Kapuni ya Global na Universities abroad

Kapuni ya Global na Universities abroad

drilling

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2016
Posts
4,905
Reaction score
5,088
Napenda kuuliza na kujua hizi kampuni ya Global na Universities Abroad zinazopeleka wanafunzi nje ya nchi wapo chini ya wizara ipi. Kama ukienda pale na ukalipa pesa lakini ukaona unazungushwa au kuna mambo huyaelewi niende wapi kupata msaada.

Kuna wanasheria wa kusaidia kujua haki zako na wanapatikana wapi na je kama chuo wanakupa mbaya ukaenda huko ukakuta sivyo walivyokuwa wakivitangaza havina ubora na masomo poor nifanye nini?

Naomba wanaofahamu wanipe waliyonayo
 
Ile kampuni ni wakala tu kama mawakala wa mabasi ubungo...yeye hajali unaenda kupata nini...yeye anachojali unapata nini...business oriented... Sijawahi kuwaamini...mbona sio mawakala wa vyuo kama havard au Massachusetts au Cambridge... Zaidi zaidi wao ni mavyuo vya chini vyenye elimu ya hadhi ya AMAZON COLLEGE au ZION COLLEGE(for African students)
 
Ata ivo ao m cjawakubali niloenda pale kuulzza mamb ya mkopo nkaona nkama betting vile yan ndan ya miez sab uwe imelud afu lazm uek bond dah yaaaan bola wngne
 
Kuna wanasheria wa kusaidia kujua haki zako na wanapatikana wapi na je kama chuo wanakupa mbaya ukaenda huko ukakuta sivyo walivyokuwa wakivitangaza havina ubora na masomo poor nifanye nini?

Naomba wanaofahamu wanipe waliyonayo

Hawa wana operate chini ya miongozo ya TCU. Hushiriki kwenye maonyesho ya serikali na wako karibu na TCU na NACTE. Hizi shughuli wamefanya kwa muda mrefu hivyo wana huduma ya kutupa. Wanaweza wasiwe na ubora wa 100% lakini uzoefu waliokuwa nao unasaidia wengi ambao wanataka kwenda kusoma nje.
Lakini pia sidhani kama kuna anaetaka kwenda nje au kupeleka mtoto nje ambae ni mbumbumbu kiasi ya kutoelewa mchakato haya makampuni wanayofanya. Wewe ndiyo wa kujua nini unataka na kama hujui wao watakushauri na wewe ni jukumu lako kupima.
Katika vitu vigumu kimoja wapo ni udahili haijalishi kama ni wa ndani au wa nje kwani taarifa nyingi za vyuo haziko kamilifu-ni kitu gani vyuo vinataka, program details ni vigumu kuzipata kwa mfano program structure, malipo yamekaaje etc hapa ndio hizi kampuni zinapoingia kurahisisha kazi. Wana ujuzi pia wa kusaka scholarship za aina mbali mbali.
Hivyo si busara kuwa diss bila kuwa na sababu za msingi.


Ile kampuni ni wakala tu kama mawakala wa mabasi ubungo...yeye hajali unaenda kupata nini...yeye anachojali unapata nini...business oriented...
Nimewasikiliza mara nyingi na ukweli ni kuwa wana ujuzi na kile wanachokifanya. Najua kama Global hufanya makongamano na potential clients na hutoaushauri kwa wanafunzi. Jambo moja husisitiza ni kupeleka mtu mwenye vigezo kwenye shule zinazo tambulika hapa nyumbani. Naongelea hao Global na UAR ambao nimewaona wakifanya shughuli zao.
 
Ata ivo ao m cjawakubali niloenda pale kuulzza mamb ya mkopo nkaona nkama betting vile yan ndan ya miez sab uwe imelud afu lazm uek bond dah yaaaan bola wngne
Mkuu najua ni haki yako ila si uandike kama msomi tu, maneno hayakamiliki kwa nini?
 
Back
Top Bottom