The Phylosopher
JF-Expert Member
- Mar 11, 2015
- 2,352
- 3,600
Rais Magufuli yupo nchini Rwanda akihudhulia maazimisho ya kumbukumbu zoa mauaji ya Kimbali yaliyotokea 1994. Ni kitu kizuri kinachoenesha mshikamano na jirani zetu kuonesha jinsi gani tumeguswa na maafa hayo makubwa.
Ikumbukwe pia leo ni maazimisho ya kumbukumbu ya kifo cha mmoja wa waasisi wa Taifa hili hayatiMzee wetu mwanamapinduzi Abeid Aman Karume.
Swali kwa Watanzania ni kwamba event ipi ni muhimu Kitaifa kati ya hizo mbili? Je haikuwa muhimu sana kwa Rais kuwa Zanzibar na kushirikiana na Wanzanzibari kuazimisha kifo cha Karume?
Je, ingekuwa kifo cha Nyerere, Magufuli angekwenda Kigali?
Mimi binafsi, msimamo wangu ni kuwa Rais amekengeuka. Natoa hoja.
Toa fikila za kibaguzi, bado muunguno ni hazina kwa tanzania wazungu wamejaribu kuua huu muungano lakini weshindwa. Yule mzee alikuwa na akiri sana.Naunga mkono hoja ifutwe tu maana hakuna alichofanya huku tanganyika
Ni kumbu kumbu ya kifo cha Gavana wa kwanza wa Zanzibar.Kumbuka koloni letu TANGANYIKA DAIMA.leo ni karume day ambapo huwa sielewagi umuhimu wake kwa huku tanganyika hadi kuifanya iwe mapumziko naona mheshmiwa rais pia kaamua kwenda kuhudhuria kumbukumbu ya mauaji ya halaiki huko rwanda nadhani ipo haja ya kuifuta hii siku kwa huku tanganyika kwani inaongeza tu utitiri wa siku za mapumziko swali la kujiuliza ni kua hivi huyo karume hadi tumkumbuke alitufanyia nn hasa watanganyika?
Nyerere day haiwezi kufutwa kwa sababu Nyerere alikua rais wa wazanzibar piaIkifutwa Karume day huku, na Nyerere day ifutwe Zanzibar??
karume day ifutwe sio relevant kwetu kabisa
karume alikua rais wa Zanzibar na rais wa Zanzibar kwetu hana umuhimu
Kwa maana hiyo huu muungano ni marufuku kwa nchi nyengine kujiunga?ndio maana wazanzibar wanasema Tanzania ndio Tanganyika imejivika koti la muungano kuitawala Zanzibar.Hapana! Hii haiko sawa i think, mie ni mfuasi mkubwa sana wa utumbuaji wa sikukuu za umma zisizo na tija ila hii naona bora ibaki tu kwa heshima ya Mama Tanzania.
Karume ni founding father wa TANZANIA kama alivyokuwa Nyerere, hakutakuwa na maana kuifuta Karume day alafu tuendelee kuwa Tanzania.
And the last thing, naona kuna hii tabia ya ubaguzi ambayo inazidi kuota mizizi kadri siku zinavyosonga! Ni kwanini tubaguane kwa utanganyika wetu na uzanzibari wetu?! Nyerere tunayemheshimu alikemea hilo kwa nguvu zake zote, kwann tusimuenzi kwa kuliishi hilo?!
Tukianza kuwabagua wazanzibar kwa uzanzibati wao na tukafanikiwa katika hilo basi tujue hatutoishia hapo, tutakuja kwabagua wahindi, wazungu, wachina na watu wa mataifa mengine, tukimaliza hapo tutaingia hadi kwenye makabila, rangi ya ngozi, urefu na ufupi, utajiri na umaskini and it will never end.
Dhambi ya ubaguzi huwa haina mwisho!
Wishing you all happy public holiday.
kijana unataka kuvunja muungano ? maana kwa sasa marehemu wawiili ndio walioshikilia huu muunganiko , walio hai wala hata hawajali kitu .Leo ni Karume day ambapo huwa sielewagi umuhimu wake kwa huku Tanganyika hadi kuifanya iwe mapumziko. Naona Rais pia kaamua kwenda kuhudhuria kumbukumbu ya mauaji ya halaiki huko Rwanda, nadhani ipo haja ya kuifuta hii siku kwa huku Tanganyika kwani inaongeza tu utitiri wa siku za mapumziko.
Swali la kujiuliza ni kuwa hivi huyo Karume hadi tumkumbuke alitufanyia nini hasa Watanganyika?