Karume anamwakilisha nani?

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
15,393
31,344
Wakuu, pengine nina mapangufu kidogo kuhusu katiba na ningeomba msaada wa kueleweshwa.
Hivi karibuni Znz wamebadili katiba [marekebisho] na kuweka wazi kuwa ni nchi kati ya zile zinazounda JMT. Lakini kimsingi ni nchi, ina Rais ambaye ana mamlaka ya kuteua wakuu wa mikoa, ana baraza la mawaziri,bunge la wawakilishi etc etc.
Huko nyuma katiba yetu ilikuwa inaweka wazi kuwa kuna makamu wawili wa Rais, bara na visiwani, na huyu wa visiwani alikuwa ni makamu wa pili. Hii imebadilishwa na Makamu wa pili anapatika kwa njia ya ugombea mwenza. Talaa linatokea lisilotarajiwa basi atakaimu madaraka ya Rais wa JMT hadi taratibu zingine zitakapofuatwa.
Majuzi Rais Karume alikuwa SADC akiwakilisha Tanzania, na pia alikuwa Kenya wakati katiba mpya inapitishwa. Huko kote alikwenda kuwakilisha Tanzania.
Kama ingetokea Rais akamchagua waziri wa mambo ya nje wa JMT au Naibu wake ambaye anatoka Znz[kwa sasa] nisingejiuliza kwasababu hawa ni watumishi wa JMT.
Sasa sijui Rais Karume alituwakilisha kwa capacity gani! Rais wa Zanzibar, mjumbe wa baraza la mawaziri la JMT au mjumbe wa kuteuliwa tu kutoka nchi ya Zanzibar!??
Nauliza hivi kwasababu kama ingekuwa ni kichama, Rais wa Zanzibar pia ni makamu mwenyekiti wa chama. Lakini kuwakilisha Tanzania, napata taabu kuwa ingetokea kuna jambo la kusaini mkataba, yeye angesaini kwa ''authority'' ipi aliyopewa na katiba ya JMT ?
Na je kwenye mkutano alikuwa addressed kama nani? Rais wa znz anayemwakilisha Rais wa Tanzania, au Mwakilishi kutoka JMT au Makamu mwenyekiti wa chama tawala Tanzania, au Mjumbe wa baraza la mawaziri la JMT?
Naomba msaada wa mawazo yenu.
Ahsanteni
 
tangu lini nchi ikawa na raisi kivuri bwana? zanzibar ni nchi ya kusadikika tu, huyo karuma mwenyewe
alikuwa kama meya wa miji ya visiwani tu
 
Karume ni kama diwani! Labda siku wanzanzibar waamke kwenye usingizi wa pono!
 
Wengi wenu hamjakanyakaga huko Zanzibar, mkienda huko mtatambua
kuwa Karume siyo Diwani au Meya. Yeye ana Serikali (Raisi), ana Mahakama, na
Baraza la Wawakilishi (Bunge) hiyo ni kwa mujibu ya Katiba ya SMZ.

Pia nimeona kuna ofisi za Balozi za nje kama India, China, Misri na Oman.
Kama hiyo haitoshi pia ana uwezo wa kuteua Wakuu wa Mikoa na Wilaya
na ana Baraza lake la Mawaziri linalotokana na WAjumbe wa Baraza la
Wawakilishi.
Nadhani Kenya amemwakilisha Rais Wa Tanzania kama Mjumbe tu na
si vinginevyo.
 
Back
Top Bottom