Kanyaboya bora za 2015, karibu mwaka mpya

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Ya kwanza, elimu bure. Hakuna ukweli juu ya hili. Ilichofanya Serikali ni kufuta ada tu. Gharama nyingine zote zimeachwa kama zilivyo na zitaendelea kuwa mzigo mzito kwa wazazi na walezi. Wananchi walivutiwa na elimu bure. Kanyaboya!

Ya pili, kutumbua majipu. Wananchi waliamini haraka kuwa Serikali ya Rais Magufuli ilidhamiria kupambana na ufisadi na rushwa. Ilisifiwa kuwa ni Serikali ya kutumbua majipu. Kulifanywa kashkash za kasi TRA na Bandarini. Kumbe, walilengwa teamLowassa. Sasa pamekuwa kimya. Kanyaboya!

Ya tatu, serikali kubana matumizi. Serikali ya Rais Magufuli iliingia kwa kasi na mtazamo wa kubana matumizi Serikalini. Ikapiga marufuku hadi posho za vikao. Wananchi wakasifia. Baraza la Mawaziri likapunguzwa. Watu wakashangilia. Hao wanakaribia kulia kwa walichokisikia.

Makatibu wakuu na manaibu wao wameongezwa maradufu. Kwasasa, Mawaziri, Manaibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Manaibu wapo 85. Ni zaidi ya wale waliokuwa kwenye Serikali ya Rais mstaafu Kikwete. Kanyaboya!

Ya nne, ilidhaniwa kuwa Serikali ya Rais Magufuli ni ya kidemokrasia. Ilionwa kama inayokuja kuimarisha ushindani wa kidemokrasia huku nchi ikisonga mbele. Lakini, Waziri Mkuu amepiga marufuku mikutano ya kisiasa nchini. Ndiyo kusema, amepiga marufuku demokrasia. Serikali inataka kutamba tu yenyewe kadiri itakavyo. Kanyaboya!

Nawatakieni heri ya mwaka mpya!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
Umenena Mkuu, Ipo siku wasioona watakumbuka uzi huu.
 
Kanyaboya nyingine ni hii Ya kumteua waziri mkuu mkiristu na waislamu wakaona ni mwenzao kisa anaitwa Kassimu kumbe jamaa ni murtadi!!Teuzi zote zina harufu kali ya Mfumo Kristo.
 
Pole sana. Afadhali leo umejitokeza kwa ngozi yako halisi. Nenda zako UKAWA. Hapa Kazi Tu
 
Kanyaboya nyingine ni hii Ya kumteua waziri mkuu mkiristu na waislamu wakaona ni mwenzao kisa anaitwa Kassimu kumbe jamaa ni murtadi!!Teuzi zote zina harufu kali ya Mfumo Kristo.

Uwongo mwingine jaman. Usifikie huko jamaa ni Muislam
 
Kanyaboya nyingine ni hii Ya kumteua waziri mkuu mkiristu na waislamu wakaona ni mwenzao kisa anaitwa Kassimu kumbe jamaa ni murtadi!!Teuzi zote zina harufu kali ya Mfumo Kristo.
Kwani rais alikuwa anateua imamu wa Msikiti mpaka aangalie kwanza kama ni muislamu kweli au muislamu jina?
 
Ya kwanza, elimu bure. Hakuna ukweli juu ya hili. Ilichofanya Serikali ni kufuta ada tu. Gharama nyingine zote zimeachwa kama zilivyo na zitaendelea kuwa mzigo mzito kwa wazazi na walezi. Wananchi walivutiwa na elimu bure. Kanyaboya!

Ya pili, kutumbua majipu. Wananchi waliamini haraka kuwa Serikali ya Rais Magufuli ilidhamiria kupambana na ufisadi na rushwa. Ilisifiwa kuwa ni Serikali ya kutumbua majipu. Kulifanywa kashkash za kasi TRA na Bandarini. Kumbe, walilengwa teamLowassa. Sasa pamekuwa kimya. Kanyaboya!

Ya tatu, serikali kubana matumizi. Serikali ya Rais Magufuli iliingia kwa kasi na mtazamo wa kubana matumizi Serikalini. Ikapiga marufuku hadi posho za vikao. Wananchi wakasifia. Baraza la Mawaziri likapunguzwa. Watu wakashangilia. Hao wanakaribia kulia kwa walichokisikia.

Makatibu wakuu na manaibu wao wameongezwa maradufu. Kwasasa, Mawaziri, Manaibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Manaibu wapo 85. Ni zaidi ya wale waliokuwa kwenye Serikali ya Rais mstaafu Kikwete. Kanyaboya!

Ya nne, ilidhaniwa kuwa Serikali ya Rais Magufuli ni ya kidemokrasia. Ilionwa kama inayokuja kuimarisha ushindani wa kidemokrasia huku nchi ikisonga mbele. Lakini, Waziri Mkuu amepiga marufuku mikutano ya kisiasa nchini. Ndiyo kusema, amepiga marufuku demokrasia. Serikali inataka kutamba tu yenyewe kadiri itakavyo. Kanyaboya!

Nawatakieni heri ya mwaka mpya!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Mimi siwezi na sitolaumiwa na ulmwengu kwa kuichagua
 
Kanyaboya ya majipu naikubali,haiwezekani majipu yaonekane Bandarini,Reli halafu Mwakyembe awe mtu makini.kwani Mpango alikuwa na cheo gani TRA?Kama mambo hayakuwa vizuri,je ni Bade pekee alifanya haya?
 
Back
Top Bottom