nuruyamnyonge
JF-Expert Member
- Mar 18, 2014
- 4,390
- 2,162
Amani iwe kwenu.
Mbunge wa jimbo la Mwibara; mh. Kangi Lugola, anatakiwa kufika mahakama ya ardhi mjini musoma kujibu tuhuma zinazomkabili. The district land and housing tribunal Musoma.
Mh.Mbunge anakabiliwa na tuhuma za kupora ardhi kinyume cha sheria akitumia rushwa kuwahonga viongozi wa kijiji kwa masilahi binafsi.
Mnyetishaji wangu amenitonya kwamba, mh.mbunge alipelekewa "summons /notice" yaani wito wa kuitwa shaurini tar.21.03.2016 lakini aligoma hakufika mahakamani.
Mahakama imeamuru tena apelekewe wito 'summons' tar. 11.04.2016 saa 08:00 Am afike bila kukosa. Walalamikaji wanadai mbunge hakai ofisini wala katibu wake hivyo popote alipo ajitokeze apokee summons yake.
Hata hivyo, nasikitika sana kuona ukimya wa mkuu wa wilaya ya Bunda, kutokuchukua hatua yoyote juu ya mgogoro huu tangu mwaka 2005 mpaka leo 2016.
Vyombo vya habari vipo kimya! Itv mko wapi siku hizi? Redio one hampo kanda ya ziwa? Mtafuteni huyu kada wa ccm atawapa stori ya huu mgogoro wa ardhi.
Eneo lenye mgogoro lipo jirani na hospitali ya Kibara kijiji cha Namibu.
Tarehe 11.04.2016 inangojewa kwa hamu kubwa sana pale kwenye viwanja vya mahakama ya ardhi Musoma. Je! Atajitokeza au atakula kona? Ufisadi kitu kibaya sana.
Majipu yatumbuliwe hakuna namna!