Kariakoo Bila Machinga wa Kichina Haiwezekani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kariakoo Bila Machinga wa Kichina Haiwezekani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mgt software, Feb 7, 2011.

 1. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #1
  Feb 7, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,728
  Likes Received: 1,636
  Trophy Points: 280
  Kukiwa kumebakia siku chache kuondolewa wamachinga wa kichina , leo nimeona tuchangie uwezekana wa machinga wakichina kutokuwepo na biashara ya kariakoo kudolora.

  Kwanza kabisa napenda kuwajulisha wale wote ambao hawajui hili la ujio wa machinga wa kichina hasa faida zao dhidi ya wafanya biashara wa kariakoo. Wachina hawa kama watu wengine wa kawaida wameingia nchini kukiwa na kibwagizo kwamba Tanzania China Friendship kama sera ya serikali, wakaja wengi wakapokelewa wakaanzisha tuviwanda tudogo tudogo, wakaifanya kariakoo ikawa bize sana kufuatana na kuwa na ushapu wa kazi na uwezo wa kufanya biashara, ubunifu wa mitindo mbali mbali , kama biashara ya maua, biashar ya viatu vya ngozi na plastiki, vifaa vya ujenzi, nguo.na Nk.
  2. Sisi wafanyabishara ndogo ndogo tunafaidika sana na uamifu wa kitu kinaitwa kupewa mali kauli, watu wengi walikuwa wakikopeshwa kwa njia hii, maduka yote ya simu za kichina wao, maduka ya vifaa vya Ujenzi , wao, hufanya kazi kwa njia ya uaminifu kwa kuwa wanajua kuwa serikali yetu inamasharti magu ya mikopo hivyo ni kama wanatuazima mali tuuze tupate faida tule nao wale, angalia piki piki zinavyosaidia watu. Bajaji na NK.
  3. Serikali isikurupuke kuwafukuza hawa machinga wa kichina kwani ni chachu ya maendeleo, wanatoa ajira, wanafundisha jinsi ya kutengeneza viwanda vidogo vidogo, hata hivyo unajua vijana wengi wanaenda china sana kuzidi hata kwenda nyumbani kwao, sasa na sisis wakitufukuza kwao itakuwaje, angalia takwimu ya watu wanaoenda china kwa siku, alafu angalia cnhi kama Zambia, Congo malawi na nchi nyingine wanakuja hapa Dar kuchukua bidhaa ya kichina na kutoongezea patao la taifa.
  4. Ikiwa serikali itafikuza wachina na kuwaacha wahindi , nchi itadoda sana, wahindi wanajifungia majumbani kwao wakisubiri dili za bandarini, au magendo kali ya kuhumiza nchi yetu, kama waziri mhusika ana uchungu, mbona posta (samora Avenue ) pamekwisha kibiashara kutokana na kuteka biashar nyingi na hawaziendelezi.
  Mwisho nasema kuwa, wafanyabiashara wote wa maduka ya kukodisha watapata hasara kubwa kwa kuwa wapangaji wengi wa kichina wanalipa kodi kubwa, hivyo marejesho yao yatakuwa mabaya, kukatisha mikata kutaleta misukosuko, nionavyo mimi, tusichukulie chuki ya wachina kuwa wengi tuliwaita wenyewe, kwa wito kuwa TZ and CHin friendship sasa wameonyesha upendo kwa watanzania kwa kuwakopesha wasio na ela na mali kauli kama mkombozi baada ya Benki Nyingi kututupa mkono na kuwaamini wahindi ambao hawana hata nyumba wanakaa NHC lakini wanakopeshwa kiraisi sisi tunamashamba lakini wanatuambia tuwe na nyumba ya Millioni Hansini, au Mia, je kijana wa Umri wa miaka 25 mpaka 35 atatoa wapi hiyo nyumba kama dhamana. Tufike sehemu tuseme waliopo waache ila wadhibiti wanaokuja ili nao wasijetufukuza kwao
   
 2. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #2
  Feb 7, 2011
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Umenena kweli wachina siyo wakuondoa hivi hivi,ufanyike utafiti kwanza ijulikane hasara na faida kwa uwepo wao na kutokuwepo kwao,
   
 3. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #3
  Feb 7, 2011
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,082
  Likes Received: 4,032
  Trophy Points: 280
  Bravo bro., mbali ya hayo bidhaa zao ni affordable ukiacha zile zilizo chini ya viwango kitu ambazo mtu mwenye akili vizuri hawezi walaumu wao moja kwa moja ila rushwa bandarini katika kuruhusu kuingizwa nchini bidhaa hizo feki kwa kushirikiana na "Wabongo wenzetu (weusi+waasia)" wasio waanifu!

