DR. MWAKABANJE
JF-Expert Member
- Nov 7, 2012
- 1,986
- 3,151
Huyu ni JUMA J. Kaponda Afisa Elimu wa Mkoa wa mbeya, kwa wanaomfahamu huyu jamaa ni hopeless, kwa neno jingine jinga la mkoa wa mbeya kwa upande wa elimu.
Kwanza amekuwa ni mbabe mno kwa walimu wa mkoa wa mbeya hakuna mwl. asiyemjua kwa ubabe wake, kitaalumu huyu ni mwalimu kutoka ngazi ya cheti hadi shahada mbili, pia amekuwa ni mpika migogoro sana, kwa mfano migogoro ya shule kama Mwakaleli nk. hasa ukizingatia ni mtu wa makundi hivyo huibuka kundi la wanaomsupport na kundi kubwa la wanaompinga, lakini ukizingatia walimu wengi ni waoga basi mambo yanaenda ndivyosivyo.
Leo katika taarifa ya habari asubuhi Star Tv. nimesikia taarifa ya utafiti wa shirika la maendeleo la Ujerumani likilipoti kuwa japo ufaulu wa wanafunzi wa darasa la saba kuongezeka katika mkoa wa mbeya lakini alama za ushauri zimeshuka kutoka daraja C kwenda D, na wakaenda mbali kwa kubainisha sababu ikiwa ni kama vile kushuka kwa morali ya kufanya kazi hadi kufikia 39%, sababu ikiwa ni pamoja na mazingira mabaya ya kufanyia kazi na sababu zingine kwani wamezitaja kwa kifupi, natumaini ukipata kuisoma utaona mambo mengi.
Kaponda ameonyesha kupeleka lawama zake kwa waalimu moja kwa moja, amesema umefika wakati wa kuwajibishana bila kufumbiana macho, mchangiaji mwingine akasema haiwezekani walimu wakadai madai yako wakati hawatimizi wajibu wao.
Binafsi napenda kumjulisha Kaponda kuwa mawazo kama yake ni ya miaka kama 60 iliyopita wasomi wakiwa wachache si kwa miaka kama ya leo.
Pili napenda kumkumbusha Kaponda kuwa, kama kunamtu anaharibu Elimu ya Mbeya ni yeye, ajitafakari Tangu ashike nafasi hiyo ni ubunifu gani ameleta ili kuinua kiwango cha elimu ndani ya mkoa wa mbeya?
Ajitafakari mahusiano yake na walimu ndani ya mkoa wa mbeya kwanza kabla hajaenda kwa waalimu moja kwa moja.
Kaponda na serikali kwa ujumla waangalie "root causes" za waalimu kushuka ari yao ya kufanya kazi baadala ya kuangalia tatizo hili juu juu vinginevyo tatizo litabaki kama lilivyo miaka nenda rudi kwa kuficha ukweli.