figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,485
Heshima kwenu wakuu,
Kuna Mkuu wa Wilaya haonekani, inasemekana walienda kufukuza mifugo ilokuwa ndani ya hifadhi. Walienda leo, hadi sasa hawajarudi.
Nmepigiwa simu na mtu ambaye mawasiliano yake yanasumbua. Hadi sasa simu haipatikani.
Mwenye kupata details kuhusu hili swala atujuze.
Nadhani Moderators wataifanyia kazi.
Mimi nmeleta kapa Tip tu.
Habari zaidi ni kwamba, Zaidi ya askari 60 Mkuu wa Wilaya, maafisa wa Serikali na waandishi wa habari, wamepotea katika msitu wa Kimisi Wilaya ya Karagwe tangu saa nne Asubuhi katika operesheni ya kuondoa Mifugo.
=========
UPDATE:
Mkuu wa wilaya ya karagwe Godfrey Mheluka akanusha taarifa iliyosambaa kuwa yeye ,askari polisi zaidi ya stini pamoja na waandishi wa habari kupotea katika msitu wa kimisi ambao ni hifadhi ya Taifa wakati wakielimisha jamii kutoka katika msitu huo na kuhamisha mifugo yao bila shuruti hapo jana
Akizungumza na Times Fm Mheluka amesema hali ya mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha katika msitu wa kimisi ilisababisha uhalibifu wa miundombinu hali iliyopelekea watawanyike kwa makundi tofauti na kupanga sehemu ya kukutana.
“Kwahiyo katika hali ya kutawanyika kwenye msitu huo mkubwa na watu zaidi ya stini wengine wakawa wametawanyika kushoto ,kulia basi inaweza kutokea hali ya sintofahamu ya kufika sehemu mliyokubaliana kwa mda unaotakiwa basi hiyo ilileta tabu kidogo watu walijua kuna baadhi ya watu wamepotea ,mnamo saa mbili na nusu usiku tulikutana wote pamoja sehemu tuliyopendekeza’’ alisema Mheluka
Pia amesema kuwa hawa kwenda kufanya oparesheni kwenye msitu huo, bali walienda kutoa elimu kwa wananchi wanaoishi kwenye hifadhi hiyo ya taifa waweze tuondoka kwa hiyari yoa, na kuwasihi wananchi wanaoishi katika msitu huo watiisheria bila shuruti.