Kaniwekea dawa za kulevya kwenye wine na kunibaka

Nawashukuru wote kwa ushauri na mawazo yenu, nipo kimya kwa kuwa sio rahisi kama mnavyofikiri, mmeuliza vitu vingi nimeshindwa hata namna ya kujibu, naomba nijibu machache

Hospital nilipewa contact za watu wa counseling, na ninaendelea vizuri, ndio maana nimepata hata nguvu za kuandika haya yote, mwanzo nilikua vibaya sana

Dalili za huyu jamaa kunihitaji zimekuwepo siku nyingi sana, ingawa hakuwahi kutamka, lakini amekua akiniomba kutoka outing mara kadhaa, hata hivyo outing za wawili tu nimekua nikizikataa, ila za wengi kama kundi la marafiki na kadhalika ndio nakubali, ila yeye na mm tu hapana

HIV nilipimwa nikawa sina, ila natakiwa kupima tena march,
Ingawa siwezi kuita ni upendo moja kwa moja, ila huyu bwana kama angenihitaji ningeweza kufikiria ombili lake, urafiki wetu wa kawaida ni wa siku nyingi, mwenendo wake ulionesha ipo siku atanitamkia, kwa kuwa hakuwahi kutamka niliendelea na maisha yangu bila kumfikiria, hivyo tukaendelea na urafiki wa kawaida wa kupeana lifti

Kuhusu mchumba wangu, pamoja na kuwa tumedumu kwa 3 yrs, lakini amekua mgumu sana kufikia maamuzi ya ndoa, mara kwa mara anaanzisha process kabla ya aadae kudai tusubiri kwanza, hadi wazazi wameshachoka nae, sasa hatujui safari hii yupo serious au la? Ndio maana huyu staff mwenzangu kama asingenifanyia kitendo cha kunibaka basi kwa asilimia kubwa nilikua tayari kumpa nafasi maana nimemsoma tabia hivi hivi tukiwa marafiki wa kawaida na kumuona ni mtu mzuri, kaja kuharibu kwa kitendo hichi alichofanya ambacho kimemuondolea heshima zote

Kuhusu polisi, mm ndie nilitoa report na kupewa pf 3 kwa ajili ya matibabu, hivyo kesi haijafikishwa mahakamani bado, lakini vielelezo vipo, polisi pia nimewaeleza kama hivi nilivyoeleza hapa, hivyo kwa mazingira ya tukio hii situation ni very tricky wakasema, baada ya majadiliano ya kina kati ya afisa upelelezi, mpelelezi, dawati la jinsia etc, wameomba nitafakari mwenyewe kama nina nia ya kuendelea na hii kesi au la? Ili ikishaanza nisiwasumbue tena, angalizo hili limetokana na historia yangu na huyu mbakaji, wao hawana tatizo, maana report ya doctor ipo na vielelezo vingine ie sms ambazo jamaa anaendelea kunitumia akiniomba msamaha akitaja tukio husika

Hivyo polisi hawawezi kuendelea na kesi bila mm shahidi namba moja kuonesha nia ya kesi, ni lazima wanisikilize mm

Katika mazingira haya ndipo nikaja kwenu, sikua na uamuzi, ila baada ya kupitia comments zenu nitapata muafaka, ingawa napitia hard time psychologically

Thanx
Mi nilisoma hadi page ya 6 nkitafuta majibu yako ikabidi ni jump hadi ya mwisho ndo nimeyakuta.

Nachokushauri mimi MSAMEHE tu huyo jamaa mana anaonesha kweli alikua na nia na ww ila ndo alikua mzito na ww hukumpa sana attention

Pili kubakwa ni psychologicaly mentality ambayo ukiamua kuifuta kwenye mind yako basi ni suala la sekunde 1 tu

All in all nakutakia kila la heri mdada

Mwamba
 
Mwishoni mwa mwezi December baadhi ya wafanyakazi tulikubaliana weekend moja tukae pamoja kama party get together, tukachagua hotel moja tukaenda, tulikua kama 18 hivi, kila mtu alijigharamia mwenyewe kula na kunywa, kuna mkaka mmoja huwa napanda sana lift yake kwenda kazini karibu kila siku, anaishi Tegeta, hivyo huwa nasimama Bamaga ananipitia hapo, siku ya get together alinipitia pia tukaenda wote.

