VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,908
Ya kwanza, elimu bure. Hakuna ukweli juu ya hili. Ilichofanya Serikali ni kufuta ada tu. Gharama nyingine zote zimeachwa kama zilivyo na zitaendelea kuwa mzigo mzito kwa wazazi na walezi. Wananchi walivutiwa na elimu bure. Kanyaboya!
Ya pili, kutumbua majipu. Wananchi waliamini haraka kuwa Serikali ya Rais Magufuli ilidhamiria kupambana na ufisadi na rushwa. Ilisifiwa kuwa ni Serikali ya kutumbua majipu. Kulifanywa kashkash za kasi TRA na Bandarini. Kumbe, walilengwa teamLowassa. Sasa pamekuwa kimya. Kanyaboya!
Ya tatu, serikali kubana matumizi. Serikali ya Rais Magufuli iliingia kwa kasi na mtazamo wa kubana matumizi Serikalini. Ikapiga marufuku hadi posho za vikao. Wananchi wakasifia. Baraza la Mawaziri likapunguzwa. Watu wakashangilia. Hao wanakaribia kulia kwa walichokisikia.
Makatibu wakuu na manaibu wao wameongezwa maradufu. Kwasasa, Mawaziri, Manaibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Manaibu wapo 85. Ni zaidi ya wale waliokuwa kwenye Serikali ya Rais mstaafu Kikwete. Kanyaboya!
Ya nne, ilidhaniwa kuwa Serikali ya Rais Magufuli ni ya kidemokrasia. Ilionwa kama inayokuja kuimarisha ushindani wa kidemokrasia huku nchi ikisonga mbele. Lakini, Waziri Mkuu amepiga marufuku mikutano ya kisiasa nchini. Ndiyo kusema, amepiga marufuku demokrasia. Serikali inataka kutamba tu yenyewe kadiri itakavyo. Kanyaboya!
Nawatakieni heri ya mwaka mpya!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam