Abby Newton
JF-Expert Member
- Nov 12, 2017
- 1,227
- 2,197
Msimu huu pekee Yanga wamebadilisha makocha zaidi ya 3 lakini timu bado haina matokeo mazuri.Kitendo cha kubadili badili makocha ni dalili tosha kuwa timu ina matatizo ndani ya uwanja.Nimekuwa nikiifuatilia Yanga inapocheza kwa makini sana. Yanga wanatatizo kila idara,na sina hakika km wanajua na wameaamua kukaa kimya tu.
1.Eneo la Makipa.
Hadi sasa haieleweki kipa namba moja wa Yanga ni yupi.Hali hii inasababisha makipa kukosa kujiamini.Kila anaepangwa kuanza anafanya makosa sababu ya kukosa kujiamini. Ni lazima kocha aamue yupi awe kipa namba moja.
2.Eneo la mabeki wa pembeni.
Hapa ndo kunatatizo kubwa la msingi. Mabeki wote wa pembeni hawawezi kupanda kushambuliwa,hawana ubunifu(Skills), passing accuracy yao ni "very poor".Hii inasababisha wapoteze mpira kirahisi sana.
Vilevile hawana uwezo mzuri wa kupiga cross au faulo za pembeni. Kwa mpira wa kisasa mabeki wa pembeni wanakuwa washambuliaji pale timu inaposhambulia. Mabeki wa pembeni wa Yanga wanachofanya ni kimoja tu kuokoa na kupiga mpira mbele ambayo ni staili ya kizamani au kwenye ndondo. Mfano,jana nimemfuatilia Adeyuni dk zote 90 sikumuona amepiga Cross au hata kufanya "Overlap" moja ya maana. Upande kulia dogo anajaribu lakini bado anamengi ya kujifunza kutoka kaka ake Shomari Kapombe.
3.Mabeki wa kati.
Mabeki wa kati wa Yanga hawana utulivu hasa pale wanaposhambuliwa mfululizo.Ni km wanachanganyikiwa. Vilevile hawana uwezo mzuri wa kuanzisha mashumbulizi kutoka eneo la nyuma. Kitu pekee wanachokifanya ni kubutua mpira mbele. Angalia Wawa na Onyango wanavyocheza kwa utulivu hicho ndicho kinachokosekana kwa mabeki wa Yanga. Lamine Moro ni beki machachari lakini si beki wa kiwango hiiiiiicho! Anacheza faulo nyingi na mbaya bila sababu. Sehemu ya kutumia akili yeye anatumia nguvu tu. Jana dhidi KMC km si huruma ya refa kadi nyekundu ingemhusu.
4. Eneo la viungo wa kati
Pamoja na sifa wanazopewa Mukoko na Feitoto,bado kila mmoja anamapungufu yake yanayogharimu timu.Mukoko anakaba sana lakini anapoteza mpira kirahisi sana. Hii inasababisha mipira isifike mbele kwa haraka na kwa wakati.
Kwa upande wa Feisal km kiungo wa mbele anashida ya kasi( speed) hasa pale timu inapoenda kushambulia. Lakini pia anacheza chini sana kitu kinachotengeneza gepu kati ya eneo la kati na eneo la mbele. Yanga wanahitaji kuongeza viungo wabunifu na wanyumbulifu wenye uwezo mzuri wa kumiliki mpira na kupiga pasi maridhawa( Killer pass) eneo la mwisho. Oh
5. Eneo la Ushambuliaji
Hapa ndo kuna janga zito. Takwimu zinaongea zaidi. Wachezaji pekee wa kigeni wenye afadhali ni Ntibazonkiza,Tuisila,na Yaocuba. Wengine waliobaki inabidi wapishe. Najua Carlinhos anajua mpira lakini kwa ligi ya Tanzania inayohitaji nguvu si saizi yake.
Mapufungu eneo la ushambuliaji ni mengi mno ambayo njia pekee ni kusajili wachezaji wenye uwezo kuliko hawa waliopo.
Karibu tujadili Ubovu wa Yanga na nini wafanye kitaalamu kabsa bila mihemko. Nawasilisha.