Kwenye saa nne tukaanza kutawanyika, yule jamaa akadai nisubiri nisiwe na haraka atanifikisha hadi nyumbani, mwisho tukabaki watatu, jamaa yake mwingine, yeye na mimi, muda wote nilikua nakunywa non alcoholic drinks, mimi ni mnywaji wa pombe kwa muda mrefu, wine, savana etc, ila siku hiyo sikutaka kabisa kuonja pombe, jamaa akanibembeleza sana ninywe hata glass moja ya wine inatosha, nikakubali, cha kushangaza akaenda kuifuata yeye mwenyewe kaunta.Baada ya trip tatu hivi nikasikia usingizi mzito sana, nimekuja kushtuka saa saba mchana kesho yake, Tegeta nyumbani kwa yule jamaa, nikiwa na kizungu zungu, sina nguvu, malaria si malaria.

Kibaya zaidi nipo uchi kitandani, nikiwa nimechafuka, nilikua peke yangu, nikajiuliza glass moja ya wine inaweza kunifanya hivi? Nikavuta picha nikagundua kuna kitu nimefanyiwa, yule bwana akaingia na supu kwenye hotpot na kuniomba nioge ninywe supu, nikavaa nguo bila kuoga na nikakodi bajaj hadi nyumbani, sikupata nafuu kabisa, kichwa kilikua kinauma mno, nikalazwa hospital siku tatu ndipo nikapona, yule bwana kwa siku tatu zote alikua na mm hospital, wazazi wanaishi mkoa, mm nimepanga bamaga mwenge, nilikua na PF3 na report ya doctor, ambayo ilionesha wazi nilikua na kiwango kingi cha dawa za kulevya mwilini, na nimeingiliwa

Kuna maelezo mengi sana ila naomba nifupishe.

Kazini hawajui chochote kuhusu hili suala, nilihofia maneno ya watu, maana mimi na yule alienibaka tunafanya kazi pamoja ila yeye ni manager ni bosi, report zote ninazo na mpelelezi wa kesi ana copy pia, nilimuomba mpelelezi asubiri kwanza, kama aendelee au la, sababu ni kuwa, huyu jamaa ameniomba na kunibembeleza sana nisiendelee na kesi hiyo, kwamba nitamuharibia kazi na future yake, kwamba alinipenda siku nyingi na alishindwa tu kuniambia ndio maana alifanya vile, ili kuthibitisha hilo twende wote mkoani akafanye taratibu zote za ndoa tufunge ndoa.

Hata hivyo mimi nina mtu wangu wa miaka 3 sasa, ambae alishapeleka uchumba mwaka jana July, akadai bado anajipanga tumpe muda, yeye haishi Dar huwa anakuja kunitembelea na kuondoka na yeye hajui chochote kuhusu yaliyonipata.

Nipo njia panda nahitaji msaada wenu

Asanteni

Pole kwa masahibu yaliyokukuta..binafsi napenda kujua vitu vichache kutoka kwako mleta sredi

  • Kuna interval gani tangu umebakwa hadi uliporipoti hospitali
  • Ulipewa PEP yoyote kukukinga na maambukizi?ni ipi?

