Karibu tujuzane viungo vya chai ya rangi

Mie chai ya rangi niwekee mchai chai tu na hiliki kidogo na vitumbua kama saba hivi na mchuzi wa kuku mkata mitaa si yule anayependa kubweteka.
Vitumbua na mchuzi wa kuku? Hainogi bana
 
Umechelewa
And the bad thing wangu hanywi chai hata utilie kitu gani!!


Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna mtu asiyekunywa chair, watu wengi hawanywi chair kwa sababu ni taste less, chair yenye viungo vya ukweli mtu hawezi kuacha kunywa.

Nakumbuka miaka kadhaa nyuma nilikunywa chair ya maziwa Bagamoyo tena mgahawq wa kawaida tu sijawahi kunywa chair yenye taste kama ile mpaka leo.

Hizi supu tunazokunywa bar uelewe mchuzi ni wa moto na chai ni ya moto ukilielewa hilo ndio utajuwa hata mlevi anaweza kunywa chair, tatizo ni chai gani?
 
Yangu naweka
Hiliki natwanga mwenyewe
Karafuu natwanga mwenyewe
Mdalasini natwanga mwenyewe
Pilipilimanga iliyosagwa
Tangawizi iliyosagwa
Mchaichai
Napenda sana huu mchanganyiko na vile nikiinywa inakuwa inawasha basi burudani.
Kama hupendi ukali unaweza kupunguza pilipilimanga na tangawizi au ukaweka kimojawapo au kuacha kabisa
 
Yangu naweka
Hiliki natwanga mwenyewe
Karafuu natwanga mwenyewe
Mdalasini natwanga mwenyewe
Pilipilimanga iliyosagwa
Tangawizi iliyosagwa
Mchaichai
Napenda sana huu mchanganyiko na vile nikiinywa inakuwa inawasha basi burudani.
Kama hupendi ukali unaweza kupunguza pilipilimanga na tangawizi au ukaweka kimojawapo au kuacha kabisa

Umeolewa mamilo??mana hii chai ndio naielewa sana.

Bila kusahau kukamulia ndimu au limao.
 
"Si ulitaka Chai Chai,
Iweje unalalamika unaungua...aaa aa a?"
 
Nimechanganya mdaladini,hiliki,karafuu,pilipili manga kidogo Kisha nikatwanga nikafungia kwenye kopo.wakati wa kuandaa na chemsha maji tuu hatimae naweka kwenye chupa ya chai na huo mchanganyiko ili kuhifadhi ladha na harufu yake ya asili.
 
Mdalasini na hiriki unatwanga pia tangawizi uweke na sukari iive pamoja bwana eeh ni tamu na rangi yake huwezi jua haina majani
 
Ndi
Mkuu unapata chai nzuri yenyerangi ya dhahabu harufu ya kuvutia na kuifanya iwe tamu,
Ukipenda pia waweza tumia chai ya mbegu za parachichi
Hapo kwenye mbegu za parachichi ndio nimekuelewa sana tu mi NDO chai yangu hiyo nachanganya na mdalasini.
 
Habari zenu wapishi.

Naomba kufahamu jinsi ya kuandaa viungo vya chai ya rangi. Yaani niweke viungo pekee bila majani ya chai iwe tamu na kunukia vizuri.
Vipi umeweza kupika chai?
 
Back
Top Bottom