Kangi Lugola umekosea sana kumfukuza Kamishna Jenerali Juma Malewa Mkutanoni mbele ya kadamnasi

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,895
KAMISHNA JENERALI JUMA MALEWA ,STAHIMILI

Na Happiness Katabazi

LEO Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amemtimua kikaoni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Dk.Juma Malewa kwa kile alichodai amechelewa kufika katika mkutano wake na waandishi wa habari.

Kitendo hicho ambacho si cha kiungwana kilichofanywa na Waziri Lugola dhidi ya Kamishna Jenerali Dk.Malewa kimewasikitisha watu nikiwemo mimi.

Waziri Lugola amemtimua Kamishna Malewa huku akiwa anarekodiwa na vyombo vya habari.

Lugola ambaye Julai Mosi mwaka huu,aliteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani amesikika na kuoneka katika video akimtimua Kamishna Jenerali Malewa atoke ukumbini kwasababu amechelewa na hakutaka kumsamehe wala kumsikiliza Dk.Malewa kwani Lugola alikuwa akisikika akisema askari wamefundishwa nidhamu ,aliagiza mlango ufungwe na akashangaa nani kafungua mlango akaingia.

Lugola huyu ambaye aliwahi kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa makosa ya kuomba rushwa lakini baadae Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) ,Biswalo Mganga alitumia kifungu cha 91 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai akamfutia kesi hiyo.

Siyo hali ya kawaida kiongozi wa kijeshi kuchelewa kufika eneo la tukio kama baadhi walivyo viongozi wa kisiasa.

Kiongozi mwenye busara na anayefikiria sawa sawa kabla ya kufikia uamuzi wa kumtimua tena mkuu wa Jeshi la Magereza Malewa tena mbele ya waandishi wa habari ama angemuacha Malewa aingie mkutano uishe amuite ofisini amwadhibu kiofisi bila hata watu wengine kujua au amuulize nikwanini amechelewa ili wakati anamuuliza TV zimmulike vizuri aonekane ni mchapakazi sanaa maana chakula cha Wanasiasa ni vyombo vya habari.

Hilo mwenzetu huyu Lugola ambaye amekuja moto wizara ya mambo ya ndani lakini ni lazima atapoa tu kwani hii ndio Tanzania kaishia kumfokea mwanaume mwenzie Malewa dunia kupitia vyombo vya habari tumeshuhudia akimfokea tena kwa kumtaka atoke nje na kwamba askari wamefundishwa nidhamu hamtaki katika mkutano wake na afande Malewa kwa unyenyekevu huku akimulikwa na TV akaondoka.

Hivi wewe Waziri Lugola ulivyosema askari wamefundishwa nidhamu wakati ukimtimua Mkuu huyo wa Jeshi la Magereza Dr.Malewa ndio unamaanisha huyu Inspkta Jenerali Malewa ambaye ni mkuu wa Jeshi la Magereza hana nidhamu?

We Waziri Lugola hivi ikitokea Malewa akija kuulizwa na aliyemteua au mamlaka zingine ni kwanini alichelewa Malewa akatoa sababu ambazo ni Za msingi kabisa utaitisha tena mkutano wa vyombo vya habari kumsafisha?

Kwanini Lugola kama nia yako ni safi kabisa kwa Malewa ukuona haja yakumvumilia aingie mkutano mmalize umuite ofisini umwadhibu kama unayomadaraka ya kumwadhibu?

Kwanini umeona fahari sana kumdhalilisha hivyo na kiongozi mkubwa wa jeshi letu mbele ya uso wa dunia leo umemuhukumu bila kumpa nafasi ya kujieleza kuwa nimchelewaji na kumtimua kama mtoto mdogo mbele ya vyombo vya habari vikimulika?

Lugola hivi huu ujasiri wa kumtimua kama kibaka Inspekta Jenerali Jeshi la Magereza ambaye ni mteule wa rais kama wewe umeupata wapi? Umetumwa?

Mtu mwenye cheo cha Inspekta Jenerali wa Jeshi ana wasaidizi,walinzi,washauri,msafara wake na pia ndio mtoa maamuzi wa jeshi la Magereza ktk mambo mbalimbali hivi kabla ya kumtimua kama kibaka kiongozi huyo kwanini ukutaka kujipa muda kwanza kutafakari nini amechelewa?Badala yake ukamtimua kama mvamiaji ?