Karibu
 
Yah, nilipata PEP baada ya kipimo cha HIV ndipo nikapewa dawa kwa ajili ya kinga, wakasema napaswa kupima tena mwezi march

Nilikwenda hospital jioni ya siku hiyo hiyo ya tukio maana nilikua najisikia vibaya sana, hospital wakasema ni sababu ya dawa za kulevya hazijaisha mwilini nikapewa drip, siku tatu mbele ndipo nikatoka hospital
 
Mbona iko wazi sana, NYIE KINA DADA, hamna cha bure kwa mwanaume! Akikupa kitu hata lift, UTALIPA TU, hamna jinsi hapo!
 
miaka mitatu kwenye mahusiano???? ulikua unasomea degree ya mapenzi nini..haya samehe maana mwenyewe umesababisha mazingira ya kubakwa..tu tena hajakubaka maana ulimfuata mwenyewe..kwenye hizo party zenu..tuliza ball wachana na makesii yatakuja kukudhalilisha zaidi..afu ukome kupewa pewa lift..nunua gari lako au komaa kwenye daladala ndo level zako..next time yatakukuta mazito kuliko haya...
 
Darling nimepata mbinu ya kuwadaka!! Halafu nimeku miss
 
miss u my jambazi..my dia ukiwa na kagari tu unayakamata haya mavichwa panzi unajipigia hataree haina haja hata ya kuwawekea unga..yaache hayafanyi kazi yamezoea tu slope...kutwa kucha yamo humu ndanii kutega mingo teh teh
 
Naona kama hukushauriwa vizuri kuhusu afya yako na mengine hayapo sawa hapa.

Kwanza hamna hospitali hapa Dar yenye uwezo wa kutoa toxicology results ndani ya siku 3.

Pili hakikisha unapima wewe na aliyekubaka magonjwa ya zinaa ikiwemo HIV leo then baada ya miezi mitatu.

Then pima ujauzito leo, then baada ya wiki 2.

Baada ya hapo go for the case, kwani huyo mtu amekuharibia maisha yako. (mahakamani au nje ya mahakama) umfunge au akulipe fidia ya kutosha, don't let this pass kilaini hivyo.

Sasa hivi unaweza kujiona upo okay, lakini kiukweli you are not the same person you used to be.
 
Cha msingi we msamehe tu koz amekiri na imesha tokea potezea an life goes on ili mradi ibaki kati yenu kuwa yasha pita.
 
Mwishoni mwa mwezi December baadhi ya wafanyakazi tulikubaliana weekend moja tukae pamoja kama party get together, tukachagua hotel moja tukaenda, tulikua kama 18 hivi, kila mtu alijigharamia mwenyewe kula na kunywa, kuna mkaka mmoja huwa napanda sana lift yake kwenda kazini karibu kila siku, anaishi Tegeta, hivyo huwa nasimama Bamaga ananipitia hapo, siku ya get together alinipitia pia tukaenda wote.

Kwenye saa nne tukaanza kutawanyika, yule jamaa akadai nisubiri nisiwe na haraka atanifikisha hadi nyumbani, mwisho tukabaki watatu, jamaa yake mwingine, yeye na mimi, muda wote nilikua nakunywa non alcoholic drinks, mimi ni mnywaji wa pombe kwa muda mrefu, wine, savana etc, ila siku hiyo sikutaka kabisa kuonja pombe, jamaa akanibembeleza sana ninywe hata glass moja ya wine inatosha, nikakubali, cha kushangaza akaenda kuifuata yeye mwenyewe kaunta.Baada ya trip tatu hivi nikasikia usingizi mzito sana, nimekuja kushtuka saa saba mchana kesho yake, Tegeta nyumbani kwa yule jamaa, nikiwa na kizungu zungu, sina nguvu, malaria si malaria.

Kibaya zaidi nipo uchi kitandani, nikiwa nimechafuka, nilikua peke yangu, nikajiuliza glass moja ya wine inaweza kunifanya hivi? Nikavuta picha nikagundua kuna kitu nimefanyiwa, yule bwana akaingia na supu kwenye hotpot na kuniomba nioge ninywe supu, nikavaa nguo bila kuoga na nikakodi bajaj hadi nyumbani, sikupata nafuu kabisa, kichwa kilikua kinauma mno, nikalazwa hospital siku tatu ndipo nikapona, yule bwana kwa siku tatu zote alikua na mm hospital, wazazi wanaishi mkoa, mm nimepanga bamaga mwenge, nilikua na PF3 na report ya doctor, ambayo ilionesha wazi nilikua na kiwango kingi cha dawa za kulevya mwilini, na nimeingiliwa

Kuna maelezo mengi sana ila naomba nifupishe.

