kwamba kitendo cha "elites" wa Tanzania kwenda Ulaya kwa matibabu na kutumia "change" inayobaki kupeleka baadhi ya wagonjwa nchini India na kwingineko kwenye bei nafuu, sio kibaya kwani hatuna "specialists" wa magonjwa hayo.
   
 18. M

  Mafuchila JF-Expert Member

  #18
  May 1, 2008
  Joined: Apr 29, 2006
  Messages: 752
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Hivi umesahau kuwa Idris Abdul Wakil, alikuwa London kwenye matibabu kipindi kile kile ambacho JKN alikuwa hapo London?
   
 19. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #19
  May 1, 2008
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0

  Tafadhali kwa khisani yako nakuomba umwache huyu Idrissa kama alivyo.
   
 20. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #20
  May 1, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Ukiuona huu ni 'mjadala wa Nyerere' basi lazima utaisha kabla hata haujaanza kwa sababu watu wamesha chagua upande.

  Nilipokuwa mdogo, wakati nina nguvu za kubishania Simba na Yanga, nilikuwa naenda kijiweni kuitetea Simba no matter what was going to be said in favor of Yanga. Nikiwa njiani, hata kabla sijafika kijiweni, ninajiandaa na pointi za kuitetea Simba, hata wakati Simba imefungwa na Yanga jana usiku.

  Kwenye 'mjadala wa Nyerere' bahati mbaya ni kama wa Simba na Yanga. Hilo jambo, Kibunango, linatufunga kamba mawazo, kwa sababu huwezi hata siku moja ukaangali upande mwingine wa Shillingi. Ni katika kujifunza zaidi, huyu kiongozi aliye tukuka, alichemsha mahala fulani?

  Sio 'mjadala wa Nyerere' hata kidogo, Kibunango. Nyerere, mimi siwezi kufunga kamba za viatu vyake. Na ninakuwa mwangalifu sana ninapo mkosoa. Yanga nawakosoa hata wakipatia!
   
Loading...