Kanuni ya Mwisho ya Akili na Ulimwengu na Mambo ya Muhimu kuyakumbuka

Mkuu tumemiss masomo yako intelligence imepooza fanya kurud na nondo 1 basi.
 
Mawazo ni uhalisia.
Mawazo ni uhalisia unaosubiri muda fulani na space kufika na uhalisia huo kuonekana katika ulimwengu wako. Kinachofanya uone mawazo sio uhalisia ni muda. Kama kungekuwa hakuna kipindi fulani cha wakati baina ya kilichopo akilini mwako na uhalisia wako ungeona ni kitu kimoja, lakini kutokana na muda unaona ni viwili tofauti na unaweza ukabisha. Inahitaji umakini wa kijitambua, kujichunguza na kuwa mvumilivu muda ufikapo utaona uhalisia wake. Leo hii unaweza ukawa ulishasahau experience hii kama uliwahi kuiwaza, au labda uliwahi kuamini hivi, n.k na vyote hivi vinakujengea ulimwengu na experience hii ya sasa huku ukiwa umeshasahau kama experience hii ilikwepo katika ufahamu wako au kulikwepo na uhalisia huu lakini hukuweka umakini kutambua.

Kama unakumbuka kanuni ya kwanza "KILA TENDO LINA MATUNDA YAKE/ CAUSE AND EFFECT/KILA JAMBO LINA CHANZO CHAKE". Chanzo hakina tofauti na tokeo. Ukipanda maembe utavuna maembe kwani chanzo hakina tofauti na matokeo. Tofauti inaweza kuwepo kwenye hali au vitu lakini usawa ni lazima utakwepo. Hivyo kama chanzo hakina tofauti na matokeo, chanzo na matokeo ni kitu kimoja bali kinachofanya tuone ni tofauti ni wakati wa utimilifu wa tokeo baada ya chanzo kuwepo.

Dunia yako ya ndani haina tofauti na dunia yako ya nje. Lakini kutokana na wakati na space (time and space) inakuwa ni ngumu kuwaza kuangalia tokeo kulinganisha na chanzo.

KUMBUKA:

  1. Kila jambo, kitu au hali kina Chanzo.
  2. Wewe ndiye mfikiriaji wa pekee na hakuna anayeweza kutumia akili yako kufikiria na kufanya maamuzi kwa uwezo sawa ulio nao wewe katika kutumia akili yako.
  3. Chochote unachokiwekea umakini huchukua nafasi kubwa katika uhalisia wako.
  4. Kilichopo katika ulimwengu wako wa ndani hutengeneza uhalisia wako wa nje yako.
  5. Hakuna chochote cha kubadilisha nje yetu bali kubadilisha reality yetu huanza kwa kubadilisha ulimwengu wa ndani kwanza.
  6. Kutokana unawaza kila wakati na mara nyingi kuna kinachoendelea akilini basi na kila wakati na kila jambo linapoendelea akilini huweka uhalisia fulani katika maisha yetu na mtazamo kwa ujumla.
  7. Huwezi kuwa na hisia bila wazo la hisia hiyo. Huwezi kuwa na hisia fulani bila kuanza kuwa na wazo lake kwanza au bila wazo lake kuwepo kwanza.
  8. Unaweza kubadili mtazamo, wazo, fikra kwa kuweka mtazamo kwenye fikra unayotaka na ile fikra ya zamani kuondoka yenyewe kwa kutawaliwa na fikra mpya.
  9. Like attracts like.
  10. Mawazo, Hisia, Fikra, au Imani sio vitu vya kuvipuuzia.

Kumbuka sheria za Akili haziangalii unajua sheria hizo au haujui, hazibagui wewe ni nani, hazina utofauti na matokeo na hutokea automatically.

Vitu vya kuweka akilini na kushikialia.

  • Ni vyema kujaribu mwenyewe na kuangalia je kuna ukweli wowote. Unaposoma na kuacha kama ilivyo au unaposikia na kuacha kama ilivyo au kujaribu mara moja sio sahihi. Jaribu kuweka mwaka mmoja, kwa kujichunguza mawazo yako, imani yako, fikra na msimamo wako, matendo yako na maneno yako. Chunguza kwa kina, tazama ulimwengu wa nje na uhusiano uliopo na ulimwengu wa ndani na jaribu kurekebisha fikra zako, mitazamo na kujipima utagundua mengi zaidi.

  • Leo hii unaweza ukaona ni kitu cha ajabu, lakini amini nakuambia kuwa elimu hii hapo kale haikupatikana huru kama hivi. Ni elimu iliyokuwa inafundishwa kwa siri, mafumbo na wapo waliokuwa wanachomwa moto kusema haya.

  • Pia cha mwisho ninapenda sana kuwasisitiza, tujichunguze kwa kina ndani yetu, tutambue uridhi tulio nao kujitambua, kuweka mawazo, matendo na maneno sahii na umakini. Tutumie akili yetu kuendelea zaidi badala ya kuendelea kuwa watumwa wake. Baada ya kujitambua ndipo tutatambua ukuu wa ulimwengu na tutatambua ni kwanini tumeumbwa kwa sura na mfano wake yeye aliye INFINITY.

mshuku wa mangi paul
 
Nimesoma mara mbili nikaelewa zaidi. Sasa nahitaji kujua zaidi kuhusu TIME AND SPACE.
Vinafanyeje kazi, ni vitu gani, kwanini n.k
Wale waliosoma quantum physics watusaidie hapa
 
Asantee..
Nadhani inafahamika dhahiri kuwa miaka na miaka watu maalumu walioweza kufunuliwa walishauri sana mwanadamu kutenda mema na yanayostahili. Ni kwanini? Unafikiri walikuwa wajinga au waliona nini baadaye? Ni kwasababu waligundua umuhimu wa kutenda hayo. Fikiria ulimwengu ungekuwaje bila watenda mema? Ungekuta vita, kuuana, uharibifu, na kungekosekana amani. Hivyo matendo mema ni msingi mkuu wa kutusaidia kuishi katika kuitafuta furaha yetu ya moyoni huku tukiwa hatuharibu furaha ya mwanadamu mwenzako.

