Karne hii bado kuna nchi zinapigana vita?

Mipaka ya nchi, sheria na taratibu zake haziondoi human nature ya kupenda kuwatawala wengine na mashindano.

Kama hujaweza kutatua tatizo lililopo katika vichwa vya watu, hayo mambo ya mipaka, sheria na taratibu hayasaidii lolote.

Zaidi, mambo ya mipaka, sheria na taratibu tofauti ndiyo yanayoanzisha vita.
Kwanini wasijikite katika kutatua hayo matatizo ya watu wao hadi wakavamie kwa wengine au wadundane ni akili gani hiyo

Mfano Russia na Ukraine hadi karne hii wanagombania mipaka katika zama za ushindani wa akili na ugunduzi wa Mambo bado wanagombania mipaka akili gani hii

Ni sawa na taifa teule kila mwaka sera ni matundu ya vyoo na barabara za kuchonga na magreda
 
Mleta uzi na wachangiaji wengine muishukuru serikali ya CCM kulinda amani ya nchi kwa wivu mkubwa. Waliovimbiwa amani ndo husema WATAKINUKISHA bila kujua KIKINUKA hata wao na familia zao hawatakuwa salama.
 
Watu hawana control kwenye mambo wanayoyafanya kama wewe unavyotaka kujiaminisha.

Mambo mengine mengi ni matokeo ya tamaduni, zinazojengwa na mazingira na mambo mengi ya practical logistic.

Katika mfumo ambao naturally watu wazuri hawawezi kupanda ngazi ya uongozi, kwa sababu ni wakweli sana, wazuri sana, hawawezi kufanya the bloodsport of politics, na narcissists tu ndio wanaweza kupata uongozi, vita ni natural progression ya politics za kawaida.
 
Hakuna cha kushukuru hapo ila tunawasihi kutumia akili kutatua changamoto za watu habari za mabavu na maguvu zilitumika katika zama za kijima ni ukosefu wa akili taifa lolote kuingia vitani katika zama za sasa
 
Ni sawa tu na hapa Tanzania ukitokea umekosoa utawala unatekwa na kuuliwa. Binadamu wabaya sana
 
Watu hawana control kwenye mambo wanayoyafanya kama wewe unavyotaka kujiaminisha.

Mambo mengine mengi ni matokeo ya tamaduni, zinazojengwa na mazingira na mambo mengi ya practical logistic.

Katika mfumo ambao naturally watu wazuri hawawezi kupanda ngazi ya uongozi, kwa sababu ni wakweli sana, wazuri sana, hawawezi kufanya the bloodsport of politics, na narcissists tu ndio wanaweza kupata uongozi, vita ni natural progression ya politics za kawaida.
Nakuelewa mkuu ila zama zinabadilika zama hizi hata hao politicians wana uelewa mkubwa wa jamii zao huku jamii pia ikiwa na uelewa sawa au kuzidi wanasiasa tofauti na zama za giza ambapo watu walikuwa wanaburuzwa kama misukule wakiambiwa wajitoe muhanga wanaenda tu

Siku hizi watu wameelimika na wanajua Mambo kiundani ni ajabu bado wapo wanaoburuzwa kwenda kutoa muhanga maisha yao

Taifa moja kulivamia taifa lingine kwa tofauti za kiitikadi na dini katika zama za wasomi ni ukosefu wa akili mambo yapo mengi ya kufanya zaidi ya hayo
 
Namuelewa mkuu ila zama zinabadilika zama hizi hata hao politicians wana uelewa mkubwa wa jamii zao huku jamii pia ikiwa na uelewa sawa au kuzidi wanasiasa tofauti na zama za giza ambapo watu walikuwa wanaburuzwa kama misukule wakiambiwa wajitoe muhanga wanaenda tu

Siku hizi watu wameelimika na wanajua Mambo kiundani ni ajabu bado wapo wanaoburuzwa kwenda kutoa muhanga maisha yao

Taifa moja kulivamia taifa lingine kwa tofauti za kiitikadi na dini katika zama za wasomi ni ukosefu wa akili mambo yapo mengi ya kufanya zaidi ya hayo
Juzi nilikuwa nazungumza na rafiki zangu tunabisahana kuhusu kwa nini CCM ambayo haina upinzani wa maana nje ya CHADEMA (ambayo imesusia uchaguzi kimsingi) inasumbuka sana na utekaji na kamatakamata ambayo inaonekana kuwa counterproductive kwa kuipa nchi jina baya bila sababu ya msingi.