  Kuwaondoa wachina maana yake kupanda gharama za bidhaa "mark my words" madhara yake hayaelezeki! theories za uchumi ndio unasema hivyo hao wamachinga wazawa + Wahindi wenye maduka watafurahia ila baada ya muda wananchi wa kawaida wataona maana yake! Tusiwe maadui wa ushindani wa kibiashara nathani "repatriation of Indians in Uganda" inaweza kutupa somo! Mie nawataka hawa watu hata waanze kuuza mafuta maana najua kuna ukiritimba unaohujumu bei ya mafuta yaani carteling sort off inayofanywa na viongozi wa nchi hii kushirikiana na ndg zetu wenye asili ya Kiasia!

  Hata umeme pia waruhusiwe kufua na kusambaza! labda tutasahau machungu ya Richmond babake Dowans!

  Inashangaza watu hawaoni jinsi Kariakoo ilivyopanuka sasa hata wahusika kufikiria kuvunja na kujenga soko la kisasa litakaloweza kuchukua watu wengi zaidi! K'koo sasa ni kitovu cha biashara kwa nchi za Afrika Mashariki unawakuta Wacongo, Wacomoro, Waganda, Wakenya, Wazambia, Wamsumbiji, Wamalawi hata Wazimbabwe! Mijitu isio na utashi wa kufikiria bwana? mbona kuna Wapemba na wachagga kibao tu bado wanafanya kazi huko K'koo kwanini na Watanzania wengineo wasiunde Cooperatives sort off ku-spear head their interests? I thought Wamachinga should be proud of a slow but sure progress they are making niliskia hivi karibuni wako mbioni kuanzisha Machinga Bank! That's a good move! wawasukume serikali wawasaidie na si kuwafukuza mabarabarani!

  Serikali isitafuate cheap popularity through economical devastating decisions! lawama za kutotoa msaada kwa watu wa SMEs kuweza kujikimu haitaondoka kwa kuondoa Wachina! Get visionary and competent individuals to run that respective ministry kama waliopo imewashinda! Chinese are good for us kwa vile we grow with them unlike Western companies kama lets say Walmart comes to K'koo hata hicho kidogo wanachopata Wamachinga kitaporwa! Cha ajabu tunawakumbatia sana watu kama Shoprite while tunajua majority of our people ni wachuuzi na hawana elimu hata kuajiriwa kwenye hayo makampuni na kuwashirikisha katika uchumi tunapaswa kuwapa nafasi kujishughulisha kwa kujiajiri! that's how microeconomics work!!! halafu tusisahau there is no innovation without competition shutting the free movement of people and goods/services meaning dragging your feet out of window of advancement that comes with globalization!
   
 4. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #4
  Feb 7, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,728
  Likes Received: 1,636
  Trophy Points: 280
  Kuna siku ambazo anakabiliwa na mambo magumu kweli kweli, kuna siku rafiki yangu alitoa michango ya harusi yake akajisahau mambo mengi, siku ya arusi yake akribu aokote makopo , alikuwa ajanunua pete ya dhahabu ya yeye na Mkewe, viatu vyake na mkewe, nikamshauri asiwe na tabu elfu ishirni haitaisha , tukaenda kariakoo akanunua viatu vya plasitik alimaarufu kam vya kichian, pete mbili ya kwake na mkewe, arusi ikafanyika vizuri ilipendeza kweli kweli, siku ya siku pete ikaanza kupauka ya mkewe, mkewe akwa analalamika kuhusu pete , nikamwambia nenda ukachingeshe nyingine kama ile mambo yatatulia hii iwe siri yako, mpaka leo wametulia amebaki na siri yake, hii inaonyesha ni jinsi gani wachina wanavyotusaidia watu wa hali ya chini ijapo kwa muda.
  Naendela kuwauliza Je HUYU WAZIRI anajua nia watz wangapi wanafanya umachinga nchini china ni wangapi, aachane nao tunabadilishana, sisi tunajaa kwao nao waje. Wewe unayelilia uwekezaji wao nchini kwako wewe kwao umewekeza nini, angalau wametuletea viatu vingi vya plastiki hatuchomwi tena na mabaki ya samaki, maana kwa uchafu wa dar watu wengi tulikuwa tunaumia sana
   
 5. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #5
  Feb 7, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Hivi wanafikiri watu huwa wanafukuzwa tu hiv hivi
   
