Ndugu zangu wanajamvi habari za asubuhi.
Nimekuja hapa kuandika uzi huu.. nikiomba ushauri.. nikihitaji faraja kutoka kwenu.
Mim ni kijana miaka 25 , mwenzangu huyu 21. nimemaliza chuo miaka miwili iliyopita.. mwenzangu kaishia form 4.
Tumekuwa kwenye mahusiano karibu mwaka na nusu. Niseme kweli nilimpenda sana na yeye alinipenda. Nilijitolea sana kwa hali na mali kwa moyo wote kumsaidia katika maisha yake... nilimpenda kwa moyo wote. Hali ilibadilika miez kadhaa tangu tuingie kwenye mahusiano...
Mwenzangu akabadilika gafla.. kaanza kunifanyia vituko.. majibu machafu.. nikimkosea tena kosa dogo laki binadamu ,mwenzangu anachukulia nimefanya makusudi.. anakuwa mkali ugomvi hauishi wiki nzima. Sms akawa hajibu.. hata calls zangu hapokei..
Nikachunguza... mabadiliko haya.. nikagundua mitandao ya kijamii ndio imemponza ..
Nikasema ngoja nipunguze mapenz. Akajirudi akawa mpole.. akawa anasema ananipenda. Nikarudisha tena mapenz tena kwake... baada ya muda akarudia ile tabia... majibu machafu.. kiburi cha wazi wazi..
Nikaenda kwa mama yake ... akasema nimvumilie.. kwa kuwa bado hajakuwa kiakili... nikavumilia ..nikampa onyo... akajirekebisha wiki mbili tu.. baada ya hapo karudia tena tabia ile ile ya kuto nisikiliza.. anataka asikilizwe yeye tu.. nikimshauri jambo anajifanya mjuaji sana..
Kiburi nje nje...
mimi sikuwah msaliti.. na despite ya vituko anavyo nifanyia..nilizidi kumwonyesha upendo, mimi nilimlipa kwa mema.. sijawah kulipiza kisasi.. kwake. Mpaka ndugu zake walikuwa wakisifia upendo wangu kwake. Lakin mwenzangu alikuwa haoni hilo.
Kila tulipo kosana... alitaka tuachane ... hata kama kosa ni dogo.. anataka tuachane..
Nikikubali anakaa week 1 moja .. anaomba msamaha.. na kuahid kubadilika.. lakin baada ya hapo tena anarudi madudu.
Jana usiku nilimpigia simu kumsalimia .. kumjulia hali.. akakata simu.. nikamtumia sms hajajibu. Nilipo mpigia mara ya pili akapokea.. nikamuuliza kwann anafanya hivyo.. akasema hajisikii kuwa na mm... nikamuuliza kwa nn, ni kosa gani nimekutenda.. akasema hakuna ila hajisikii tu.. na ananitakia maisha mema na masiano yaishe.
Sasa wadau.. sijamtenda baya lolote .. lakin yeye kaamua hiv.. nifanyaje.. naomben ushauri?