Tulikuwa tunafanya uchambuzi logical na reasonable kwa assumption kuwa viongozi wa CCM na wananchi wa Tanzania ni logical, reasonable na fairly educated in one way or another.

Mimi nikafanya a contrary observation kwamba, najinukuu.

"Labda tuna wa overestimate uwezo wao (CCM) wa kuwa strategic thinkers wakati tuna underestimate mtaji wao wa ujinga wa Watanzania wengi.".

Naona kama wewe unafanya kosa hili pia, kimataifa.
 
Uwezo wa kufikiri wanao tena mkubwa tuu kwa Afrika kinachoturudisha nyuma ni ulimbukeni wa maendeleo hatuwezi kuyatafuta wenyewe tunategemea kuletewa ndio maana viongozi wanaacha logic reasoning na kujivika ujinga wa makusudi

Mataifa makubwa yashavuka huko ila bado yana ukiritimba wa itikadi na uvamizi wa mipaka kitu ambacho kwa karne hii kipo outdated
 
Inashangaza kuona karne hii bado mataifa yanaona vita ndio suluhisho la matatizo yao yani ili mambo yaende sawa na watu wafuate ustaarabu ambao ulishakuepo hadi wadundane kama majogoo atakaeshindwa ndio atawaliwe kwa shuruti

Bado Wana dhana ya survive for fittest dhana zilizokwisha muda hasa katika utawala na kugombania mipaka
 
Silaha zina matumizi mengi siyo specific kwa vita tu, kuna kulinda Mali dhidi ya wezi na majambazi

Vita ni ukosefu wa matumizi ya akili kisawasawa
Upande ni biashara kwa hao unaowasema hawana akili ila nuclear bombs na silaha kubwa kubwa mataifa yanatengeneza kama yalitokea hivi karibu I.

Israel ameamua kuivamia Iran

Ila vita mwisho wake ni hasara tu mpaka kwa wasiokuwemo.
Angalia sasa wanasema matetemeko ya Ardhi yaliyotokea Iran yalikuwa ni majaribio ya Nuclear weapons.

Vita nimeishuhudia na ninajua madhara yake
 
Madhara ni makubwa sana sio tu kwa kushuhudia hata kwakufikiria kwa mwenye akili timamu hawezi ingiza nchi au taifa lake katika Vita

Hebu fikiria marekani ana suply silaha kwa Ukraine ambayo miundo mbinu inaharibiwa na Urusi nchi inarudi nyuma kimaendeleo hizo pesa zao watazipataje na ni mabilion ya pesa ukilinganisha na rasilimali zinazopatikana katika kanchi kama Ukraine na inavyozidi kuzoroteshwa na Vita, the same to Israel and Palestine

Ndio tuje Africa huku Congo au Sudan huwa wanapata faida gani, tuje kwa wapiganaji wenyewe wanashindwa kutumia akili kusolve their disputes? Hadi waingize nchi zao vitani kila siku kuanza tena kujenga miji na uchumi? Vita ni matumizi madogo ya akili
 
Wapo wengi wanaotembe uchi mkuu hujawahi kukutana nao?
Kutembea uchi wala sio kipimo cha kustaarabika
Wazungu hawakai uchi, je hawajastaarabika ? Wazungu wanamaklabu ya kucheza uchi, kufanya ngono za wengi na kuna nchi wanayo siku ya kutembea uchi.
Wazuru kucheza ngoma yao waliwa maziwa wazi unadhani hawajastaarabika ?
Halafu neno "kustaarabika" ni kuishi kama mwarabu ndio maana ya neno hilo.
Waxungu wanatumia civilization. Waafrika kustaarabika ni kuishi kama wazungu au warabu kitu ambacho ni ukoloni mamboleo tu. Kwani masai hawezi kuishi maisha yake na skawa mstaarabu
Nikuulize swali, wazungu kioana wanaume ni ustaarabu ?
 