Kazini hawajui chochote kuhusu hili suala, nilihofia maneno ya watu, maana mimi na yule alienibaka tunafanya kazi pamoja ila yeye ni manager ni bosi, report zote ninazo na mpelelezi wa kesi ana copy pia, nilimuomba mpelelezi asubiri kwanza, kama aendelee au la, sababu ni kuwa, huyu jamaa ameniomba na kunibembeleza sana nisiendelee na kesi hiyo, kwamba nitamuharibia kazi na future yake, kwamba alinipenda siku nyingi na alishindwa tu kuniambia ndio maana alifanya vile, ili kuthibitisha hilo twende wote mkoani akafanye taratibu zote za ndoa tufunge ndoa.

Hata hivyo mimi nina mtu wangu wa miaka 3 sasa, ambae alishapeleka uchumba mwaka jana July, akadai bado anajipanga tumpe muda, yeye haishi Dar huwa anakuja kunitembelea na kuondoka na yeye hajui chochote kuhusu yaliyonipata.

Nipo njia panda nahitaji msaada wenu

Asanteni
Alikupiga dry bibie????
 
Nakuomba uje hapa OFISI za Tanzania Gender Network Program (TGNP) Tuiprocess hiyo kesi haraka haraka iwe fundisho kwa wauwaji kama hiyu bazazi.... Njoo sinza mori halafu ulizia mtu yeyotw ofisi za TGNP zipo wapi..

Au kama unaona aibu nenda kituo cha sheria na haki za binaadamu(LHRC) kipo nyuma ya chuo cha ustaw wa jamii kijitonyama.... Nakwambia hutaombwa hata shiling 1 ila ataisoma namba....

Pia usisahau kwenda tawla
 
Hilo ni kosa la jinai,ilitakiwa umtaje polisi siku ile ile!Hata hivyo makosa ya jinai unaweza fungua siku yyt ukitaka lkn tatizo litakuwa ushahidi!Jamaa huyu usiogope madaraka yake!Mfunge jela
 
Mwenye picha ya "ukipenda chips usiogope mimba" aiweke plse.
CGJz3vOUQAEgfri.jpg:small
 
Yah, nilipata PEP baada ya kipimo cha HIV ndipo nikapewa dawa kwa ajili ya kinga, wakasema napaswa kupima tena mwezi march

Nilikwenda hospital jioni ya siku hiyo hiyo ya tukio maana nilikua najisikia vibaya sana, hospital wakasema ni sababu ya dawa za kulevya hazijaisha mwilini nikapewa drip, siku tatu mbele ndipo nikatoka hospital

Ni ngumu sana kuthibitisha kama ni madawa kama hospitali hawakufanya toxicology tests.

Pili kama hospitali hawakufanya sperms /semen analysis test kwa comparison na za jamaa ushahidi utakuwa mgumu ukizingatia wakati wa tendo ulikuwa umelala.

Mimi nashauri uendelee kumuona hao wataalamu wa ushauri tiba, pili endelea kuchek your health.

Tatu tafuta mwanasheria au nenda TGNP au LHRC upate ushauri wa kitaalamu, what is your chance kesi ikienda mahakamani usije ukapoteza.

Nne mshirikishe huyo mchumba wako, liwalo na liwe.

Huwezi kufanya hayo, jamaa akulipe fidia ya pesa nyingi mmalizane nje ya mahakama and you shut your mouth forever.

Pole sana aiseeeh.
 
Back
Top Bottom