Karatasi za kupigia kura zanaswa D’Salaam zikirudufiwa

Kilaza

JF-Expert Member
Feb 28, 2013
3,324
1,377
Wakuu

Leo nimeona kwenye magazeti mengi kuwa CHADEMA na UKAWA wamekamata masanduku ya kura huko Dar, sijashtuka sana kwasababu ndio mbinu waliyobakiwa nayo ili washinde lakini kweli hadi huku kwenye serikali za vijiji na vitongoji CCM wanaiba!

Mimi nilidhani ni uchaguzi mkuu tu ndio wanaiba kura kumbe hata huku chini hivi kweli CCM hamna hata mshipa wa aibu?

Swali la kujiuliza hii ni sehemu moja tu ambayo kura zimedakwa huko kwingine ambapo hakujadakwa hali ikoje?

Tume huru ya uchaguzi should be part of our nation agenda.



NB: CCM NI VIUMBE VILIVYOPO HATARINI KUTOWEKA
Karatasi za kupigia kura zanaswa D'Salaam

kova.jpg

Kamanda wa Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika kesho nchini kote
Dar es Salaam. Wakati Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ukitarajiwa kufanyika kesho nchi nzima, wafuasi wa (Chadema) na Jeshi la Polisi, wamekamata karatasi zinazodaiwa za kupigia kura kwenye uchaguzi huo za Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro, zikirudufiwa jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Katibu wa Chadema Jimbo la Ubungo, Justine Mollel, tukio hilo lilitokea juzi saa 12 jioni wakati mwanachama wa chama hicho alipokwenda katika duka la vifaa vya shule na ofisini saa 8 mchana kwa lengo la kurudufu karatasi za chama hicho lakini aliambiwa arudi saa 12 jioni.

Gazeti hili lilifanikiwa kuiona moja ya nakala hizo kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo ikiwa na nembo ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa, ikiwa na nafasi ya kupigia kura kwa wagombea wa CCM na Chadema.

Habari zaidi zinaeleza kuwa tayari zaidi ya nakala milioni moja zilisharudufiwa, huku zikiwa zimewekwa alama ya ndiyo kwa mmoja wa wagombea wa vyama hivyo.

Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura alisema: "Uchunguzi bado unaendelea kwani waliokuwa wanarudufu walijitambulisha kuwa ni wasimamizi wa uchaguzi, hivyo tunaendelea na uchunguzi na hakuna mtu tunayemshikilia."

Aliongeza: "Nimemwagiza OCD (Mkuu wa Polisi wa Wilaya) kuwasiliana na Tamisemi (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa) ili kujua hizo karatasi ni kweli zilitakiwa kutengenezwa hapo au la... Kama ni hapo mambo yaishie palepale na kama siyo halali basi hatua zichukuliwe kwa wahusika."

Mkurugenzi wa Uchaguzi katika Ofisi ya Waziri Mkuu Tamisemi, Khalist Luanda alisema kurudufu karatasi za kupigia kura kunatakiwa kufanyika katika wilaya au mkoa lakini siyo nje ya mkoa.

"Ni kosa kuchapa fomu za wagombea kutoka wilaya moja kwenda nyingine walipaswa kurudufu katika eneo kunapofanyika uchaguzi au wilaya husika na mchakato unaopaswa kuwa wa siri sana na siyo kila sehemu kwani haitakuwa rahisi kusafirisha kwa usalama bila kutiliwa shaka."

Aliongeza kuwa: "Nimesikia katika vyombo vya habari na nimetuma wataalamu wangu kwenda kufuatilia jambo hilo kwani ni makosa na mkurugenzi huyo inaonyesha alikuwa na malengo au masilahi binafsi na kama ni kweli anatakiwa kuwajibika."

Awali akisimulia tukio hilo Mollel alisema: MwanaChadema alikwenda pale kurudufu karatasi zake kwani gharama yake ni Sh25 kwa karatasi moja na aliambiwa arudi jioni kwani walikuwa na kazi maalumu, hivyo wasingeweza kumrudufia karatasi zake."

Aliongeza: "Alipokwenda tena saa 12 aliambiwa bado hawajamaliza kazi hiyo maalumu hapo alipata hofu na kuanza kuchunguza kazi iliyokuwa ikifanyika, ndipo alipoona karatasi za kupigia kura zikirudufiwa."

Mollel alifafanua kuwa alipoona hivyo mfuasi huyo aliwaita wanachama wengine wa Chadema waliozingira duka hilo lililopo maeneo ya Mabibo kabla ya kutoa taarifa Kituo cha Polisi Mabibo umbali wa takriban mita 100.

Alisema polisi wa Mabibo na baadaye wa Magomeni walipofika waliwachukua wahusika na kuwapeleka Kituo cha Polisi Magomeni kwa ajili ya kuandika maelezo.

