Muulize ana maana gani maana hata mimi amenishangaza.
Rafiki yangu kaniomba nimsindikize benki achukue pesa akanunue kiwanja kaenda kaunta kachukua pesa kanituma nikamnunulie maji akidai ananisubiri hapo ndani ya benki kwani kuna receipt anaingojea.
Narudi simkuti nampigia cm hapokei, baada kama ya robo saa ananipigia cm eti alishaondoka nimfuate huko anakonunua kiwanja.
Hapa nikaanza jiuliza huyu kaomba lift yangu huko tena kaenda nanani?
Na kwanini anitoroke?
Jamani wana JF huyu anamaana gani?
amekuona huna shughuli za maana ndio maana kakuacha kwenye mataa
Madai yake eti aliona milion 8 ni nyingi akaita escort ya police. eti alipewa ushauri na accountant wa benki.:smile-big:???
ha ha ha ha! Nacheka kama mazuri. Msamehe tu mpenzi. Si unajua tena binadamu tulivyo.