 6. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #6
  Feb 7, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Mwana nakubaliana na wewe,pia tutambue kuwa mchina na hapa kwao wao wanapiga kazi na wanafanyabiashara ya kila kitu,kwa mfano ukienda supermarket ya china utakuta hata miguu na vichwa vya kuku vin auzwa na navyoongelea supermarket namaanisha,ila sisi wabongo ni wavivu tunaleta uzuri ktk kazi sasa jamaa wamekuja na kutuonyesha kwanini watu wanaendelea tumeanza kulia
  tusilalamike sana tupige kazi wakuuuu

  msema ukweliii hapendwiii daimaaaaaa:clap2:
   
 7. Shomari

  Shomari JF-Expert Member

  #7
  Feb 7, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,107
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Hivi huyu Waziri anajua anachokifanya, isije ikawa wahindi wanamtumia kwa wivu wa kibiashara, wahindi hawataki kabisa kuwaona wachina hapo k/koo, kwa dunia ya sasa umfukuze mchina unategemea nini wakati ndio baba mtarajiwa wa dunia, majuzi tu hapa Rais wa china alifunga safari na kuelekea marekani kuimarisha uhusiano wao kibiashara , Obama mwenyewe anawakubali, sisi ndiyo tunajifanya tunajua uzalendo sana, mnawaonea wachina mimi nasema wafukuzeni wahindi kwanza.
   
 8. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #8
  Feb 8, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Chinese chicken farmers ruffle Zambian feathers


  By Justin Rowlatt
  BBC News, Lusaka
  [​IMG]

  For many Chinese entrepreneurs, Africa is seen as a continent of opportunity. Now even small businessmen are arriving in force - and some local traders in Zambia just cannot compete.
  [​IMG] Traders sell almost everything in Lusaka's city market

  If you want to get an idea of how China is reshaping the world economy just try to buy a chicken in the Zambian capital, Lusaka.
  The city's main market is hot, humid and very, very busy.
  As you push your way through the crowds, the hawkers and traders will shout and cajole, offering you almost every product imaginable.
  You will probably not see a single non-African there. Until, that is, you get to where the chickens are sold.
  Here you will see a row of trucks piled high with cages, each packed with plump white chickens all fussing and squawking.
  The African shoppers will be weighing the birds in their hands and looking their prospective purchases in the eye.
  In the background you might spot the owners of the trucks - Chinese men and women holding wads of money and making sure things go smoothly.
  These people are chicken farmers.
  [​IMG] Please turn on JavaScript. Media requires JavaScript to play.
  </p>
  [​IMG]Click to play


  Click to play
  Mr Pan feels business opportunities are better in Lusaka than back home

  It sounds extraordinary but these Chinese businessmen and women spotted an opportunity to make a bit of money raising chickens on small farms in Zambia. They upped sticks and travelled 11,000km (7,000miles) from their homes to do just that.
  I got talking to one of the farmers, Pan Wei Zhi, a small, friendly man in his early 60s.
  Mr Pan invited me to visit the smallholding he and his wife run on the outskirts of Lusaka.
  As we sat together outside the tiny two-room house they share with their teenage son, I asked why the family had made this epic journey.
  "Simple," Mr Pan told me with a gentle smile, "because it is so much easier to make money here in Africa than back home in China."
  He said it cost $40,000 (£25,000) to set up their farm and within a couple of months they were already making a profit. Two years on and they are selling 2,000 birds a week.
  "At my age in China I can't do any serious work," Mr Pan said. "Here I don't feel old, I can still do something."
  Mr Pan may feel liberated by his African enterprise, but push your way a bit deeper into the market and you hear another side to the story, because the Chinese are not the only people who farm and sell chickens in Zambia.
  'Left destitute'
  Right in the centre of the market, down one of the unmarked narrow alleyways you will find the Zambian chicken traders.
  Some chicken traders are struggling to compete with their Chinese rivals

  You will know immediately if you are in the right place because there is a miasma of dust and feathers in the air and a terrible sour stench from the chickens.
  The chicken traders will probably be laughing and chatting in the shaft of bright sun that lights the alley, or in among their birds in the dark pens on either side, waiting for customers to push their way in.
  There are fewer of those than before, the traders claim, thanks to the arrival of Chinese chicken farmers.
  They say they are lucky to sell 50-100 birds each a week these days, and that it barely covers their costs.
  [​IMG] THE CHINESE ARE COMING
  Justin Rowlatt has been on a global journey to explore the effects of China's policy of "going out" into the world to secure the energy and raw materials its rapidly growing economy needs
  Episode one will be broadcast on Tuesday, 8 February, 2011 at 2100 GMT. Or catch up afterwards on BBC iPlayer