Shuhuda ambaye hakutaka kutajwa jina lake alisema: "Niliingia dukani hapo nikakuta wanachapisha hizo karatasi, lakini sikujali sana kwani nilikuwa nina haraka zangu, lakini baadaye niliporudi nikakuta baadhi ya hizo nyaraka zikiwa mezani na ndipo nikagundua kuwa ni nyaraka za siri ambazo hazitakiwi kuonekana kwa muda huo."

Wakati huohuo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki alisema maandalizi kwa ajili ya uchaguzi huo yamekamilika kwa vifaa vyote kufika katika maeneo yatakayotumika kwa uchaguzi huo.

Alisema jumla ya wenyeviti wa mitaa 559 na wajumbe 2,795 wanatarajiwa kuchaguliwa. Jumla ya vituo 1,674 vya kupigia kura vitatumika huku masanduku yakiwa 5,022 na karatasi za kupigia kura zikiwa 1.7 milioni.

"Vituo vitafunguliwa kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 10 jioni, tunawaomba wananchi waliojiandikisha wajitokeze kupiga kura lakini wazingatie taratibu na sheria za uchaguzi," alisema Sadiki.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema, "Kila chama kihakikishe hakivunji sheria kwani hatutakuwa na hiana na mtu yeyote, ukienda kinyume tutakuchukulia hatua kali bila kujali chama ulicho na wadhifa wako."

Aliongeza: "Tunawaomba wanawake ambao mara nyingi wamekuwa waoga kwenda kupiga kura wakihofia usalama wao kujitokeza kwa wingi kwani tumejipanga vizuri kiulinzi kuhakikisha uchaguzi unaanza na kumalizika salama."

Chanzo:Mwananchi
 
juzi akina. laki si pesa walikuwa wanagombea chumvi geita na sijui kama alipona maana haonekani hata jukwaani
 
Last edited by a moderator:
Na Mkulu kabanwa tezi na mmarekani juu ya Escrow hahahahahaaaaa
 
Hv unafikiri mchawi ana aibu toka lini? Hawa ccm ni wachawi hawana huruma hata chembe 1, ondoa akili mwako kuwa wataleta maendeleo.
 
Hukumu nzuri ni ile anaepewa muhusika kukiwa na ushahidi wa kweli. Hawa wanaokamatwa kuhusika na ulaghai huu wananchi watumie sheria kuwahukumu na si kupeleka polisi panapopoteza ushahidi kila kukicha.
 
Ccm wana mbinu nyingi za kuiba kura ikiwemo kununua wagombea wa upinzani. Mfano kule nyasa komba kawapa rushwa ya bati na simenti wagombea wa upinzania wa cdm. Maccm hayana aibu kamwe kwenye rushwa.
 
Ccm wana mbinu nyingi za kuiba kura ikiwemo kununua wagombea wa upinzani. Mfano kule nyasa komba kawapa rushwa ya bati na simenti wagombea wa upinzania wa cdm. Maccm hayana aibu kamwe kwenye rushwa.

Geita wamegawa chumvi. Duh! Wasukumamnajidjalilisha sana! Mnauzaje utu wenu? Tena kwa chumvi tu?
 
Uchakachuzi kura za wajumbe BMK ushahidi tosha mchezo mchafu wa CCM tangu jadi hadi kesho. Mtu umemfumania live kachomeka, oh sijui kweli au wanataniana,oh maamuzi mahakamani. Watanzania tubadilike vinginevo CCM itatutia jiti hadi kingdom come.
 
Huwezi kuipa dhamana TAMISEMI iendeshe uchaguzi mkubwa kama huu...

Haina rasilimali kufanya zoezi hili kwa weledi...

Yaleyale...mazingaombwe TZ...
 
shame on you ccm hakika mtahukumiwa kwa maovu yenu ambayo mliyatenda toka mnaingia madarakani hadi siku mtakayotoka iwe mwakani au vinginevyo, kiukweli ni jambo la aibu kwa chama kikubwa na tawala kama ccm kufikia hatua ya kuchakachua hadi uchaguzi wa serikali za mitaa, ndio inafahamika ya kuwa ili uweze kujijenga katika uongozi sharti uwe vizuri kuanzia ngazi za chini ndipo utakapofanya vyema katika chaguzi nyingine za juu lakini siyo kwa chama kikubwa kama ccm ambacho kimeongoza taifa hili toka tunapata uhuru hadi sasa kufikia hatua ya kufanya huhuni wa mchana kama huu wa kudurufu karatasi za kupigia kura kutoka wilaya ya kilosa mkoani morogoro.
na kwa hali ya kawaida tafsiri ya hali hii ni kuwa imeonekana ccm katika sehemu kubwa wananchi hawaikubali ccm na ndio maana wanaamua kutumia njia ambazo siyo halali
 
Nyie chadema ni wapumbavu sana ongeeni hata mkijigeuza muongelee kwa huku nyuma habari ni kwamba CCM ndiyo baba yetu hamtapata kitu na mkiendeleza vurugu zenu mtaozea jela mamamamamaaae
 
Back
Top Bottom