Umesoma vibaya au hujaielewa content, huyo mdau kasema binadamu siku hizi ni wanyama(likija suala la kuuana) kasoro hawatembei uchi ndio nikamwambia wapo wanaotembea uchi kabisa sasa sielewi hujaelewa nn
 
Vita ni nature ya watu mkuu, na huo ustaarabu unaousema ni wa kufikirika zaidi.

Watu ni wanyama fulani waliojiwekea u special kwamba wao si wanyama kwa sababu wanajiona wanaweza kufanya mambo mengi tofauti na wanyama wengine, lakini kila tukijifanya wastaarabu na tuko tofauti, kuna matukio yanatukumbusha vinginevyo. Tunakumbushwa kuwa na sisi ni wanyama tu bado.
Mkuu nikuongezee tu kuwa ustaarabu ni tabia ya kudumaza mila za watu wegine.
Ukichunguza neno ustaarabu utagundua ni utaratibu wa maisha ya wazungu na warabu.
Mfano kujazana kwenye miji na kutengeneza msongamano usio na maana. Kupenda mavazi ya wazungu na warabu.
Vile mie naona kuunda masilaha kwa mabilioni ya hela ili kuua na kuteka wengine sio ustaarabu bali ni ujinga na uprimitive. Hakunaga faida yoyote wanapata zaidi ya sifa. Tujikumbushe vita ya USA na Vietnam kuna faida gani walipata zaidi ya hasara ?
Huu mfumo wa vita ni mfumo wa wazungu na sisi sote tumeingizwa kwenye mfumo bila kupanga .
 
Yupo mchonganishi ili malengo yake yatimie. Anaweza asiwe binadamu, yupo tafuta kuelewa zaidi
 
Katika karne ya watu waliostaarabika na welevu wa Mambo mipaka ya nchi iliyogawanywa kila nchi na mipaka yake na itikadi au falsafa zake vita zanini?

Kama ni kigezo cha dini kila nchi au taifa Lina utaratibu wake wa kuabudu katika mipaka yake bila kuingiliwa na taifa lingine vita zanini?

Vita zilikuwa enzi za ujima ambapo watu walikuwa wanatumia nguvu zaidi kuliko akili ni ajabu sana kuona mataifa bado yanaendekeza vita katika kutatua changamoto zinazohitaji akili ndogo tu

HAPANA. ZINAPIGANA MITI.
 
Yupo mchonganishi ili malengo yake yatimie. Anaweza asiwe binadamu, yupo tafuta kuelewa zaidi
Labda asiwe binadamu ila kama ni binadamu either hana akili kabisa au ameamua kutumia 0.01% ya akili aliyonayo
 
Madhara ni makubwa sana sio tu kwa kushuhudia hata kwakufikiria kwa mwenye akili timamu hawezi ingiza nchi au taifa lake katika Vita

Hebu fikiria marekani ana suply silaha kwa Ukraine ambayo miundo mbinu inaharibiwa na Urusi nchi inarudi nyuma kimaendeleo hizo pesa zao watazipataje na ni mabilion ya pesa ukilinganisha na rasilimali zinazopatikana katika kanchi kama Ukraine na inavyozidi kuzoroteshwa na Vita, the same to Israel and Palestine

Ndio tuje Africa huku Congo au Sudan huwa wanapata faida gani, tuje kwa wapiganaji wenyewe wanashindwa kutumia akili kusolve their disputes? Hadi waingize nchi zao vitani kila siku kuanza tena kujenga miji na uchumi? Vita ni matumizi madogo ya akili
Huwa nashindwa kuelewa tamaa zinazowapelekea mpaka kuanza vita
Fikiria Marekani yeye ana angalia maslahi yake wala sio amani wala nini bali Mali za wenzake

Sasa sijui wanataka mafuta ya Iran?
Sio kwa kushabikia kote huku
Hata DRC vita yote kisa madini
Kwani hawawezi kupatana bila nguvu

Unasema kweli ila ndio hivyo
 
Baada ya kuona hii vita ya Iran/ Israel, sasa NATO wanatandisha bajeti zao za silaha mpaka 5% ya GDP

Wanahaha sasa
UK watanunua ndege za F-35 ambazo zitabeba nuclear war heads zenye uwezo wa kuuwa maelfu ya watu kwa wakati mmoja

Yaani ni maajabu sana
Hasara walizopata Israel kwa interceptors tu zilikuwa ni $200m kwa siku
 
Back
Top Bottom