Kangi Lugola kuchukiwa na askari, ukweli wawekwa hadharani. Huenda wanyonge wakakumbuka utawala wake

Elitwege

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
5,154
10,809
Nenda Lugola nenda Lugola, sisi wanyonge tunakulilia.

Siku zote nabii hakubaliki kwao na ukitaka kuchukiwa sana basi simamia haki, Lugola alikuwa ni moja ya mawaziri makini waliosimamia haki Wizara ya Mambo ya Ndani.

Siri ya Lugola kuchukiwa na askari hadi kufikia hatua ya kushangilia alipotumbuliwa hizi hapa.

1. Kangi Lugola alikuwa waziri wa kwanza wa mambo ya ndani kufyeka kichaka cha rushwa kwenye magari ,ikumbukwe kabla ya Lugola kila kosa kwenye gari lilikuwa linatozwa shs 30,000!

Yaani gari haina indicator elfu 30
Gari halina rangi elfu 30

Tairi imeenda upande elfu 30

Yaani trafiki alikuwa na uwezo wa kukusome makosa 10x30,000 =300,000 hiyo anaondoka nayo asubuhi asubuhi tu!
Lugola aliamuru makosa yote hayo yako chini ya kosa moja tu la ubovu wa gari na mwenye gari anatakiwa alipe elfu 30 tu badala ya laki 3! Kwa hali hii askari wala rushwa (Chadema) watampenda Lugola?

2. Kabla ya Lugola ilikuwa ukiwekwa mahabusu weekend hutoki kwa sababu hamna dhamana, lakini waziri huyu shujaa alikuja kuamuru dhamana zitolewe hadi siku ya Jumapili!

Je kwa hali hii Polisi watapenda?

3. Ni Waziri shujaa Kangi Lugola aliamuru bodaboda zote ziondolewe kwenye vituo vya Polisi. Kumbukeni bodaboda zilikuwa zinarudikwa kwenye vituo vya polisi hadi kituo chenyewe kinakuwa hakionekani. Lengo la kitendo hiki ni kutengeneza mazingira ya rushwa na ufisadi ili askari wapige dili.

Kwa hali hii wanyonge watamchukia Lugola?

4. Kabla ya Lugola mabasi ilikuwa ni marufuku kuendelea na safari baada ya saa sita usiku. Hali hii ilileta usumbufu na gharama kubwa kwa abiria na kwenda kinyume na Sera ya viwanda na uchumi wa kati.

Lugola alifyeka kichaka hiki kwa kuwaambia askari wakae sawa magari yatembee usiku kucha na wananchi hawawezi kupangiwa muda wa kusafiri na majambazi.

Kwa hili wanyonge watamchukia Lugola?

5. Chini ya Waziri Lugola matukio ya utekaji, mauaji na ujambazi yalipungua sana nchini. Wote ni mashahidi wa hili muda wote mabasi yamesafiri usiku kucha hamna basi hata moja lililotekwa.

Kwa hili wanyonge watamchukia Lugola?

Nenda Lugola ila huenda kilichokuponza pia ni kuwa upande wa maslahi ya wananchi sana na kupuuza kulea rushwa za maaskari tulizozizoea tangu uhuru, lakini wahenga walisema tenda wema uende zako usingoje shukrani ila uwe na hakika Lugola siku ya kiama utavishwa taji na wanyonge.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh askari wala rushwa kumbe ni chadema tena?

Ohoo yamekuwa hayo tena

Sent using Jamii Forums mobile app
Na Rais kamchukia huku akisema IGP alikuwa amamlalamikia Lugola kila siku. Sikujua huyu Rais na IGP ni Chadema na wapiga dili wakubwa kiasi cha kumchukia Lugola.
Mleta mada huku sio kufikiri bali kuharisha, Polepole njoo uone taka taka zako huku!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unyonge maana yake ni udhaifu na katika huu muktadha unyonge limetumika kama mtu fukara ,nadhani hatupaswi kulifurahia hili neno, maana maneno huumba kataa unyonge unyonge ni ufala

NB yote uliyoyaandika kuhusu ninja Lugola ni ukweli mtupu alikua upande wa raia sana na aliwanyoosha vijana wake vyakutosha tatizo hatujui huyu aliekuja hizo buti zitamtosha au ataungana na mabibiloni kudhulumu raia haki zao
 
Kweli kabisa

Mnyonge siyo mtu fukara bali ni mtu ASIYEJITAMBUA.

Kwa mfano Chadema ni chama cha matajiri kwa mujibu wa katiba yao lakini wasiojitambua......kwahiyo wale ni WANYONGE tu!
 
Back
Top Bottom