Kardinali Pengo na Askofu Malasusa ni kielelezo cha unafiki wa viongozi wa dini

Sijielewi vp? Ndio maana tunapigania katiba Mpya sisi tunaojielewa maana kwa hiii tuliyo nayo hatuna chochote cha kuwafanya watawala hata wakiamua kuiuza nchi, wewe kenge ukiambiwa katiba Mpya unadai wananchi hawali katiba, halafu hapa unajamba ooo CAG sijui kafanya nini na ripoti yake. Jielewe wewe
Kwani Kenya si wamepata katiba mpya mbona kwao ufisadi upo juu sana je hiyo katiba mpya ya Kenya imeshindwa kumaliza ufisadi wa Kenya tukaitolea mfano inchi iliyokomesha ufisadi kwa kupata katiba mpya?
 
Hivi wakati huyu Msiba anatukana, kukashfu na kutishia watu, wao walikuwa wapi?

Maaskofu wa Kanisa Katoliki waliwahi kuandika Waraka kukemea maovu wakati wa Magufuli lakini Pengo aliukana waraka ule. Leo yeye wa kumwombea Msiba msamaha kweli?

Viongozi wa dini walikaa kimya hawakuonya chochote kipindi kile cha Giza wakati uovu ukitendwa hadharani au kazi yao SI kukemea Bali kuwaombea msamaha wahalifu wa wakati huo. Na kwa nini msamaha uwe ni kwa Msiba tu?

Kuna watanzania wangapi wameonewa lkn hawakuwaombea msamaha kwa waliowaonea?

Kama ni msamaha basi aliyestahili angalau kusikilizwa na kachero Membe ni ASKOFU MWAMAKULA kwani wote ni mashahidi alisimama na kweli hata kipindi kile tunapitishwa kwenye moto.

Msiba anastahili kulipa gharama za uovu wake Ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama zake. Kama ni msamaha huuombwa na mtu mwenyewe aliyekosa kwanza. Yule jeuri na mwehu hakuwahi kuomba msamaha licha ya nafasi aliyopewa.

Kila mmoja ataubeba msalaba wake mwacheni Msiba aubebe Msiba wake. Pengo na Malasusa acheni unafiki huu utaliangamiza taifa. Huyu kichaa SI wa kusamehewa hata kidogo.Au Hawa watumishi ni chawa wa Msiba?

Membe shikilia hapo hapo na mnada wa Mali zake za wizi urushwe live TBC taifa Kila mtanzania aone jinsi mshahara wa dhambi ulivyo mauti. Kwani wale waliomuunga mkono wako wapi Leo?
#membealipwetu#
Hapo hakuna kiongozi wa dini hata mmoja ni matapeli tupu
 
we ndiyo akili yako imeyumba, ameeleza vizuri sana kuwa walikuwa wapi wakati anadhalilisha wenzake? Km ni amani, ndiyo wanaona leo? Pengo yuko upande wa Musiba na Magufuli, alikuwa anafurahia Musiba alipokuwa anatumika kudhalilisha wazee waliotumikia nchi hii kumfurahisha Magufuli akifikiri Magufuli ni Mungu hatakufa. Viongozi wa dini wamejisahau nao wanaangalia maslahi yao
Well said
 
Kukemea ndio kumtukana rais Magufuli matusi leo unayaona makosa ya Musiba ila kina Mange kimambi na Tobias Marandu hukuona wewe na genge lako la nyumbu ndio wanafiki wakubwa na mmejaa uzandiki na visasi
ACHA matusi mkuu raisi magulpfuli hakuwahi kutukanwa na hao viumbe maana angewanyoosha bwana
 
Watanzania wengi ni WAPUMBAVU sana, ripoti ya C.A.G haijafanyiwa kazi. Gharama za maisha zimepanda sana kwa wananchi wa kawaida walio wengi na ufisadi kila sehemu. Wanasiasa wamewageuza wananchi mazuzu wanawachezesha gwaride wanavyotaka na JF yote kwenye siasa mnajadili watu wawili Membe na Misiba, mna akili kweli!?!?.., hakuna mambo ya msingi ya kujadili zaidi ya Membe na Musiba!?
Jikite kwenye mada. Mada iliyoko mezani inahusu maaskofu Pengo na Malasusa kumuomba Membe amsamehe Musiba.
Ripoti ya CAG na kupanda gharama za maisha, ni concern kubwa, tunapaswa kijadili barabara kwenye nafasi yake.
 
Maaskofu wa Kanisa Katoliki waliwahi kuandika Waraka kukemea maovu wakati wa Magufuli lakini Pengo aliukana waraka ule.
Haikuwa poa sana, nadhani hata kanisa lilikwazika. Nadhani around that time, (and partly for that reason) ndipo akateuliwa Ruwaichi kuwa askofu mkuu mwandamizi.
 
Mafisadi wanaendelea kupiga pesa na wewe usiyejielewa kodi zako zinapigwa umekalia kuandika uharo mitandaoni uliojaa chuki na visasi eti Membe shikilia hapo hapo itakusaidia nini sasa huku mafisadi wakiendelea kuchezea kodi zetu kwa raha zao
Kwani we hutoshi kuandika habari uzitakazo mpk utupangie na sie kuandika uyapendayo?
 
We Una akili timamu kweli, Dini kazi yake ni Amani, kazi ya kiongozi wa dini ni kusuruhisha whatever the case, ujinga umekujaa
Usijifiche kwenye kivuli cha amani ya dini kama mnataka amani si imetafutwa kwa mjibu wa sheria mahakama! Sasa zile kashfa za msiba kipindi kile zilikuwa na amani gani??? Na je mliiomba hiyo amani kwa waliokuwa wanachafuliwa?
 
Kukemea ndio kumtukana rais Magufuli matusi leo unayaona makosa ya Musiba ila kina Mange kimambi na Tobias Marandu hukuona wewe na genge lako la nyumbu ndio wanafiki wakubwa na mmejaa uzandiki na visasi
Na wewe nenda Mahakamani ukathibitishe hayo matusi alotukanwa marehemu wenu
 
Pengo na Malasusa ni viongozi wa dini vibaraka wa serikali, wamekuwa wakitumika na serikali waziwazi kuikinga kwenye kashfa zake pamoja na viongozi wao.
Right. Mchungaji anapaswa kulinda kondoo dhidi ya kila hatari, hata ikibidi kupoteza uhai. Wakati wa magufuli wachungaji walijificha uvunguni wakamwachia mbwamwitu akawatesa kondoo wa bwana.
 
Back
Top Bottom