Fall Army Worm
JF-Expert Member
- Jan 8, 2015
- 19,370
- 14,517
Heshima zenu Wakuu....!!!!, Awali ya yote nianze kwa kushukuru MUNGU, kwa kutulinda Salama kwa Mwaka mzima. Ninasema Baba Asante kwa Huruma na Upendo wako usio na Kifani, aidha tunakuomba utulinde na Mwaka huu tunaotegemea kuuanza masaa machache yajayo.
Baada ya Shukurani na Maombi hayo sasa nije Moja kwa Moja kwenye Mada. Ni hivi kuna Tabia Chafu kwa baadhi yetu hasa Vijana kutumia Vibaya Sherehe hasa Mwaka mpya kwa kutenda maovu. Utakuta mtu Mwaka mzima amejitahidi kuishi vizuri akimpendeza MUNGU, lkn ajabu ni wakati ule wa Kuuaga Mwaka na Kuukaribisha Mwaka mwingine, Ndipo utakapoona au kusikia watu wakisimuliana na kujisifu km vile Aah !!, Usiku ule wa Mwaka mpya nilikunywa pombe Mpaka majogoo. Wengine utawasikia wakijisifu, japo ni Uzuzu kuwa Walichezea Visimi balaa yaani Walifanya Uzinzi Vilivyo, Wengine Watajisifia kwa kuchoma matairi, au kuvuta bhangi au kucheza Disco Mpaka Asubuhi.
Binafsi ninawaasa Ndugu Zangu tusifanye hivyo kwa Mwaka huu badala yake tutumie muda huo Kumshuru MUNGU kwa Wema wake kutulinda Mwaka mzima maana ni Wengi walitamani Kuuona Mwaka mpya lkn walishindwa sasa kwanini kutumia Sherehe hizi vibaya kwa kufanya maovu ???. Ni Busara baada ya Kumshukuru MUNGU, ukakaa na Familia yako ukafurahi kwa kiasi lakini, au basi na Rafiki zako kwa kiasi sio Mpaka kupoteza Network au kupelekea kutenda uovu. Tunapotenda maovu wakati MUNGU ametulinda Mwaka mzima, tunakuwa tunamkufuru MUNGU, kiasi kwamba MUNGU anajilaumu kwa kukulinda Mwaka mzima wakati kuna watu Wengi waliokatishwa maisha na hali walikuwa ni wema machoni pake. Chonde sana Tusizitumie sherehe za Mwaka mpya kutenda UOVU.