Karibu mama yetu jamvini, mimi ningependa sana hoja yako ya kwanza ambayo ni kubwa mno kuizungumzia ni ile ya mji mpya wa kigamboni, hii inagusa sana hisia za wakazi wa mji huu ambao wanatakiwa kupisha mradi mpya.
1. Waziri Mkuu alifafanua kwamba tathmini ifanyike upya sababu mambo mengi hayakufuata sheria za re-allocation, sasa hili unalizungumziaje, maana hatujaona watathimini wowote toka wizarani kwako wakianza kazi mpaka sasa hivi?
2. Je serikali italipa fidia nyingine kwa wananchi wa eneo hili baada ya kuwazuria kutoendeleza makazi yao kwa miaka miwili -- stop order ya serikali mwaka 2008 - 2010? katika eneo hili?
3. Kuna eneo kubwa sana baada ya Dar Zoo, hilo lipo wazi ambalo linafika hadi Tundwi Songani, Kimbiji, Mbutu nk, ni km 25 - 50 toka katikati ya jiji. hilo halijaendelezwa na linafaa kabisa kujenga mji huu mpya wa kisasa, kwa mantiki hii serikali haitaingia gharama kubwa za ulipaji wa fidia, je mweshimiwa hii hoja unaionaje?
4. Je serikali inapata kigugumizi kipi kuweka kwazi kwamba wananchi wa eneo hili watafute wawekezaji wenyewe na kuingia nao mikataba (wabia kwenye ardhi) ili kujenga mji mpya kufuata ramani iliyopo? kuna hisia za wananchi kwamba serikali inafanya udalali (mtu wa kati) kati ya wananchi na wawekezaji.
Mwisho karibu sana JF.