Karejea upyaaa, wazee chadema na viongozi wakubali kufukia mabonde ya kijana wao

sixgates

JF-Expert Member
Mar 19, 2011
3,979
1,662
Zitto, naibu katibu wa chadema ambae hivi majuzi amewaaga wana wa chadema kigoma kaskazi baada ya kuongoza jimbo hilo katika vipindi viwili tofauti,taarifa za ndani sana zinadai sasa amerejea chadema na he is going to start over right from the scratch. Mwanasiasa huyu kijana ambae hivi majuzi alivuliwa nguo hapa JF kuwa ni mmoja wa wafadhili wa Masalia.. kwa taarifa za ndani zinadai, hana mpango wa kuacha siasa wala kuondoka chadema, ila kwa sasa ana kazi kuu moja kufanya matengenezo na kufukia mabonde yake ndani ya chama baada kupitia vipindi mbali mbali vya kupoteza imani ya wanachama haswa viongozi wake waandamizi kufikia hatua ya kutoifanya kazi yake ya unaibu ipaswavyo. Tayari ameshaomba nafasi ya kukaa karibu na viongozi na wazee ndani ya chama, na alilihitaji hiyo nafasi mapema na sasa ipo katika mchakato(ikumbukwe mbowe katika mkutano wa juzi hakupenda mjadala wa Zitto upewe coverage ili kuucha upepo upite wamalizane ndani ya chama). Taarifa za kuaminika kutoka kwa washauri wa Zitto zinadai hatagombea nafasi yoyote ndani ya chama,(unless atapewa shinikizo na wazee/baraza la ushauri).."Pengine hata yeye anajiuliza mbona yeye ni kiongozi mzuri lakini kila kukicha anakutana na setbacks ambazo kama kiongozi alipaswa nazo awe na uwezo wa kuzimaliza, but its consistent inamfanya aweke silaha chini, akaanze upya" chanzo hicho kilizidi kilidai. . Zitto hutamsikia kwa sasa akijadili habari za yeye kugombea urais, hutamsikia akizungumza habari ya kugombea uongozi ndani ya chama, ila anasubiri ratiba ya nguvu ya umma ikamilike utamsikia katika mimbari ya kisiasa mikoa ya tanzania akiipigania chadema..(Mark my words).. Ndiyo kauli ya mwisho nlioambiwa na mtu wa karibu sana na Zitto.

MY TAKE
Hivi urafiki wa Zitto na CCM(Kikwete) umeisha?

Je ni kweli anaweza akawa amemsikiliza Mama yake ambaye pamoja na wazee wengine walipewa kazi ya kuketi naye kitako wamsikilize na kumshauri?

Vipi nafasi ya masalia? Jee ni kwamba ameamua kumkataa shetani na kazi zake zote?

Ni wazi kuwa Zitto yupo comfortable kwa sasa, na strategy ya kurudi nyuma kuanza ku toil kwa ajili ya chama nadhani ni uamuzi mzuri.. Pengine mpaka ifike 2015 chadema ikashangaza watu ambao wanafikiri kitapasuka. Naona Zitto umri unakuja na busara,na pia nawapongeza viongozi wa chadema kwa kuamua kusolve hii issue ya Zitto kwa namna ambayo wapinzani wenu watakua confused wakiwa washachelewa!
 
afanye kazi ya kujenga na sio kubomoa chama chake,2015 atakuwa kwenye nafasi nzuri zaidi
 
Hii info is from reliable source.. Labda kama ni kweli Zitto Kabwe aje hapa sio kuthibitisha bali kuiweka sawa kama imekosewa.
 
Last edited by a moderator:
....... Kuwapa maadui wako wanachotaka"

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
afanye kazi ya kujenga na sio kubomoa chama chake,2015 atakuwa kwenye nafasi nzuri zaidi

Uyu jamaa in spite of every thing he is smart.. Ivi angekuwa anatumia hiyo akili kukijenga chama si wangekua mbali CDM?.. Mie yangu macho.
 
Vyovyote vile, zitto kayaacha mashirika ya umma hasa taasisi za vyuo vikuu vijiendeshe vikiumiza watumishi wake kwa kulipwa mishahara hiyohiyo tangu 2009 (Scale) na hajawahi kutana na viongozi wa wanataaluma asikie matatizo yaliyoko humo. Leo akisema anaenda kugombea urais tena kwakutumia nguvu nyingi kama anavyofanya sasa namshangaa. ANAFUATA NINI IKULU KAMA MASHIRIKA YA UMMA HASA VYUO VIKUU TU HAKUWAHI KUTANA NA WAFANYAKAZI AWASIKIE NA WAO BADALA YAKUSUIRI TAARIFA DSM KWENYE KAMATI YAO?
 
hatushangai siasa za udikteta za chadema Atakuwa amelazimishwa aseme hivyo.ili kunusuru CHAMA.Ukweli utajulikana siku za mwongo ni40
 
Km ndivyo na kajitoa kwa moyo wote ni habar njema kwa cdm na msumal kwa walokuwa wanaiombea mabaya cdm
 
Karibu tena kundini ZZK. Ila hili usafishwe dhambi zako inabidi ufanye malipizi. Adhabu yake inabidi ulete wanachama 150,000 kwa miezi mitatu kwa kuzunguka mikoa tofauti kupata wanachama wapya wa kuziunga Chadema na kufungua matawi. Naomba ukabidhiwe hizo kadi na vitendea kazi uanze mara moja. Baada ya hapo dhambi zako zote zitakuwa zimesamehewa
 
Namtakia heri, lakini asijisahau kwa kuwa: Historia huwa haina haja na wale wote
wenye kushindwa, labda tu kunukuu tarehe walizokutwa na umauti wao...
 
Kama ni kweli Zitto kamaliza sintofahamu hii nimefarijika sana maana namkubali na kumuamini sana jembe langu la ukweli.
 
Back
Top Bottom