Kanisa la Ufufuo na Uzima la Gwajima, lakanusha kufutiwa usajili, kuwachukulia hatua wazushi

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Kumekuwa na taarifa zinazozunguka katika mitandao ya kijamii tangu mapema asubuhi ya Leo, kuhusu kufutiwa usajili wa kanisa la Glory of Christ Tanzania Church maarufu kama Ufufuo na Uzima. Taarifa hizo *SI ZA KWELI*, zenye lengo la Kupotosha na zipuuzwe na watu wote.

Kanisa kama taasisi hatujapokea barua yoyote ya kuhusu kufutiwa usajili. Ni kosa kisheria kwa mtu kusambaza taarifa zisizo sahihi hivyo, tunawaomba watu wote kuzipuuza taarifa hizo zisizo na tija kwa Ustawi wa Taifa Letu. Pia, toa taarifa kwa vyombo vya sheria iwapo mtu atakutumia uzushi na uongo huo.

David Mgongolwa
Mkurugenzi wa Habari na Mahusiano,
GCTC, Makao Makuu.
12 Julai 2016.
 
Watu wanavimba hadi mishipa ya kichwani kusambaza taarifa mbovu mbovu, asante sana kwa taarifa sahihi.
 
TAARIFA SAHIHI KUHUSU KANISA LA GLORY OF CHRIST TANZANIA CHURCH maarufu kama UFUFUO NA UZIMA

Kumekuwa na taarifa katika zinazozunguka katika mitandao ya kijamii kuhusu kufutwa kwa usajili wa kanisa la Glory of Christ Tanzania Church Maarufu kama Ufufuo na Uzima. Taarifa hizo SI ZA KWELI, zenye lengo la kupotosha na zipuuzwe na watu wote.

Kanisa la Glory of Christ Tanzania Church kama taasisi hatujapokea taarifa yoyote ya kufutiwa usajili. Ni kosa kisheria kusambaza taarifa zisizo sahihi hivyo, tunawaomba watu kupuuza taarifa hizo zisizo na tija kwa ustawi wa taifa letu. Pia, toa taarifa kwa vyombo vya kisheria iwapo mtu atakutumia uzushi na uongo huo.

David Mgongolwa
Mkurugenzi wa Habari na Mahusiano,
GCTC, Makao Makuu.
Asante kwa taarifa mdau davidm
 
Ajira zimesimamishwa, chura hayupo, kucheza pool table mchana ni mwiko, shisha ndo vita mpya.... Kwanin vijana wasikae kitako kupika majungu kwa hali hii?
 
Back
Top Bottom