Pia kulikuwa na mashindano ya Taifa ya Disco ambayo yalikuwa yakiendeshwa na chama cha Disco Tanzania(TDMA) ambacho kilikuwa chini ya uenyekiti wa Abdulhakim Magomelo(DJ Kim wa Kim & The Boys) na katibu mkuu Samweli Semkuruto.....
Ilikuwa raha sana kuona upinzani mkali miongoni mwa wacheza Disco wetu,na nakumbuka mara nyingi katika mashindano ya Bingwa wa kucheza Disco Taifa upinzani mara nyingi ulikuwa ni kati ya hayati Mussa Simba 'Black Moses' na Bosco Cool J....
Baadhi ya wacheza Disco wengine waliotamba enzi hizo ni pamoja na Athuman Digadiga, Ally Baucha, Samy Cool, Sydney, Huessin Shadrack Guga 'Kokoliko', Kibengo Shaban 'Kadet Bongoman', Savy Pops, Maneno Super Ngedere, Kanda Kid wa Kenya, King Jobiso, Bebe Computer, Sabbah A Jackson, Sammie Cool, Tito Jackson, John Maganga, Bob Richie, Smart Boy, MC Chunusi,Chuchu Lee, Shaba Ranks wa Tanzania, Max Prince/Priest na wengine wengi......
Kwa wacheza Disco wanawake wadada nawakumbuka wachache kama Jessica Ongala, Ashura Mponda 'Queen Clouds', Big Mama, Queen Eliza, Janet Jackson, Homa ya jiji na wengine.............