Kandoro asitisha wizi wa gari la serikali

ntamaholo

JF-Expert Member
Aug 30, 2011
12,906
6,909
Hbr wana JF.
Hbr nilizozipata ni kwamba, Mh. Abasi Kandoro aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Mwanza kwa sasa mkuu wa mkoa wa Mbeya, ameamua kuachana na mpango wake wa kujiuzia kwa milioni mbili tu 2,000,000/= gari la mamilioni ya shilingi. Gari hilo ni TOYOTA V 8 namba za usajiri STK 3643 lenye speed mita 260. watalamu wa magari mtaiweka vizuri.

Ilikuwa ni gari ya mkuu wa mkoa aliyepita kabla ya kandoro, alipokuja kandoro akaona haimfai japokuwa ilikuwa na miaka chini ya kumi tangu inunuliwe kwa mamilioni ya shilingi. Kandoro alinunua nasikia wanataja G8 V8 sina hakika kwani magari miye siyajui lakini ni la kifahali na ni piston 8 wakati ya awali ilikuwa piston 6 Kandoro aliyoona haimfai akiwa ofisini lakini inamfaa ikiwa mali yake.

Awali niliriport mpango huo kupitia JF kwa linki
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/171833-ya-kandoro-inatisha-ajiuzia-gari-la-tzs-milioni-300-kwa-milioni-2-tu.html , ni maneno na ufuatiliaji wa wadau mbalimbali ulifanikisha kuokoa gari hilo.

Kati ya sababu zilizomfanya kuahirisha kukwapua gari hilo ni pamoja na:
1. Kufuatwafuatwa na watu wa kada mbalimbali walienda kumhoji juu ya taarifa zile.
2. Kujisafisha kisiasa kwani ana mpango wa kugombea jimbo moja la mkoani Iringa na kama angeendelea na wizi ule, vyama vya upinzani vingemshambulia kwa kuiba mali za serikali huku akitumia ofisi za umma.

Hata hivyo, wapenzi wa maendeleo, tuendelee kulilinda gari hilo ili siku likikosekana katika viwanja vya Ofisi za mkuu wa mkoa, tupae tena hewani kuhoji liko wapi isije kuwa tumeingizwa mkenge.

Nawasilisha.

linki:-
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...gari-la-tzs-milioni-300-kwa-milioni-2-tu.html
 
Bravo!
Hii ndiyo kazi ya awali ya uandishi....kuripoti kwa jamii ambako kunaleta impact!
Mzee, aksante sana, kompyuta na modem yako vimeokoa milioni zaidi ya mia!
 
Utakuta Kandoro kasitisha kumbe kuna mtu ana mpango wa kuinyakua
 
bravo!

ni sahihi mkuu, kwa pamoja tutaokoa mali za walipa kodi mpaka tutakapoweza kuzuia ununuzi wa magari ya kifahari
 
Utakuta Kandoro kasitisha kumbe kuna mtu ana mpango wa kuinyakua

Atakaye thubutu tutajua lazima na yeye tumharibiwe mipango yake mufu. kwa sasa gari hilo linafanya kazi za hapa mkoani na mara nyingi limepaki kusubiri ziara za mawaziri au viongozi waandamizi wa serikali ya baba ritz1
 
Mnalishangaa hilo! Hebu pelelezeni Magari yaliyokuwa yamenunuliwa na CCM kipindi cha Uchaguzi wa 2010 wameuziana kwa TSh.1 (Shilingi moja) Nimebahatika kuuona mkataba huo uliosainiwa na Wakili mmoja ambaye CCM wanamtumia sana kwenye Mambo yao ya Kishenzi na ndie aliyemsaidia Ritz Zero kufungua kesi yake dhidi ya Dr. Mmoja wa watu waliouziwa gari kwa bei hiyo ni Dr. Mohamed Ghalib Bilal. Kama kuna mtu anayeweza kufuatilia hili afuatilie na atakuja na majibu haya haya.
Nilipouliza ni kwanini Sh. 1 si bora wangepewa bure, nikaambiwa kisheria unapomuuzia mtu kitu lazima utaje gharama/thamani. (Wanasheria tunaomba mlifafanue hili) Otherwise wamepewa bure.
 
Huu wizi waandishi wa habri waufatilie kwani ni jukumu letu kulinda mali zetu,pili mkuu tunashukuru jitihada zako zimeokoa mil kadhaa za umma thanx thumb up my dawg
 
hongera mkuu hii kitu niliiona kweli na am happy kupata feedback from you once again
 
Mnalishangaa hilo! Hebu pelelezeni Magari yaliyokuwa yamenunuliwa na CCM kipindi cha Uchaguzi wa 2010 wameuziana kwa TSh.1 (Shilingi moja) Nimebahatika kuuona mkataba huo uliosainiwa na Wakili mmoja ambaye CCM wanamtumia sana kwenye Mambo yao ya Kishenzi na ndie aliyemsaidia Ritz Zero kufungua kesi yake dhidi ya Dr. Mmoja wa watu waliouziwa gari kwa bei hiyo ni Dr. Mohamed Ghalib Bilal. Kama kuna mtu anayeweza kufuatilia hili afuatilie na atakuja na majibu haya haya.
Nilipouliza ni kwanini Sh. 1 si bora wangepewa bure, nikaambiwa kisheria unapomuuzia mtu kitu lazima utaje gharama/thamani. (Wanasheria tunaomba mlifafanue hili) Otherwise wamepewa bure.

waligawiana magari yaliyonunuliwa kwa bil.40 pesa za epa. yalikuwa ni landcruiser mpya 200
 
hongera mkuu hii kitu niliiona kweli na am happy kupata feedback from you once again

yeah, ni vizuri kutoa update ya vitu hivi. kama tusingeandika gari lingeuzwa kitapeli. Kandoro mwenyewe alichoka na kuwalaumu waandishi wa habari na baadhi ya watendaji nadi ya office yake kwani ndio waliovujisha siri hiyo ikawa gumzo ofisini mpaka ikafika hapa JF
 
huu wizi waandishi wa habri waufatilie kwani ni jukumu letu kulinda mali zetu,pili mkuu tunashukuru jitihada zako zimeokoa mil kadhaa za umma thanx thumb up my dawg

siyo jukumu la waandishi wa habari pekee, ni wajibu wa kila mtanzania kulinda mali za umma. Ili mradi tu uweze kuandika, hapa hakuna editor kila mtu anaandika anvyoweza. Lengo kuu ni kulinda mali za walipa kodi. Usijewanyima watanzania taarifa kwa kisingizio cha waandishi wa habri.

