mcmzungu
Member
- Jul 11, 2015
- 48
- 66
Nimeguswa mara nyingi kuzungumzia juu ya viongozi wa makanisa yanapogeuza dini kuwa biashara ya kuleta utajiri kwa kutumia jina la Yesu kwa kufanya usanii tu kudanganya Watu.
Pamoja na Biblia kusema wazi siku hizi za mwisho Watatokea Manabii wa uongo kiukweli Wametokea na Wapo dhahiri.
Binafsi ni muumin wa kawaida Kanisa la ........ Tanzania,mara nyingi Nimesikitika sana na Watumishi wa Mungu ambao Wanapohubiri wanalindwa na mabaunsa wamevaa miwani rangi nyeusi yaani nashangaaga kiukweli.
Utakuta Mtumishi anakemea mapepo na Watu kuanguka majamaa Hayaguswi na huo upako wala mahubiri kuwagusa yaani hamna tofauti na Baunsa anayemlinda Diamond na baunsa anayemlinda Mtumishi wa Bwana,wapo sawa hamna tofauti pia ulinzi wa kulindwa na mabaunsa weengi wa nini anayejua anisaidie kuhusu hili.
Nashangazwa pia na Watumishi ambao kutwa kucha wanahubiri mafanikio tu bila kuhimiza Waumini kufanya kazi maana Biblia yenyewe inasema asiyefanya kazi na asile,bali Wanaombea tu Utapata kazi bila vyeti japo hakuna kinachoshindika mbele za Bwana.
Waimbaji wa kwaya Sitawasahau kiukweli kwa tabia ya Kutuonyesha mbele za Watu utakatifu wakati kiukweli wengine ni wahuni na Tunawajua Wanajificha kwenye kuimba,kuna rafiki yangu mmoja Namjua katembea na wanakwaya wenzie wa kwaya zaidi ya wanne hapo bado mabinti ambao hawaimbi kwaya Nina imani kuna Watu Wanataja jina la Yesu hata Yesu hawajui kabisaaaa.
Kiukweli Tunahitaji kumwabudu Mungu katika roho na Kweli.
Sent using Jamii Forums mobile app