Karaha za star times

Karaha za star times

Renzo

New Member
Joined
Sep 20, 2011
Posts
4
Reaction score
1
:israel:Jamani Leo nimeamua kufunguka kwenu pengine mtaweza kunisaidia! Tatizo langu ni huu wizi na ubabaishaji unaofanywa na Star Times Kama ifuatavyo:

  1. Bei inapanda asubuhi,mchana na jioni! Ilianza miaka 2 tu iliyopita ikiwa shs 9000, tukaona ni ukombozi wa mtanzania Kama Mimi nisiyeweza kumudu DSTV, Leo ni 52,000- sasa baada ya miaka 2 si bei itaizidi hata DSTV? Hivi si tuliahidiwa kuwa kuzimwa analogia sio kunyimwa habari? Sasa M-TZ si ni kanyimwa habari kijanja? Au anastahili tu kuona locals tena si zote - Sibuka Eti inabidi ulipe tofauti na Ina package yake yenyewe! Hivi hii si Kazi ya TCRA?
  2. Mvua ikinyesha tu ujue siku hiyo hakuna signal Kwenye stesheni nyingi, hasa zile maarufu hapa TZ, kwamfano ITV!
  3. Jua likiwa Kali sana, joto Au hata upepo kidogo tu, basi ujue hiyo TV siku hiyo ni kikohozi tu muda wote. Chanel nyingi zinafanya Kama zinakohoa kisha zinazimika... Au zinasena NO signal!
  4. Chaneli kadhaa zimewekwa Kama mapambo, hazijawahi kuonekana japokuwa zinahesabiwa katika channels tunazonunua - yaani Kama unasubscribe Mambo package, channel Kama WAP TV, STAR AFRICA2, STAR CHINESE 2, JIMJAM, etc. Ndio maaana nimesema ni wizi!
  5. Ni wababaishaji - vipindi vingi havina cha maana, hata series zinajirudia hizo hizo. Kibaya zaidi channel zilizoingiza Watusi Star Times kwa mfano AMC, MTV, Nikoledeon zimeondolewa bila taarifa. Hivi jamani, kwa kuwa Watanzania hatulalamiki ndio maana hakuna anayetuchukuliaseriously? Ninaamini sisi ni wateja, na Kama wateja tuna haki zetu and we should exercise our rights. Vipi consumer protection rights hazitulindi Wa Tanzania?
  6. Imefika mahali sasa tudai value for money. Tusiendelee kutoa hela zetu bure. Hii pesa ya siku hizi jamani imekuwa ngumu kuipata na tusikubali kuletewa substandard! Kukubali kuingia digital isiwe unyonyaji na udanganyifu-
  7. ninaomba wataalamu mnijuze ni Nini Ninachoweza kununua (sijui dikoda?) niweze kupata habari bila usumbufu - yaani nitakachonunua nisiwe tena na hizi karaha za kulipa hela kila mwezi Kama kodi ya nyumba ilhali huduma mbovu. Ningependa kuona locals mfano TBC, ITV, Channel10,star TV.
  8. wandugu -hebu nifarijini basi kwa busara zetu na tusaidiane. Kupata haki zetu. Wasalaam.
 
9. Ukikiwasha kwa masaa nane mfululizo kinajizima na ili kiwake mpaka ipite saa moja.

USHAURI WA BURE.
kama unajijua una hasira usinunue hiki king'amuzi. Ingia Azam stress free zone.
 
ndugu ihi nchi ni shamba la bibi,tcra ni kama hawapo,yuliambiwa na serikali kupitia naibu waziri wa mawasiliano bw makamba,kwamba serikali imeondoa ushuru wa vingamuzi kwaiyo bei itashuka kama yalivyokua matarajio ya wengi, lakini ndio bei imekua maradufu ya kabla ya kupunguzwa kwa kodi ya vingamuzi na serikali,alafu chakushangaza ivi vingamuzi vya startimes sio [hd] sasa nashangaa kwanini wanawauzia watu t1 kwa 10,7000 wakati wenzao wa [ting][contnental] wanauza [ting 90,000] [contnental 95,000]???na ivi ni [hd]? tatizo watanzania wengi hawana uelewa vitu ndio maana wananunua startimes ambayo ni t1 yaani kingamuzi cha kwaliti ya chini kabisa, tena kwa bei mbaya,wakati [hd] iliyo kwaliti bora na yenye ubora wa hali ya juu hawanunui wakati bei yake ipo nchini,sasa utaniambia kwa nini mchina asiwakamate wajinga?
 
Shortcut is the longest way you were not going....lakini vilevile kumbuka bure aghali ...!! Jipinde utoke na zuku
 
Bure ni Gharama. we ulidhani waliamua kulipia DSTV walikuwa wanataka kupunguza Msongamano wa Noti kwenye Vibegi na Wallet zao? ukiona huduma inatolewa kwa bei Rahisi lazima ujiulize kwanza kabla ya kukimbilia kupenda vya bure.
 
Nataka kununua Azam decoder soob,nijuze please!!
 
Muanzisha mada kwa kweli upo sahihi star time ni janga
 
Back
Top Bottom