Kangi Lugola: CCM wanaweweseka

Kangi Lugola: CCM wanaweweseka

Kicheba One

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2014
Posts
399
Reaction score
194
Katika magazeti ya leo,mbunge tajwa hapo amenukuliwa akisema kuwa CCM wana hofu kwakuwa wabunge wake 25 hawaingii bungeni.


====

Lugola: Kukubali serikali tatu ni kukwepa unafiki

Kwa ufupi
Asema Rasimu ya Tume ya Warioba ni maoni ya Watanzania, hivyo kumpinga ni kumkosea heshima
By Habel Chidawali,Mwananchi
Dodoma. Mjumbe wa Bunge la Katiba Kangi Lugola, ametaja msimamo wake wa kuunga mkono serikali tatu kwamba ni kukwepa unafiki.

Lugola, ambaye alisema kwenye kikao cha Bunge la Katiba kuwa atakuwa wa mwisho kuisaliti Rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, alisema kinachowasumbua wanasiasa wengi ni suala la unafiki ambalo ameapa hatakuwa tayari kulisujudia.

Akizungumza na gazeti hili kuhusu msimamo wake unaopingana na chama chake cha CCM, alisema wanaounga mkono miongozo ya vyama kwenye Bunge la Katiba, wanafanya hivyo kwa unafiki na hofu ya kisiasa.

Alisema kitendo cha kupinga Rasimu ya Pili ya Katiba ambayo iliwasilishwa na mwenyekiti wa Tume, Jaji Joseph Warioba, ni sawa na kupinga mawazo ya wananchi.

“Tumetumia fedha nyingi kwa ajili ya Tume ya Jaji Warioba kukusanya maoni ya wananchi na alichokileta bungeni ni matakwa ya Watanzania. Leo hii tunaanza kuchakachua kile ambacho alikifanyia kazi kwa uaminifu mkubwa?” alihoji Lugola.

Alisema hawezi kukubaliana na dhambi ya unafiki. “Nawataka wana-CCM wenzangu muweze kupima mambo badala ya kuburutwa,” alisema.

Kuhusu muundo wa Muungano, alisema hata sasa hakuna Muungano kwani Zanzibar imeshajitangazia mamlaka yake.

“Kama wanataka kurudisha Muungano, Serikali ya Zanzibar inatakiwa ivunjwe ili ieleweke kuwa hakuna Tanganyika na hakuna Zanzibar. Sasa hakuna lolote ambalo linaweza kunishawishi kuwa kuna Muungano,” alisema Lugola.

“Muundo wa be huyo alisema kuwa serikali tatu unawezekana na tayari upo unafanya kazi, lakini ukiwa katika kivuli cha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” alisema ambaye wiki iliyopita aliwatahadharisha wajumbe wenzake dhidi ya hatari kwa wengi kuwaburuza wachache.
 
Tatizo lake huwa anakurupuka angekuwa anajenga hojaangefaa sana,anakurukupa ili kupata sapoti ya watu ipo siku watamtelekeza.
 
Weka Nyama kwenye hoja, mfano hoja ya katiba haimo kwenye ilani ya maccm. Kwa kifupi kifupi wamedandia hoja ambayo si yao. Kweli CHADEMA wana sera nzuri ambazo walozibeza wanazifuata na kuziiga. CHADEMA ndo mkombozi wa watanganyika wote tuipe support sana ili Tanganyika iwe huru siku 1. Rab ibarii CHADEMA, TANGANYIKA NA WANANCHI WAKE. AMINA.
 
Hawakwenda kwa vile wanapinga kinachoendelea bali wako kwenye shughuli zao sasa CCM wanakuwa na kiwewe kuwa akidi haitatimia

OK,kama ndio hivyo basi Lugola pamoja na mapungufu yake yupo sahii,ujue pia wananchi siku hizi wanaangalia Mbunge wao anafanya nini pale bungeni,hata ccm wakimfukuza uwanachama atapata ubunge kupitia chama chochote kile.hii ndio demokrasia halisi.
 
Kangi Lugola ni kubwa jinga anaependa media attention

Nakumbuka mama mingoi aliyekuwa anatikisa mt.a.k.o nch nzima ndio wewe siyo? Umeacha hako katabia ka kizaramo na kikwere?
Naona ccm mnatupiana mawe wenyewe kwa wenyewe!!! Unabii huuuuoooo unachanja mbuga kutimia na hakuna wa kuuzia!!!
 
Huyu mdogo wangu simwamini kabisa hasa baada ya kugeuka wananchi kwenye bajeti ya nishati na madini. Tangu hapo simwamini kabisa.
 
katibu wao Mhagama alisema wapo 25 na anawatafutia dawa

Ujue Double Chris,huyo Mhagama amechemka kwa kipindi hiki kilichobaki kabla ya uchaguzi 2015,ni kifupi sana hivyo mbunge huwezi kumtisha.
 
OK,kama ndio hivyo basi Lugola pamoja na mapungufu yake yupo sahii,ujue pia wananchi siku hizi wanaangalia Mbunge wao anafanya nini pale bungeni,hata ccm wakimfukuza uwanachama atapata ubunge kupitia chama chochote kile.hii ndio demokrasia halisi.

Kama ni hivyo basi Sugu haitaji kampeni Mbeya mjini kwa kuwa amevunja rekodi ya kipimbi bungeni.Wananchi wanahitaji kushughulikiwa kero zao zinazowakabili katika maisha yao ya kila siku kama elimu,maji na barabara sio mbunge kugeuka kuwa msema hovyo
 
Nakumbuka mama mingoi aliyekuwa anatikisa mt.a.k.o nch nzima ndio wewe siyo? Umeacha hako katabia ka kizaramo na kikwere?
Naona ccm mnatupiana mawe wenyewe kwa wenyewe!!! Unabii huuuuoooo unachanja mbuga kutimia na hakuna wa kuuzia!!!
Samadi inakuwasha
 
Back
Top Bottom