Mimi siyo mwandishi wa habri, lakini nikiona jambo linakwenda kinyume, nitaliandikia na kama wana habari wataliona linafaa wataangalia namna ya kuliweka vizuri. Au vipi wakuu
 
kweli kufumaniwa kubaya, mzee katema vx jua la mchanaaaaaa

kama ningekuwa na kamera ningepiga picha ya gari hilo. Lakini simu yangu ya mchina hainiwezeshi kupiga picha na kuziupload/kuziatach hapa. Ni gari zuri mno, likizimwa linasinyaa na kuwa dogo kimtindo, likiwashwa tu, linainuka na kuwa juu kidogo tofauti na likiwa limezimwa.
 
Utakuta Kandoro kasitisha kumbe kuna mtu ana mpango wa kuinyakua
Hakika akina Kandoro wako wengi. Wapo waliokuwa wanalitaka lakini wakashindwa kwa sababu Kandoro alikuwa boss wao. Sasa kaondoka ni nafasi yao kulipora gari hilo. Kweli tuchunge viwanja hivyo tuone kama daima litakuwepo au sasa litabebwa kinyemela zaidi.
 
Hongera mkuu kwa kazi nzuri iliyookoa mali iliyonunuliwa kwa kodi wa walalahoi. wazalendo na wenye uchungu na nchi hii tufichue vitendo vyote viovu vinavyofanywa na mafisadi kuhujumu mali ya umma
 
Utakuta Kandoro kasitisha kumbe kuna mtu ana mpango wa kuinyakua

KWA Mwanza nadhani wanaogopa, labuda huko mbeya. watu wa Mbeya mjiandae. Lengo lake apate gari la kufanyia sijui kampeni hiyo 2015? Mshahara wake mkubwa, si aende shoo room? au aende kukopa benki anunue kwa halali
 
Mbeya hawahitai kujiandaa na chochote, kwasababu ndivyo walivyo.
Muulize Matteo Qares kilichompata baada kutoa kauli ya dharau kwa wananchi pale walipotwa na janga tetemeko la ardhi.
 
Nyie mnashanga ya kandoro! Wakati mwenzenu enock aliyekuwa mkuu wa mkoa mara baadae kagera amejinunulia gari alilokuwa anatumia:
walikuwa safarini ghafla injini ikanoki, akafika ofisini na kuandika barua gari hili bovu, jamaa wa magogoni wakatuma kitu kipya.
Kupigwa mnada akalichukua kwa makubaliano akatwe kwenye stahili zake......mjini shule!
 
Hbr wana JF.
Hbr nilizozipata ni kwamba, Mh. Abasi Kandoro aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Mwanza kwa sasa mkuu wa mkoa wa Mbeya, ameamua kuachana na mpango wake wa kujiuzia kwa milioni mbili tu 2,000,000/= gari la mamilioni ya shilingi. Gari hilo ni TOYOTA V 8 namba za usajiri STK 3643 lenye speed mita 260. watalamu wa magari mtaiweka vizuri.

Ilikuwa ni gari ya mkuu wa mkoa aliyepita kabla ya kandoro, alipokuja kandoro akaona haimfai japokuwa ilikuwa na miaka chini ya kumi tangu inunuliwe kwa mamilioni ya shilingi. Kandoro alinunua nasikia wanataja G8 V8 sina hakika kwani magari miye siyajui lakini ni la kifahali na ni piston 8 wakati ya awali ilikuwa piston 6 Kandoro aliyoona haimfai akiwa ofisini lakini inamfaa ikiwa mali yake.

Awali niliriport mpango huo kupitia JF kwa linki
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/171833-ya-kandoro-inatisha-ajiuzia-gari-la-tzs-milioni-300-kwa-milioni-2-tu.html , ni maneno na ufuatiliaji wa wadau mbalimbali ulifanikisha kuokoa gari hilo.

Kati ya sababu zilizomfanya kuahirisha kukwapua gari hilo ni pamoja na:
1. Kufuatwafuatwa na watu wa kada mbalimbali walienda kumhoji juu ya taarifa zile.
2. Kujisafisha kisiasa kwani ana mpango wa kugombea jimbo moja la mkoani Iringa na kama angeendelea na wizi ule, vyama vya upinzani vingemshambulia kwa kuiba mali za serikali huku akitumia ofisi za umma.

Hata hivyo, wapenzi wa maendeleo, tuendelee kulilinda gari hilo ili siku likikosekana katika viwanja vya Ofisi za mkuu wa mkoa, tupae tena hewani kuhoji liko wapi isije kuwa tumeingizwa mkenge.

Nawasilisha.

linki:-
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...gari-la-tzs-milioni-300-kwa-milioni-2-tu.html
shukran mkuu kwa kazi nzuri. Hivi jamani hamna hata mmoja aliyeko ccm msafi. Mbona hata wale ambao sikuwatarajia inakuwa kinyume chake?
 
Back
Top Bottom