KANISA KATOLIKI halitamualika E. Lowasa - ASKOFU NZIGILWA

mizambwa

JF-Expert Member
Oct 8, 2008
4,422
1,790
Askofu Msaidizi wa Jimbo kuu la DSm (Askofu Nzigilwa) amesema kuwa "Kanisa Katoliki halijamualikwa Mh. E. Lowasa katika Harambee ya kuchangisha pesa kwa ajili ya sherehe za Uzinduzi wa Jimbo Katoliki la Ifakara kama ilivyoripotiwa hapo awali.

Askofu Nzigilwa aliyasema hayo alipokuwa akijibu shwali toka kwa mmoja wa viongozi wa Parokia walioshiriki katika kikao cha pamoja cha Tathimini ya Mavuno 2011, Msimbazi Centre DSM.

MY TAKE: TUNASHUKURU SANA KANISA KATOLIKI KWA KULIONA HILI na viongozi wa kanisa Katoliki kwa kupitia mada zetu hapa JF. Hongera pia kwa kiongozi aliyeuliza hilo swali kuhusu mwaliko wa Mh. E. L kanisani kwa moyo wako wa ushujaa.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
It was historical mistake to RC Church of Tanzania! Maneno ya askofu wa Mwanza yamelipaka mapote kanisa! Bora aende kama muamini wa kawaida tu na sio kutoa hotuba za kisiasa kwenye madhabahu!
 
Naliaminia Kanisa Katoliki!
Waumini wa RC wanajulikana kwa utoaji, na Mungu amewajalia kipato, na wanaweza kuchanga pesa yoyote ile bila uwepo wa fisadi!
Mbona ni kanisa hilo hilo katoliki ndio lilituambia Kikwete ni chaguo la mungu! je wameshawahi kuwaomba radhi Watanzania kwa mateso wanayoyapata kutoka kwa chaguo la mungu?
 
Kwasasa TUNAONGELEA kupokea michango ya Lowassa!
 
Askofu Msaidizi wa Jimbo kuu la DSm (Askofu Nzigilwa) amesema kuwa "Kanisa Katoliki halijamualikwa Mh. E. Lowasa katika Harambee ya kuchangisha pesa kwa ajili ya sherehe za Uzinduzi wa Jimbo Katoliki la Ifakara kama ilivyoripotiwa hapo awali.

Askofu Nzigilwa aliyasema hayo alipokuwa akijibu shwali toka kwa mmoja wa viongozi wa Parokia walioshiriki katika kikao cha pamoja cha Tathimini ya Mavuno 2011, Msimbazi Centre DSM.

MY TAKE: TUNASHUKURU SANA KANISA KATOLIKI KWA KULIONA HILI na viongozi wa kanisa Katoliki kwa kupitia mada zetu hapa JF. Hongera pia kwa kiongozi aliyeuliza hilo swali kuhusu mwaliko wa Mh. E. L kanisani kwa moyo wako wa ushujaa.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!

Ni kwa sababu gani hawamwaliki? Kwa vile ni mgonjwa au yeye mwenyewe (EL) ametoa udhuru wa kutohudhuria tokana na ushari wa daktari kupungunza muda wa kazi kwa mapumziko? Je ni kwa vile wamegundua pesa anazotoa ni zile pesa chafu?
 
Mbona ni kanisa hilo hilo katoliki ndio lilituambia Kikwete ni chaguo la mungu! je wameshawahi kuwaomba radhi Watanzania kwa mateso wanayoyapata kutoka kwa chaguo la mungu?

Ieleweke kuwa kutenda kosa siyo kosa bali kurudia kosa.......

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Ni kwa sababu gani hawamwaliki? Kwa vile ni mgonjwa au yeye mwenyewe (EL) ametoa udhuru wa kutohudhuria tokana na ushari wa daktari kupungunza muda wa kazi kwa mapumziko? Je ni kwa vile wamegundua pesa anazotoa ni zile pesa chafu?

Hii ni kuonyesha kuwa JF, mada zake zinasomwa na watu wengi. Hivyo wengi wanautmia jamvi hili kupata habari mbalimbali. Huyo aliyeuliza swali bila shaka ni member hapa au alipita hapa na kukuta ile THREAD tuliyojadili kwa muda mrefu mwezi Feb. 2012 hapa JF.

HONGERA JF kwa mada nzuri za kukosoa jamii na kujenga maadili mazuri.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Ni kwa sababu gani hawamwaliki? Kwa vile ni mgonjwa au yeye mwenyewe (EL) ametoa udhuru wa kutohudhuria tokana na ushari wa daktari kupungunza muda wa kazi kwa mapumziko? Je ni kwa vile wamegundua pesa anazotoa ni zile pesa chafu?

Alichokifanya Askofu ni kukataa kuwa hawawezi kumualika kiongozi wa Kisiasa katika shughuli kama hiyo ya Kikanisa kwani italeta kutokuelewana.

My Take: Wamefanya vizuri kwani inaeleweka nyumba za Ibada hakuna itikadi za kisiasa. Waumini ndio wana itikadi za kisiasa. Hvyo pale Kanisani kuna Wanachama wa vyama tofauti vya Siasa. Kweli italeta mtafaruku katika kanisa mfano; Mimi ni Mkatoliki lakini sikubaliani na hili kabisa. nafurahi viongozi wa kanisa Katoliki wamesikiliza maoni yetu. Isipokuwa napenda pia kutoa angalizo kuwa isiwe amejibu hivyo kisha kesho akakanusha maneno yake ikatuletea mchezo wa kauli za Waziri Mkuu PINDA kuhusu mgomo wa Madakitari.

Ni kama nilivyochangia katika ile THREAD iliyotangulia kuhusu tukio hili.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Askofu amesema HALIJAMUALIKA, wewe kwenye title umeandika HALITAMUALIKA !!! Ni vitu viwili tofauti. Inawezekana halijamualika lakini akahudhuria na asifukuzwe! Inawezekana pia halijamualika (kwa hadi sasa) lakini litamualika (hapo baadae harambee itakapokaribia). Narudia tena, HALIJAMUALIKA is not necessarily HALITAMUALIKA
 
Ni Vyema ukirudi Darasani ukasome tena Kiswahili.

Pia katafute Gazeti Tumaini Letu, au Piga Simu Radio Tumaini watakuwa na habari kamili.

Askofu amekataa kuwa hawawezi katika shughuli kama hii kumpa mwaliko kongozi yeyote wa Kisiasa. NDIVYO ALIVYOSEMA KAMA KUNA MENGINE MIMI SIJUI.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Mbona ni kanisa hilo hilo katoliki ndio lilituambia Kikwete ni chaguo la mungu! je wameshawahi kuwaomba radhi Watanzania kwa mateso wanayoyapata kutoka kwa chaguo la mungu?

Alieyasema hayo tayari amechukuliwa hatua za kikanisa na ulikuwa msimamao wake bianafsi na si kauli rasmi ya akanisa.......au ushawahi kumsikia au kumuona Dari Salama(Safe Roof)?
 
Back
Top Bottom