Karagwe: Mkuu wa Wilaya kapotea na Maaskari zaidi ya 60 Pori la Kimisi

Huyu PK siyo wa kucheka naye. JPM fanya mambo,tumwombe Mungu hawa vijana wetu wasidhuriwe na hawa Watusi.
 
Heshima kwenu wakuu,

Kuna Mkuu wa Wilaya haonekani, inasemekana walienda kufukuza mifugo ilokuwa ndani ya hifadhi. Walienda leo, hadi sasa hawajarudi.

Nmepigiwa simu na mtu ambaye mawasiliano yake yanasumbua. Hadi sasa simu haipatikani.

Mwenye kupata details kuhusu hili swala atujuze.

Nadhani Moderators wataifanyia kazi.

Mimi nmeleta kapa Tip tu.

Habari zaidi ni kwamba, Zaidi ya askari 60 Mkuu wa Wilaya, maafisa wa Serikali na waandishi wa habari, wamepotea katika msitu wa Kimisi Wilaya ya Karagwe tangu saa nne Asubuhi katika operesheni ya kuondoa Mifugo.
Inamaana na radio zimezima?
 
Possibly ni mkoa wa Kagera hiyo...in late 1999s ilishawahi kutokea kitu ya aina hiyo, but alikuwa ni OCD wa wilaya mojawapo mkoani Kagera!
Baadaye ilikuja kujulikana "alijipoteza" ili kupata kiki kwa IGP wa kipindi hicho, Mahita!
Haaaaa haaaa enzi hizo kiki zilijuwa hazilipi. Ila kwa sasa angepewa japo alinde geti la magogoni
 
Back
Top Bottom