Civilian Coin
JF-Expert Member
- Dec 2, 2012
- 2,305
- 4,379
KANISA KATOLIKI TANZANIA.
Kanisa kwasasa liko katika mpito mgumu sana na bado halijagundua, ndani ya Kanisa kumechangamana mambo mengi sana yanayokinzana kifikira. Kanisa linaonekana kutaka kuangushwa kiroho na limekosa mtetezi kiroho, baadhi ya viongozi wamefungwa imani zao na hawaoni ndani tena na wamekuwa vipofu wa roho kabisa.
Mambo ambayo Kanisa linapaswa kuyafanya kwasasa:
1. Kufanya mabadiliko ya Kadinari endapo kama hakutakuwa na mbinu mbadala ya kumjenga upya Kiongozi wetu wa kiroho ili kuendana na mazingira mapya ya kiroho. Msiogope, mpaka sasa tuna Mapapa wawili, anayeongoza Kanisa Papa Fransisko na Papa aliyejiuzuru Papa Benedikto. Hata hili la Makadinari laweza fanyiwa kazi kwa muda.
2. Mapadre na Masista wote waliofanya makosa wakasimamishwa waondolewe vifungo vyao nakufanyiwa Recruitment mpya ya kiroho ili waendelee na kazi ya Mungu. Mnapomfunga Padre au Sista mnafunga Kanisa kiimani.
3. Mapadre walioondoka na kuacha Upadre na kuamua kuoa, warudishwe na kuwafanya kuwa Mapadre Walei huku wakiendelea na familia zao, wakitokea makwao.
4. Mashemasi wote waliokatizwa nakuamua kuoa, wapadrishwe na kuwa Mapadre walei.
5. Mafrateri waliofukuzwa kabla ya Ushemasi warudishwe na kutendewa haki zao
6. Watawa ambao wameanzisha familia wapewe vyeo vya kikanisa ili kulijenga upya kanisa
7.Wote waliowahi kupita seminaries wapewe nafasi ya kuhudumu shule za kanisa maana tayari ni hadhina ya Kanisa.
Nina mengi lakini sio lazima yafanyiwe kazi yote. Nawatakia mfungo Mtakatifu wa Kwarezima.
Ndimi kijana wenu;
Deogratius Nalimi Kisandu
MKOMBOZI WENU.
Mwanza, Tanzania.