nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,862
- 5,797
Steven Kanumba
Kwa mujibu wa maombi yake kwa mashabiki wake, sasa Muigizaji Steven Kanumba analazimika kufanya kazi na msanii, Ramsey Nouh kutoka Nigeria.Kanumba kupitia mtandao wake aliwaomba mashabiki wamchagulie staa mmoja wa filamu barani Afrika ili afanye naye kazi na wamemchagulia Ramsey Nouh.
Katika ombi hilo aliorodhesha majina ya wasanii watatu wakubwa kutoka Nigeria na Ghana ambao ni Desmond Elliot, Ramsey Nouh na Van Vicker.Mashabiki wake wengi wamependekeza Ramsey Nouh huku wakimtaka atumie lugha ya kiingereza katika filamu hiyo ili iweze kubamba sehemu kubwa ya bara la Afrika na duniani.
Ombi lake kwenye mtandao lilikuwa kama hivi;
"Kwa mwaka huu nimepanga kufanya kazi na msanii mmojawapo kati ya hawa hapa Desmond Elliot, Ramsey Nouh au Van Vicker,Sasa nakupa nafasi kwa wewe shabiki wangu kunichagulia ni yupi ambaye ungependa kuona nafanya nae movie kwa mwaka huu nami nitatimiza ahadi,
filamu itahusu mambo ya 'secret society' yaani jamii fulani ambayo haiamini Mungu kabisa bali shetani na wamefanikiwa kuiteka dunia kwa 'power',pesa,umaarufu na 'technology' ambao pia wana ishara zao na ibada zao.
Pia amewaomba mashabiki wakae kupendekeza jina la filamu hiyo ambayo anatarajia kuifanya baadae mwaka huu. Bado anakaribisha maoni unaweza kumuandikia kupitia info@kanumba.com This e-mail address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it .