Mgombea Uenyekiti CHADEMA Kansa Mbarouk amejitapa atalindwa na Msajili wa vyama vya siasa Francis Mutungi endapo kama Kamati ya uchaguzi ya chama hicho itaondoa jina lake kwa kukosa vigezo
Akizungumza na Radio VOICE OF TABORA Kansa Mbarouk amesema endapo kama jina lake litaondolewa atashtaki kwa Msajili wa vyama Francis Mutungi na anaamini atarudisha jina lake kwani anayo Imani kubwa na Msajili huyo.
Amedai anafuatilia kwa ukaribu kila kinachoendelea katika uchaguzi wa chama chake na atawasilisha ripoti kamili kwa Msajili wa vyama.
Mbarouk amedai kufurahishwa na kauli ya Msajili Francis Mutungi aliyoiotoa leo kuunga mkono Pingamizi lake dhidi ya Mgombea Uenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe.
Kansa Mbarouk amekuwa akidaiwa kuwa ni mwanachama wa chama cha ACT Tanzania chama kinachosemekana kufadhiliwa na CCM
MY TAKE:
Ni wazi sasa ofisi ya Msajili wa Vyama imejiweka wazi kwamba inatumiwa na maadui wa Chadema kuangamiza chama hiki.Kitendo cha Msajili Francis Mutungi kuchekelea pingamizi dhidi ya Mbowe ni kujianika wazi yeye ni kati ya maadui wa Chadema.
Huyu Kansa Mbarouk amekuwa akifanya kazi za CCM kupitia ACT pale Tabora kwa muda mrefu na ameshahojiwa na chama mara kadhaa.Ni demokrasia tu ya Chadema iliyovuka mipaka kumuacha Mbarouk kuwa ndani ya chama hiki mpaka leo kwani alitakiwa awe amefukuzwa siku nyingi.
Nimhakikishie tu Msajili Francis Mutungi kwamba mbinu zinazoratibiwa na ofisi yake kwa kushirikiana na CCM kamwe hazitafanikiwa kuvuruga Chadema.Zitashindwa kama mbinu nyingine zilizowahi kufanywa!!