Kamusi zina maana gani?

jimmy mroso

New Member
Dec 2, 2014
2
0
Habari! Hivi mm nataka kujua kuna maana gani ya kusoma kamusi za kiswahili wakati tunaongea kiswahili??
 

Watu8

JF-Expert Member
Feb 19, 2010
53,131
2,000
Kamusi ni kitabu cha marejeo chenye msamiati uliokusanywa kutoka kwa wazungumzaji wa jamii fulani na kupangwa katika utaratibu maalumu, kisha kufafanuliwa kwa namna ambayo wasomaji wanaweza kuelewa.

AU

Kamusi ni orodha ya maneno yaliyo katika nakala ngumu au laini yaliyopangwa kialfabeti na kutolewa maana pamoja na maelezo mengine na kuhifadhiwa katika kitabu, santuri, simu, tarakilishi au katika mfumo wa kielekroniki.
 

Watu8

JF-Expert Member
Feb 19, 2010
53,131
2,000
Hivyo kwa mantiki ya maana hizo hapo juu bila shaka ni ngumu kuwa na uelewa wa maana ya kila neno kwenye lugha ya Kiswahili...

Na kamusi hutumika kama nyenzo ya kutafuta maana zaidi iliyo fasaha ya maneno au tafsiri tusizozielewa.

Pia kuna kamusi zenye kujumuisha lugha mbili tofauti zikielezea tafsiri ya misamiati kwa lugha mbili. Kamusi za namna hii hutumika kama nyenzo kwa mzungumzaji wa lugha moja kupata tafsiri mbadala kwa lugha nyingine.
 

kasigazi kalungi

JF-Expert Member
Dec 22, 2013
3,411
2,000
Kwa kuongezea hapo, faida nyingine za kamusi ni kama ifuatavyo;
1. Kumuwezesha mtumiaji wa lugha husika kujua matamshi sahihi ya maneno.
2. Kujua asili ya neno husika mfano neno sheria utaambiwa asili yake ni kiarabu.
3.Kuonesha matumizi mbalimbali ya maneno. 4.Mifano ya matumizi ya maneno katika sentensi.
5. Kupata taarifa za kisarufi.
NB: Kazi ya kamusi sio kutoa maana ya maneno tu, kuna taarifa nyingi zinazopatikana katika kamusi kama nilivyozitaja.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom