Kamwe usimkabili mchepuko wa mumeo

Kamwe usimkabili mchepuko wa mumeo

Kasiano Muyenzi

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2018
Posts
13,972
Reaction score
22,933
Sio busara kumkabili mchepuko wa mume wako. Usithubutu kufanya hili kosa. Nasisitiza kwa ukali kabisa sio busara kumkabili mchepuko wa mumeo.

Nina sababu zangu mbili za kukushauri hivyo;

1. Ikiwa mume wako ana tabia ya kuchepuka, hawezi kuridhika na mwanamke huyo mmoja ataendelea kurukaruka kutoka kwa mwanamke mmoja hadi mwingine. Hebu jiulize utaweza kukabili wanawake wangapi? Tunza jibu lako.

2. Huna biashara ya kumdhibiti mchepuko wa mumeo, wewe sio chuo chake cha maadili. Huyo mchepuko wa mumeo hawezi kukuahidi kuwa atakuwa mwanamke mzuri kwa mumeo. Wala huna uwezo wa kumgeuza huyo mchepuko awe mtakatifu kwa mumeo.

Tambua mara moja kuwa kosa lipo kwa mume wako ambaye amevunja ahadi ya kuwa na wewe tu. Ongea na mumeo kwa heshima licha ya hisia zako zenye kuumiza. Huwezi kuushinda ubaya kwa ubaya.

Kupigana na mchepuko wa mumeo ni kujidhalilisha tu. Ikiwa nyote wawili mko tayari kufanyia kazi ndoa yenu, basi ndoa yenu inaweza kusalimika.

Simama katika malengo yako ya ndoa na jinsi utakavyoyatimiza. Unaweza kuchagua kuendelea na mumeo ama kuachana naye.

Hii inaweza kuhitaji mwongozo kutoka kwa mkufunzi wa ndoa yenu.

Ubarikiwe.
 
Sio busara kumkabili mchepuko wa mume wako. Usithubutu kufanya hili kosa.

Nasisitiza kwa ukali kabisa sio busara kumkabili mchepuko wa mumeo.

Nina sababu zangu mbili za kukushauri hivyo.....

1. Ikiwa mume wako ana tabia ya kuchepuka, hawezi kuridhika na mwanamke huyo mmoja - ataendelea kurukaruka kutoka kwa mwanamke mmoja hadi mwingine. Hebu jiulize utaweza kukabili wanawake wangapi? Tunza jibu lako.

2. Huna biashara ya kumdhibiti mchepuko wa mumeo - wewe sio chuo chake cha maadili. Huyo mchepuko wa mumeo huyo hawezi kukuahidi kuwa atakuwa mwanamke mzuri kwa mumeo. Wala huna uwezo wa kumgeuza huyo mchepuko awe mtakatifu kwa mumeo.

Tambua mara moja kuwa kosa lipo kwa mume wako ambaye amevunja ahadi ya kuwa na wewe tu.

Ongea na mumeo kwa heshima licha ya hisia zako zenye kuumiza. Huwezi kuushinda ubaya kwa ubaya.

Kupigana na mchepuko wa mumeo ni kujidharirisha tu.

Ikiwa nyote wawili mko tayari kufanyia kazi ndoa yenu, basi ndoa yenu linaweza kusalimika.

Simama katika malengo yako ya ndoa na jinsi utakavyoyatimiza. Unaweza kuchagua kuendelea na mumeo ama kuachana naye

Hii inaweza kuhitaji mwongozo kutoka kwa mkufunzi wa ndoa yenu.

Ubarikiwe
Nakubusu njoo huku 😜😎☺️🏃🏃🏃🏃
 
Mume akichepuka na mke achepuke, tena abebe mimba nje afu ambambike mumewe,

Both team to score. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Michepuko iheshimiwe

 
Back
Top Bottom