Malipo ni hapa hapa duniani. Maisha ya mwanadamu katika dunia ya chini, kutokana na matendo yake, maneno yake na ufahamu wake vinabeba energy sawa na matokeo yake. Kuishi kwa kuhakikisha unaishi katika haki hukusaidia kujitambua, kufahamu maisha yalivyo, kuwa tayari kusurrender kwa chochote haushikiliwi na tamaa za kidunia na mwili, unaweza kuiongoza akili yako na mwisho wa maisha yako ufahamu wako unakuwa mwepesi kurudi katika ulimwengu mkuu au unaweza ukawa mwepesi kuchagua form mpya ya uhali kutokana na kiasi cha mema uliyonayo.

Anayeishi kimakosa utagundua anafanya matendo kuutumikia mwili, anaona furaha ni kuutumikia mwili kwa kuupata raha unazotaka kwa kutumia milango yake ya ufahamu, anaharibu furaha na amani za wanadamu wengine, huyo Karma yake au matokeo ya matendo yake hupelekea nafsi yake kuwa nzito na kushikiliwa na mwili hata baada ya kifo, wengine walioweza kuona maisha ya mbele zaidi huamini kuwa ataendelea kuzunguka kama roho akiteseka kukosa mwili, wengine huingilia wanadamu wadhaifu (ambao kwa baadhi ya imani huitwa mapepo), wengine hukaa makaburini kuuzunguka mwili uliokuwa wake kwa zamani na huteseka kwani hawana uhuru kama waliokuwa nao wa kutumia milango ya ufahamu ya kimwili na hawawezi kuonekana wala kuingilia ulimwengu wa kifizikia. Baada ya muda fulani kutegemeana na energy waliyotoa katika matendo yao, mawazo yao na maneno yao, huzaliwa katika form mpya ya uhai na kupewa mwili wa uhai wowote kwa ufahamu mdogo bila kujitambua, na kuendelea kuzunguka maisha na kujifunza mengi mfano kuna waliokuwa wakatili wakazaliwa wanyama katika familia za zinazokula nyama na kuchinjwa kama walivyofanyia wengine, wengine huzaliwa katika hali mbaya au kuishi kwa muda mfupi kutegemeana na karma yake au matokeo yake ya zamani.

Kuishi kwa nidhamu ya uoga sio tatizo. Haijalishi wewe ni imani gani kinachojalisha ni matendo yako. Hivyo kama matendo yako yalikuwa sahihi na uliitumikia nafsi zaidi ya tamaa za mwili na dunia basi baada ya maisha Ufahamu wako huweza kuexperience hali nyingine nzuri kutokana na mema yako. Mema na mazuri yako hayatakutupa kamwe popote uendapo. Ni kama vile ukipanda maembe ni lazima utavuna maembe huwezi kuvuna au tunda nje ya maembe.

Hapa ni kwa wale ambao wameweza kufunuliwa. Mfano kwa waliofikia Enlightenment wanafahamu maisha yao yaliyopita, wanafahamu stage walizopitia na kila life form. Wanakuwa wamepata kumbukumbu ya maisha yao yote, wanakuwa wamejitawala kiakili, kimatendo, kimaneno, na hutafuta furaha ya ndani mwao bila kutoka nje yao. Wengi hawa baada ya maisha hufikia level sawa kama Eternal Bliss au wengine hurudi katika source kuu ya ufahamu (The devine) na kuwa kitu kimoja.

Lengo la maisha ni kujitambua, Maisha ni Ufahamu unapewa Matter kujiexperience lakini katika msitu wa Ujinga, Tamaa, Mazoea na illusion. Lengo ni kujitambua na kutoka katika kifungo hicho kurudi kwenye uasili yako (Devine/Utakatifu mkuu).

Tatizo sio unaamini nini, tatizo ni unatenda matendo gani, unajifahamu kiasi gani, umejichunguza kiasi gani, kufahamu kinachoendelea akilini(ndani yako), na kimatendo. Kama umeishi katika haki bado future yako itakuwa katika haki.

Elimu kama hiyo inapatikana kwa Gurus, waliokuwa Enlightened, na walioweza kuexperience Meditation kwa muda mrefu. Kwani wanakuja kufahamu undani na kilichopo ndani yao vyema, na kufahamu wao ni nani badala ya kujifahamu kupitia mwili, tamaa, mawazo, mazoea na kadhalika.

Cha msingi unaamini Imani gani sio tatizo, tatizo ni kutenda yanayostahili. Yote ni kuandaa maisha baada ya kifo ufahamu (consciousness) yako iende palipo sawa kwani maisha ni mafupi sana na tunayutumia kufahamu nini lengo lake.

KUZALIWA MWANADAMU NI LEVEL YA JUU SANA YA UFAHAMU, NI LEVEL AMBAYO UNAWEZA KUBADILI DESTENY YAKO NA KUTUMIA MAISHA YAKO KUAMKA.
 
Back
Top Bottom