Karume amtembelea Mansour kituo cha Polisi

Karume amtembelea Mansour kituo cha Polisi

Kibo10

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
11,278
Reaction score
8,868
mansour.jpg

Aliyewahi kuwa Waziri wa SMZ, Mansour Yusuph Himid ambaye alikamatwa na silaha mbili za moto na risasi 412, nyumbani kwake Chukwani hivi karibuni.

Zanzibar. Rais mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Amani Abeid Karume jana alifika Kituo cha Polisi Madema kumjulia hali shemeji yake, aliyewahi kuwa Waziri wa SMZ, Mansour Yusuph Himid ambaye alikamatwa na silaha mbili za moto na risasi 412, nyumbani kwake Chukwani hivi karibuni.

Karume alifika katika kituo hicho ambacho ni Makao Makuu ya Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi saa 5.30 asubuhi na kumjulia hali Himid ambaye amewekwa mahabusu akisubiri uchunguzi wa polisi dhidi ya tuhuma zinazomkabili.

Habari za uhakika kutoka ndani ya polisi zinadai kuwa Rais Karume alizungumza na shemeji yake kwa muda usiopungua dakika tano na kumtaka kuwa mstahimilivu wakati vyombo vya dola vikiendelea na utaratibu wake.

Viongozi wengine waliofika katika kituo hicho ambacho kimeimarishwa ulinzi tangu alipofikishwa juzi, ni pamoja na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kutoka CUF; Hija Hassan Hija (Kiwani), Saleh Nassor Juma (Wawi), Hassan Hamad Omar (Kojani ) na Naibu Waziri wa Maji, Nishati, Makazi na Ardhi, Haji Mwadini Makame ambao walimpa mkono wa pole 6.30 mchana.

"Mansour anastahili pongezi na siyo kupewa pole, inashangaza mambo ya ulinzi na usalama ni ya Muungano kwa nini upande mmoja uruhusiwe kumiliki silaha na upande mwingine uzuiwe, ndiyo maana tunasema Zanzibar haitendewi haki," alisema Hija muda mfupi baada ya kutoka kituoni.

Hata hivyo, alisema Jeshi la Polisi linapaswa kuendelea na operesheni ya kuwasaka viongozi wengine wanaomiliki silaha na kuwafikisha katika vyombo vya sheria kwa vile tukio hilo limewafunza mambo mengi na kutaka haki itendeke.

Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai Zanzibar, Salum Msangi alisema polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na matokeo yake ndiyo yatakayoamua wapi pa kufunguliwa mashtaka kati ya Zanzibar au Tanzania Bara.

"Kwa mujibu wa sheria za Zanzibar, hairuhusiwi raia yeyote kumiliki bastola," alisema.

Himid alipekuliwa nyumbani kwake juzi baada ya Jeshi la Polisi kupata taarifa za kiintelejensia kuwa anamiliki silaha za moto.

Taarifa kutoka katika eneo la tukio zinaeleza kuwa kazi ya upekuzi wa nyumba mbili zilizopo katika eneo moja ilifanywa kwa kutumia mashine maalumu.

Chanzo: Mwananchi
 
Police wanajidhalilisha tu ... hakuna kesi hapo! ... Malima alijifanya baby akanyonya sana chuchu, mwisho akapiga Usingizi wa kutosha pale Moro! Alipoamka akakuta Tanzanite, fedha, Bastola na SMG vimekombwa vyote!!! Police walimsaidia kurejesha Bastola na SMG! ... Swali la Msingi ni Je? Naibu waziri wa bara anaruhusiwa kumiliki silaha za kivita? Hii Double Standard Approach kwenye nchi moja ni SAWA? ... Acheni fitna za kisiasa! Kosa la Mansour ni kujiunga CUF...
 
Wananikumbusha ishu ya kutengeneza ya visu vya cuf 2000....mahita alijitoaga ufahamu...sijui iliishiaga wapi ile kitu???
 
CCM wametarget uchaguzi ujao hayo ni maandalizi ya kumkosesha Mansour haki ya kugombea uwakilishi/ubunge katika uchaguzi ujao nisuala la muda tu.
 
3 zinahitajika sana ili kutoa hii sintofahamu ya miaka zaidi ya 31 sasa
 
Police wanajidhalilisha tu ... hakuna kesi hapo! ... Malima alijifanya baby akanyonya sana chuchu, mwisho akapiga Usingizi wa kutosha pale Moro! Alipoamka akakuta Tanzanite, fedha, Bastola na SMG vimekombwa vyote!!! Police walimsaidia kurejesha Bastola na SMG! ... Swali la Msingi ni Je? Naibu waziri wa bara anaruhusiwa kumiliki silaha za kivita? Hii Double Standard Approach kwenye nchi moja ni SAWA? ... Acheni fitna za kisiasa! Kosa la Mansour ni kujiunga CUF...

Na hii ni tishio kwa wengine wanaoota kujiunga na upinzani ......... kuna hatari ya rais mstaafu Karume kukigawa chama (ccm) kadiri 2015 inavyokaribia
 
Kumbe ni mtu na shemejiye...
 
Himidi ni jambazi polisi wachukue hatua za kisheria hakuna kumchekea tumechoka kufuga majambazi.
 
Police wanajidhalilisha tu ... hakuna kesi hapo! ... Malima alijifanya baby akanyonya sana chuchu, mwisho akapiga Usingizi wa kutosha pale Moro! Alipoamka akakuta Tanzanite, fedha, Bastola na SMG vimekombwa vyote!!! Police walimsaidia kurejesha Bastola na SMG! ... Swali la Msingi ni Je? Naibu waziri wa bara anaruhusiwa kumiliki silaha za kivita? Hii Double Standard Approach kwenye nchi moja ni SAWA? ... Acheni fitna za kisiasa! Kosa la Mansour ni kujiunga CUF...
Hujitambui nyie ndiye mlikuwa mnapewa hizo silaha mnaenda kuuwa watu ngoja tuwanyoshe mpaka muache ugaidi wenu.
 
Yupo Mahkamani sasa, hapana shaka atapata dhamana...
 
Police wanajidhalilisha tu ... hakuna kesi hapo! ... Malima alijifanya baby akanyonya sana chuchu, mwisho akapiga Usingizi wa kutosha pale Moro! Alipoamka akakuta Tanzanite, fedha, Bastola na SMG vimekombwa vyote!!! Police walimsaidia kurejesha Bastola na SMG! ... Swali la Msingi ni Je? Naibu waziri wa bara anaruhusiwa kumiliki silaha za kivita? Hii Double Standard Approach kwenye nchi moja ni SAWA? ... Acheni fitna za kisiasa! Kosa la Mansour ni kujiunga CUF...

Sheria za znz huwezi kumiliki silaha kama ana kibali cha bongo basi ame vunja sheria ataenda jela,question katoa wapi znz hakuna sehemu wanauza hayo mavitu?Tano zimetumika ametumia wapi?Znz hakuna uhalifu napata wasi wasi atakuwa gaid
 
Kumbe nchi ya Zanzibar hawaruhusu kumiliki bastola!

Huku Tanganyika bastola zinapigwa hata kwenye ma baa.
 
Himidi ni jambazi polisi wachukue hatua za kisheria hakuna kumchekea tumechoka kufuga majambazi.

Ni sahihi mkuu,:kuna watu wengine himu jf ni kama vile ma KJ, kila ishu za msingi kabisa wao wanaingiza siasa!
 
namshukuru mungu kwa kuniwezesha kuikataa kazi ya polisi .
 
Back
Top Bottom