Karne ya 21 Tanzania bado inalia na Mikataba feki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Karne ya 21 Tanzania bado inalia na Mikataba feki

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by apolycaripto, Jul 15, 2011.

 1. apolycaripto

  apolycaripto JF-Expert Member

  #1
  Jul 15, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 637
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Nimesikiliza kikao cha bunge jioni hii kwa kweli inasikitisha sana kwa Nchi hii mpaka leo tunalia na mikataba feki has ya madini.Hivi tatizo ni shule ama ufisadi uko katika mishipa ya damu.Hawa wanasheria wetu wanakazi gani ndani ya Serikali?Nani anaandaa hii mikataba hii?Nimeshangaa akina Mwijage wanajigamba kwa shule walizonazo huku walicho ama wanacho deliver mbona hakionekani.

  Wenzetu wanafikiria kwenda kuishi sayari nyingine sisi tunasumbuliwa na jinsi ya kukokotoa mrahaba/mrabaha.Hii ni aibu jamani kuendelea kulilia BGM,Buzwagi,IPTL na wengine huku tunazidi kufilisika.Tazama Zitto anadai Symbion imenunua haramu Dowans wote tumeufyata kwa maana ya kutotoa tamko la kutoafiki kisa USA Coy.Naungana na Zitto kwani pamoja na giza kuongezeka mara mbili hata baada ya Symbion kuingia hakuna anayethubutu kuhoji Kampuni hii na faida yake.Bado Tanesco imeingia mkataba kinyemela na hatujui kiasi gani wanalipwa hawa wafisidi.

  Mbali na ukosefu wa uzalendo,na wasi wasi elimu waliyonayo hawa wanasheria wetu na watendaji wetu kwani hii si rushwa tu bali kuna ujinga katika vichwa maake imepitiliza.Aibu,aibu imefikia hatua kujivua gamba kuingie kwa watendaji wa serikali ambao wanatuathiri zaidi ya athari tunazopata kisera.
   
 2. 22nd

  22nd JF-Expert Member

  #2
  Jul 15, 2011
  Joined: Aug 1, 2010
  Messages: 498
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Ninachoomba mungu ni kwamba haya madini yaishe,maana sijawahi kuona faida yake nikiwa kama mwananchi wa kawaida.
  kwani nchi ngapi wanaishi bila ya madini? na bado matajiri? kwahiyo bora yaishe tubakie na kazi ya kufukia mashimo.
   
Loading...