  [​IMG]

  Angolan railway's Chinese makeover
  Chinese karaoke fans sing Angola's praises
  An invitation to dine in the Amazon
  Brazil's Chinese bikini problem
  Difficult times for blue-collar America

  "They are going to drive us out of business," wails Mildred when I ask how she has been affected. "We'll be left destitute unless something is done."
  What she cannot understand is why anyone would want to travel halfway around the world to set-up a chicken farm.
  "If they want to have small, small businesses," says Mildred, exasperated, "let them go back to China and do those small, small businesses in China, not here."
  But Chinese migrants are now setting up small businesses across Africa. The latest estimates suggest there are more than a million Chinese people living and doing business on the continent. Most have arrived within the last 10 years.
  In the West it is the big infrastructure projects and huge mineral deals that set the terms of the debate about China's role in the world, this staggering migration tends to get less attention.
  But, in the long run, it may well be that the vast and growing diaspora of Chinese entrepreneurs like the Pans that will have the greatest impact.
  That is certainly what the Zambian chicken traders think.
  They may have been a bit complacent about their businesses, hidden away down their dark alleyway, but their growing anger at this new competition is very real.
  Mr Pan says he is not worried.
  "A few Zambian chicken farmers will probably go out of business," he concedes, "but that is what happens in a competitive market."
  He believes very passionately that his business is good for Zambia. "Our chickens are cheaper," he says, "and that means more people can afford them."
  I ask him whether he thinks more Chinese people will, like him and his wife, go out into the world to set-up businesses.
  "Chinese people have a bit more money now and China has become a powerful country," he tells me. "We will not get bullied and pushed around any more."
  There is no hint of threat in his voice. This is a statement of fact.
  How to listen to: From Our Own Correspondent
  BBC Radio 4: Saturdays, 1130. Second weekly edition on Thursdays, 1100 (some weeks only)
  BBC World Service: See programme schedules
   
 9. n

  nndondo JF-Expert Member

  #9
  Feb 8, 2011
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 1,250
  Likes Received: 535
  Trophy Points: 280
  Tanzania ni nchi yenye viongozi ambao akili zao ziko kwenye makalio na makalio ndio yako kichwani. Wakati dunia nzima inatafuta mbinu za kufanyabiashara na China Nyalandu anataka umaarufu kwa kuwafukuza. Halafu nchi nzima akiwemo rais anayedai kutokujua chochote wamekaa kimya. Huyu kijana mpenda sifa asiyekua na uwezo wa lolote na aliyeshindwa hata kumaliza shule kwa kubaka na kukimbia huko marekani anaachiwa akifanya kitendo cha hatari sana kwa nchi yetu.Wachina hawa ndio waliojenga reli ya Tazara na kutupatie mtambo wa kutengeneza vyuma wa ilipokua kilimanjaro machine tools, mtambo ambao waliotuoa kwa korea kusini na sisi tu katika nchi zote marafiki duniani, sasa huyu kituko katokea wapi na tunamlea. Actually kama ni lazima kufukuza watu Tanzania will be better kumfukuza yeye Nyalandu than hawa wachina. Tatizo letu sisi na huyu bwana mdogo ndio hatujui how to engage the chinese dawa ni kujifunza na sio kuwa fukuza. Eti unafukuza elimu kwa kushindwa kujifunza CCM tumechoka kusema jamani tuwatoeni tu kwenye madaraka ili tutende.
   
 10. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #10
  Feb 8, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,728
  Likes Received: 1,636
  Trophy Points: 280
  tukiwa tunaendelea na hii fukuza na wachina, tukumbuke kwamba wachina wameanzisha ukusanyaji wa taka zitokanazo na plastic hawali tulielezwa na wanamazingira kuwa taka za plastic zikichomwa ni hatali sana sasa wao wanazibadilisha ndala za Yebo Yebo, wanasaidia wazalisha taka wakina Mengi na Barehesa wanozalisha taka za plastic kwa chupa za maji. Hawahawa wanatufundisha jinsi na kuyeyusha chuma na kufanya ulembo mbali mbali wa chuka kama magaiti, milango na sasa hivi kuna milango inamwonekano kama ya mbao kumbe ni chuma tupu iko vizuri sana badala ya kuangaika Drilili unachukua mlango mzima unaweza usiite fundi ukabandika mwenyewe, Wachina wakwanza kuokoa mazingira ya TZ kwa kuwa wao wan chchu ya kugundua TZ kunaitajika nini, angalia Madrisha ya Alminium yalivyokoa ukataji wa miti hovyo kwa ajir ya mbao.
   
Loading...