Kangi Alphaxard Lugola: A new Sheriff in Town

Kangi Alphaxard Lugola: A new Sheriff in Town

Mimi nina hamu ya kupata Majibu kuhusu Mbwa wa Bandarini Jibui Lisiwe Kinyemela tunahitaji Kelele Zilezile kwa Majibu yenye Mashiko
 
Kwa namna Rais Dk. John Pombe Magufuli alivyoiendesha Serikali yake akisaidiwa na PM katika miezi yake miwili tangu aapishwe tarehe 5.11.2015, ilikuwa ni wazi kuwa mmojawapo ya Wabunge ambao wasingekosekana katika Baraza lake la Mawaziri alilotangaza Disemba 10, 2015, ni Kangi Lugola.

Hata hivyo, bahati haikuwa yake akaachwa benchi. Hata alipoteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Muungano na Mazingira, haku-deliver kufanya mtu ku-notice.

Mambo yamebadilika kabisa baada ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani. Though maamuzi yake mengi yamekuwa controversial, still ameleta vionjo vipya kwenye utendaji kazi ambavyo haviko kwa Viongozi wengine. Amemfunika 'another' Sheriff in Town - Paul Makonda, ambaye kwa miaka miwili ameiteka media kwa kiwango kikubwa.

Baadhi ya Maagizo ambayo yameleta mijadala mikubwa nchini ni:
  • Jeshi la Polisi kushughulikia zuio la Mabasi ya abiria kusafiri usiku.
  • Jeshi la Polisi kutafuta Mbwa wa Kikosi cha Farasi na Mbwa aliyepotea.
  • Jeshi la Polisi kumpeleka ofisini kwake, Mmiliki wa Lugumi.
  • Dereva na mmiliki wa gari bovu likipata ajali kuwekwa mahabusu kabla ya kupelekwa mahakamani.
Faida kubwa ya Lugola, ni kulifahamu vyema Jeshi la Polisi ambalo kwa hakika ni synonymous na Wizara hiyo.

Ushauri kwa Kangi Lugola: Ajitahidi kutoa maagizo kwa staha hasa kwa Wateule wa Rais, hasa IGP kwani pasipo kupata legitimacy ya Sirro, kazi yake itakuwa ngumu.

View attachment 815468
Mh. Waziri Lugola anaonekana kama ni professional, mimi sijui profession yake ni nini lakini nadhani naye ni askari pia. Ninaanza kuona dalili kuwa ata-deliver kwa kiwango cha juu sana katika wizara hii, in short I like him. Hata hivyo nashauri tu maagizo yake anayompa IGP, awe anampa katika staili ya kirafiki zaidi, anapokuwa ni mali kiasi kwake anaweza wakati mwingine akamchanganya asifanye kama anavyomtaka afanye. Sirro is a man of action, kwa hiyo waziri awe comfortable maagizo yake yote anayoyatoa yatafanyiwa kazi kama anavyotka, asiwe mkali sana hata kwa Siroo!
 
Mh. Waziri Lugola anaonekana kama ni professional, mimi sijui profession yake ni nini lakini nadhani naye ni askari pia. Ninaanza kuona dalili kuwa ata-deliver kwa kiwango cha juu sana katika wizara hii, in short I like him. Hata hivyo nashauri tu maagizo yake anayompa IGP, awe anampa katika staili ya kirafiki zaidi, anapokuwa ni mali kiasi kwake anaweza wakati mwingine akamchanganya asifanye kama anavyomtaka afanye. Sirro is a man of action, kwa hiyo waziri awe comfortable maagizo yake yote anayoyatoa yatafanyiwa kazi kama anavyotka, asiwe mkali sana hata kwa Siroo!
Ili tujue anafanya kazi kwa weledi, aamuru jeshi la Polisi lifanye Yale ambayo hayakufanywa na mtangulizi wake sio hayo ya mbwa au kumleta Lugumi ofisini.
Yapo mambo yenye kugusa sana watu kama mauaji ya RAIA kuchunguzwa upya, kupotea kwa watu taarifa kuwa hadharani ya uchunguzi na kushambuliwa kwa risasi RAIA(hata viongozi) mchana kweupe.
Hapo ndio tutaona ubora wake dhidi ya yule aliyeondolewa kwa uzururaji
 
Na kweli huyu Waziri anaitendea haki ajira yake
Yeye ndio Sheriff in Town
Hatusikii matamko kwa Dar pres tena
 
mie alinichekesha madreva watapimwa kilevi kila kituo,lol
 
Nakumbuka kipindi kifupi nyuma, miaka takribani 9 au10 iliyopita, kulikuwa na gazetini moja la kiuchambuzi, liliitwa Rai Nguvu ya hoja.
Kulikuwa na wandishi nguli wa makala za uchambuzi, hasa katika uwanda wa siasa.
Namkumbuka Marehemu Muhingo Rweyemamu (R.I.P) aliyeandika makala moja yenye kichwa kilichosema, "Rais Kikwete Nyamaza Rais Machibya Aongee". Huyo Machibya alikuwa Rais wa Udsm wakati huo na makala hiyo iliandikwa wakati kukiwa na mgomo wa wanafunzi wa UDSM wakidai maslahi yao.
Kulikuwa na manguli kadhaa, kama Generali Ulimwengu, Johnson Mbwambo, Fr. Privatus Karugendo na Joseph Mihangwa, na wengine wengi. Baadaye walihamia Raia Mwema, kisima cha maarifa. Humo wakaendeleza 'libeneke'. Nakumbuka makala zao;
"Je! Siku za furaha zitarudi tena?"
"Nani atawalinda walinzi wetu?"
"Ni nani anayemuongoza kiongozi wetu?"
"Watanzania walitaka Rais wakaletewa Jakaya Kikwete"

Wakati huo, mimi na rafiki yangu Prof. Justin Banyukwa tulikuwa tukiyaita magazeti haya "Nyaraka". Na tulikuwa tukiyatunza ili kurudia rudia kuyasoma.

Zama zimebadilika.
Siku hizi kuna mengi ya kuandika zaidi ya wakati huo. Kama Kikwete alisemwa vile, vipi kwa Magufuli?
Kama teuzi za Kikwete zilileta mtafaruku, vipi teuzi za Magufuli?
Wakati fulani tulikuwa na Jaji mkuu aliyeitwa Chande Othuman, kisha mdogo wake aliyeitwa Rashidi Othman akateuliwa kuwa mkuu wa Usalama wa Taifa. Kulikuwa na kelele nyingi sana juu ya teuzi hizo nyeti kwa ndugu wawili. Watu walihoji, endapo kutakuwa na mgongano wa maslahi katika ofisi hizo, je! Wakuu hao watatafuta suluhu kiofisi au kidugu?

Lakini hayo yamepita, na sasa yapo mengine mengi ya kuandika. Lakini waandishi wamekuwa na hofu kuu. Hofu ya kutekwa na kupotea, usionekane tena. Hofu ya kufungwa kwa maelekezo ya kisiasa, sio sheria.
Hofu ya kuharibiwa biashara.
Hofu ya kutekwa na wasiojulikana.
Ndio maana mengi hayaandikwi. Lakini mtu mmoja kati ya hao niliowataja aliandika, "Imbeni juu ya domo la Wanasiasa". Akiwahamasisha wanaharakati hasa wale wanaofanya harakati kwa kuandika; kwamba waimbe (waandike) yale ambayo wanasiasa wanayachukia, ambayo ni ya maana kwa Taifa lakini si ya maana kwa wanasiasa.

Natamani siku zile zirudi tena. Natamani leo tuandike namna Kangi Lugola anavyoboronga katika wizara ya mambo ya ndani, mapema kabisa. Natamani tuandike kwa kukosoa mabadiliko haya ya wizara ya mambo ya ndani, kupwaya kwa nafasi hii nyeti aliyokabidhiwa mtu wa vituko na vitendo vya kikaragosi. Mbaya zaidi mwenyewe anaamini anafanya mambo ya msingi.

Wakati Mwigulu Nchemba akihudumu wizara hii ya mambo ya ndani, alibanwa.
Hakuweza kufurukuta kwa sababu ya kujua mipaka yake ya kazi, lakini pia akiwa 'ameduwaa' sana na kushangaa shangaa huku muda ukienda bila kuchukua hatua pale alipotakiwa kufanya hivyo. Alikuwa akizungukwa.
Mwigulu ni mtu ambaye, angalau alijua cha kufanya, lakini hakuweza kufanya kwa sababu ya 'kubanwa' na nguvu zaidi ya zile alizokuwa nazo. Ndio maana alikuwa anatoa kauli za mdomoni huku moyo wake ukipata shida, ili kulinda nafasi, kwa faida za kisiasa za leo na baadae.
Huyu tuliyeletewa sasa, hajui hata afanye nini.
Tulikuwa na waziri wa mambo ya ndani aliyeshindwa kuonesha uwezo wake kwa sababu za kuharibika kwa mfumo wa kidola (ukitoa jeshi la wananchi), na sasa tumeletewa Kangi Lugola asiyejua la Kufanya.
Natamani tumuandike Kangi Lugola bila hofu, ili tusiendelee kushuhudia ongezeko la vitendo vya hovyo ndani ya vyombo vyetu vya dola vya ndani.Tuandike na kuchambua bila hofu, namna Rais Magufuli alivyomfuta kazi waziri wa mambo ya ndani, kwa sababu ya kushindwa kutekeleza majukumu yake, lakini kwa hamaki kuu, akatuletea Kangi Lugola.
 
Mkuu asante kwa uandishi wa enzi za Rai. Nakumbuka enzi hizo nilikua secondary ila nilikua nasoma sana hilo gazeti bro zangu walikua hawalikosi na walikua wakilisoma wanaanza kuhadithiana hivi jinsi gazeti lilivyotamu nikajikuta nimekua member nasoma kila page. Daah, gone are those days
 
Back
Top Bottom