Kanda maalum ya ushirikina

Kanda maalum ya ushirikina

View attachment 397023kila kinachotokea kwenye ulimwengu wa macho ya kawaida ni replica ya ulimwengu wa roho! (Ushirikina ni mkusanyiko wa juju uchawi ulozi chumaulete kuwanga nk)
Tunapozungumzia kanda maalum ya kitu maana yake ni kwamba eneo hilo lina uhitaji wa ziada wa huduma fulani
..mfano Dar kwa sasa ni kanda maalum ya kipolisi kutokana na matukio ya ujambazi kushamiri! Kariakoo kwa sasa ni kanda maalum ya kodi za mamlaka ya mapato Tanzania kutokana na uhitaji wake!
Eneo lote la pwani ya Dar nenda mpaka bagamoyo msata wami pangani mbwewe mkata mpaka tanga mjini ni kanda maalum ya ushirikina
Hapa ndio kuna vilinge vingi vya ushirikina kuliko sehemu nyingine yoyote Tanzania, hapa ndio kuna wachawi waganga na walozi(kwa ujumla wao washirikina wa kila aina)
Hapa ndo kuna kila aina ya matibabu kuanzia miti shamba tunguli kisomo mpaka uganga/uchawi wa kitabu
Unaweza kwenda mikoani na sehemu tofauti kama gambosh nk lakini ukashindwa kwa hakika kukutana na ushirikina halisi....huu ukanda hukosi
View attachment 397030
Kwanini ukanda huu lakini?
Mazingira na jiografia yanaruhusu, malighafi za baharini na nchi kavu vinapatikana kwa wepesi urahisi na kwa wingi! Taka viungo vya binadamu hupati shida! Taka makombe na mazao bahari mengine ni rahisi mno! Taka variaties ya mizizi miti magome na hata matunda na majani huku sio tatizo kabisa
Lakini kwanini isiwe ndani ya Dar na ni nje ya Dar na maeneo ya karibu au mbali kidogo?
Ushirikina ni mambo ya kiroho zaidi yasiyo na ithibati za kisayansi! Yanahitaji ukimya utulivu upweke usiri uchache wa watu na kitu chochote kilichoendelezwa na binadamu kwenye ulimwengu wa teknolojia..teknolojia na usasa ni sumu kubwa kwenye ushirikina
Unaposhuhudia misafara isiyokoma kwa waheshimiwa sana Unaposhuhudia ajali za kila siku! Unaposhuhudia upotevu wa watu wazima na watoto! Unaposhuhudia mambo ya ajabu ajabu usishangae sana bali jua kwamba uko karibu kabisa na ukanda maalum wa kishirikina View attachment 397053
Huu, kama kama kawaida yako Mshana.Hebu tuambie basi, mashetani yanaweza kuzaa na mswahili?
 
Mkuu ina maana Pwani ina rasilimali za kutosha juu ya uchawi? Je wale wachawi wa kanda za mbali na pwani kama sumbawanga hufunga safari kuja pwani kufuata rasilimali?
Inategemea na aina ya uchawi
 
Sawa kamishna wa kanda hiyo,kwa hyo huku sumbawanga kunaongozwa na makamishna wasaidizi waandamizi sio eee?
 
Mshana unabidi uchunguzwe wewe...kama sio jipu basi utakuwa kipele na utatumbuliwa hivohivo maana siku hizi majipu yanajificha kwenye vipele...we toa siri za watu tu.
 
Historia ya uchawi inaaza tangu uumbaji wa ulimwengu (kwa waamini na waaminio) Mungu aliumba kila kitu na kinyume chake...uchawi ni nguvu hasi kinyume cha nguvu chanya
Ha ha kwahiyo alikuwa anataka kujichallange mwenyewe ama..?
 
Where there is a demand there is always a supply
Vile vifo vingi mfululizo vilivyotokana na ajali mwezi wa tatu mwaka jana mpaka leo hakuna mwenye maelezo yaliyonyooka japo kuna watu fulani wanajua kila kitu na kwanini karibia zote zilitokea kanda hii

kumbe kuishi sitimbi ni bora zaidi kuliko mjini.. lower demand, lower supply 😎
 
Challenge ni ya uumbaji si ya Mungu kwakuwa mwili ama roho haviwezi kujidhuru
"challenge ni ya uumbaji"
na vitabu vyake vinasema muumbaji ni yeye basi kuna upungufu ktk uumbaji wake na kama roho na mwili haviwezi kujidhuru mbona mnasema mtu akiwa ktk mwili akitenda dhambi inaenda kuhukumiwa roho yake..?
 
"challenge ni ya uumbaji"
na vitabu vyake vinasema muumbaji ni yeye basi kuna upungufu ktk uumbaji wake na kama roho na mwili haviwezi kujidhuru mbona mnasema mtu akiwa ktk mwili akitenda dhambi inaenda kuhukumiwa roho yake..?
Hukumu inatolewa na mwingine sio within self
 
Hukumu inatolewa na mwingine sio within self
sijauliza anaetoa hukumu bali hilo dhara baina ya roho na mwili unalizungumziaje wkt umesema roho na mwili haviwezi kujidhuru
 
Back
Top Bottom