A town nmewahi danganywa ambapo hadi leo yule mjinga namuona hana akili japo ana Mtoto. Baadhi ya uongo wake ni km ifuatavyo:
1. Mtoto wangu anaenda rikizo dar, kwa babu zake...(naomba nirushie pesa ya kula na nauli ya Mtoto jamani!... Kumbe Mtoto yupo A town)
2. Kuna tafiki yangu wa karibu sana amefiwa na mama yake mzazi.Moro... (Naomba nitumie pesa namsindikiza rafiki yangu huko Moro, nitumie za kutumia nikiwa huko...nitakaa siku tatu tu... (Kumbe hakuna tukio hilo)
3. Mume naomba nitumie pesa jamani, natamani nile via na nguruwe...nipo karibu hapa...hebu naomba nitumie alafu usisahau kunitumia na ya Chipsi nimbebee Mtoto nyumbani..(najipinda tigopesa yake...puuuuh!)
4. Aisee nina mimba ila sitaki kuzaa kwa sasa, dume napigilia msumari iache...ukitoa tusijuane kuanzia siku hiyo......anaanza tumbo linasumbua naomba nitumie pesa niende hospital...(kumbe mimba haipo, bili zinakuja nyingi balaa)
5. Naumwa jamani, nakapicha kanatumwa amelala....nmepimwa naumwa U.T.I matibabu nmeambiwa elfu 88 na mia saba, duuh!, inatumwa. Anadai ni hospitality ya private pale Njiro....
6. Mama hayupo ameenda kahama kusimamia vitalu vyake vya madini, nitumie tu hela za umeme...umeme kila siku na mivocha daily...za kula daily....japo sijamuoa.
7. Mume nakukumbusha hutumi pesa ya saloon, hutaki nipendeze km wengine jamani. Tuma basi ili nami nionekane jamani...hee!, ngapi??... Tax..elfu 10, za kutafuna nikiwa humo ukituma elfu 10 tosha, nywele na fundi... Elfu 58.
Baada ya kujipambanua: nikaamua kumchunguza wangu wa ndani, nikagundua ni muongo balaa...hizo zote hazikuwa zikitumika ktk hayo aliyokuwa anayaeleza. Nikaongea na shemeji yake mmoja...nikaambiwa huyo anajirusha balaa..inatakiwa uwe na pesa za kutosha, kuna watu wapo migodini wanamuhonga balaa...nyumbani hakaliki. Nikaona km makamasi yanataka kutoka...hahahaa!... Bahati nzuri naye akawa km kagundua kwamba uongo wake umegundulika... Hadi kesho kila mtu ana maisha yake...hahhaa
Ni mtu mzima ana Mtoto huyo mmoja, alinizidi miaka 3. Sina hamu ya kuhonga, akija yeyote akiomba hela tu...nahisi kupasuka kichwa nina majibu ya hivyo sana kuhusu hilo ombi....siwaamini tena hao mashetwani