Lugola ulivyokuwa polisi hukuwahi kufikia kufikia cheo cha Inspekta Jenerali kama alichonacho Dk.Malewa basi leo kabla ya kufikia hatua ya kumtimua Inspekta Jenerali Malewa kwa dharau vile ukutafakari basi kidogo kuwa licha wewe hivi sasa ni waziri lakini yule Malewa amekuzidi cheo katika jeshi uone haja basi ya kumpa heshima yake ?

Kwa kitendo hiki ulichomfanyia Mkuu huyo wa Magereza ,hivi wale wanaongozwa na kamanda huyo wanamuonaje hivi sasa au wanakuchukuliaje wewe hivi sasa kwa kitendo hicho ambacho mimi nasema sicha kiungwana kwa afande wao Malewa ?

Au wale mahabusu / wafungwa waliopo gerezani ambapo magereza yote yapo chini ya Jeshi la Magereza ambalo jeshi la Magereza linaongozwa na Inspekta Jenerali Malewa?

Kamanda Malewa nyamaza kaa kimya ila akili kumkichwa Muachie Mungu atakulipia hilo uamini kabisa kwanini namimi nilishakutwa na tukio kama hilo chuoni nilichelewa dakika tano kuingia darasani asubuhi nanilichelewa kwasababu nilitokea hospitali nilikokuwa nimelazwa na mtoto ,nikamwacha mtoto wodini na ndugu yangu amtazame minikawahi chuoni nikitokea wodini huku nikiwa nina uchovu ile nafungua mlango naingia class huyo mwalimu alishika kipaza sauti akanitimua kama alivyokutimua huyo Bwana Lugola kama takataka fulani vile nilimwomba msamaha nakuomba nijieleze alikataaa kunisikiliza nikatoka nikarudi wodini kumuuguza mwanangu Queen nanilimshitakia Mungu amtie adabu huyo mwalimu kwa muda wake na kweli aikuzidi miezi sita mwalimu huyo alikumbwa na skendo mbaya ya fedhea na akatimuliwa kazi kwa fedhea.

Mungu atakulipia madamu aukuwa na dhamira ya kuchelewa katika hicho kikao .

Mtu yoyote mstaarabu na muungwana hatujafurahishwa na hiki kitendo ulichomtendea kiongozi huyu wa Jeshi la Magereza Malewa ambaye kwanza hajawahi kusikika katika jamii kuwa anatuhuma za uhalifu kama tuhuma kupokea au kuomba rushwa kama wewe kwani wewe Lugola Ukiwa mbunge ulishafunguliwaga kesi ya rushwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kesi yake baadae DPP alikuja kuifuta.

Kuna baadhi ya waliowahi kuwa Mawaziri wa Wizara hiyo ya Mambo ya ndani walivyoingia katika hiyo wizara wakajifanya wajuaji kutwa kutaka askari fulani akamatwe mtovu wa maadili,kuagiza askari polisi fulani wasimamishwe kazi,wachunguzwe.

Na nilikuwa nawaonya nikikutana nao chemba waachane na mambo ya kusikiliza umbea wa mitaani kutoka wapiga kura wao na wapambe wao kwani mwisho wa siku jeshi litabaki kuwa jeshi na wao ni mawaziri tu ni watu wa kupita katika hiyo wizara hawakunisikia mwisho wa siku wale askari waliokuwa ameagiza wachunguzwe wakaonekana na vyombo vya polisi wapo safi, na hao mawaziri enzi za utawala wa Rais Kikwete nao Kikwete alikuja kuwaondoa kwa sababu anazozijua yeye na wengine na uwaziri hivi sasa wanausikia redioni.

Lugola na Malewa wote ni viongozi wa Taifa letu mnaitaji kuheshimiana na sisi tuwaheshimu kama mnamdhaifu yenu malizaneni ndani lakini siyo kwa stahili hii ya leo ya waziri Lugola kumtimua kiongozi huyo wa Jeshi la Magereza kwa mtindo ule ambao auleti picha nzuri kwetu.

Ni itimishe kwa kumwambia Waziri Lugola katika hayo madaraka yako mapya ya Waziri wa Mambo ya Ndani nenda taratibu,hekima na busara vikuongoze.

Acha pupa kwani Mwenye Pupa hali tamu.

Mungu ibariki Tanzania.

Mwandishi wa makala hii ni Mwandishi wa Habari Mwandamizi nchini na Mwanasheria.

FACE BOOK: Happy Katabazi

6/7/2018


My Take:

tar.26.05.2017 katika mahakama ya ardhi mjini Musoma "The district land and housing Tribunal Musoma " mbunge wa Mwibara alipata tabu sana na wakati mgumu kujibu tuhuma zake za kupora ardhi ya mjane kinyume cha sheria. Kangi Lugola aburuzwa mahakamani leo, kesi yaahirishwa tena hadi 29/06/2017

Siku ile Wabunge waliopandishwa Mahakama ya Kisutu ni Victor Mwambalaswa, Sadiq Murad na Kangi Lugola Mbunge wa Mwibara.

Wabunge hao waliopandishwa Kisutu, wanatuhumiwa kumuomba Mkurugenzi wa Halmashauri ya Gairo rushwa ya Shilingi Milioni 30.

Wabunge hao wanakamilisha taratibu za dhamana kila mmoja kulipa Millioni 5 na kesi kusikilizwa April 15.

TUHUMA ZA RUSHWA BUNGENI: Wabunge watatu waburuzwa mahakamani

Ila leo kawa msafi kiasi cha kumfukuza mtu kwa kuchelewa dakika moja bila kujali miundombinu yetu.

Tukipewa kichwa tusile na masikio.

Yote hayo mbona tumemvumilia? Kiongozi hutakiwi hata kutuhumiwa.
 
Wakuu,

Ni kwamba, Ndg. Malewa alifika mapema sana tu na akakaa ktk ukumbi mwingine wa mikutano kabla ya huyo Lugola kufika kumbe ukumbi ulikuwa umebadilishwa bila kutaarifiwa akaja kutaarifiwa baadae kuwa ukumbi umebadilishwa ndio akaenda ukumbi mwingine na kukutana na fedheha hii ya kudhalilishwa na mwanasiasa.

Hivi vyeo vya kisiasa vinawagharimu watendaji wengi serikalini!
 
unatetea ujinga kabisa kuhusu huyo bosi kutimuliwa kikaoni.....na hiyo ndiyo shida ya sisi waafrica kutetea ujinga tu Lugola amefanya inavyotakiwa na hiyo namna ilivyo dunia kwa waliendelea ...nidhamu kwanza....tumefanya mashirika ya kimataifa tumeyaona hayo ya kufuata muda ktk vikao
 
unatetea ujinga kabisa kuhusu huyo bosi kutimuliwa kikaoni.....na hiyo ndiyo shida ya sisi waafrica kutetea ujinga tu Lugola amefanya inavyotakiwa na hiyo namna ilivyo dunia kwa waliendelea ...nidhamu kwanza....tumefanya mashirika ya kimataifa tumeyaona hayo ya kufuata muda ktk vikao
Huyo Lugola angekuwa na nidhamu asingeingia kwenye kashfa ya kuomba rushwa
 
Lugola hajui hawa makamanda (wa polisi na JWTZ) kuwa huwa wanaongea lugha moja.

akiendelea kuwa treat rudely hivi, basi yeye na anayemtuma wakae mkao wa kupigishwa lapa fasta!
Jeshini ni amri moja tu go out go out hakuna mjadala hapo huyo kamishini akajipange upya namna ya kufanya kazi kijeshi
 
Kwa Kweli Nimesikitika Sana Kwa Huyo Malewa Kufukuzwa Kama Mbwa Koko Tena Mbele Ya Vyombo Vya Habari Bila Kusikilizwa Sababu Imempelekea Afanye Hivyo.

In Short, Huo Ni Udikekta Mkubwa Sana, Pia Sio Utaratibu Mzuri Uliotumika.

Let Law Of Karma Do It's Work
 
Kwa Kweli Nimesikitika Sana Kwa Huyo Malewa Kufukuzwa Kama Mbwa Koko Tena Mbele Ya Vyombo Vya Habari Bila Kusikilizwa Sababu Imempelekea Afanye Hivyo. In Short, Huo Ni Udikekta Mkubwa Sana, Pia Sio Utaratibu Mzuri Uliotumika.

Let Law Of Karma Do It's Work
ile amri ya kijeshi haipingwi.........acha kutetea ujinga hapa....unapiga salute na kuondoka
 
Back
Top Bottom