kampuni za simu zinatuibia(kodi)

Godwine

JF-Expert Member
Jan 15, 2010
1,371
281
Tanzania ni nchi inayoendelea kwa kasi katika matumizi ya simu ikiwa na wastani wa watumiaji wa simu za mkononi millioni 15, kwa wastani inasadikiwa kila mtanzania anatumia shs mia tano kwa siku kwa hiyo kwa jumla za fedha wanazopata ni kama shillingi bilioni 7 kwa siku. kutokana na mapato hayo kama tukitoza kodi ya VAT na zinginezo kwa asilimia ishirini(20%) inatakiwa tupate shs billion 1.5 kwa siku kwa hiyo ukichukua kwa mwaka siku kama 360 inakuwa shillingi billion 540, lakini cha kushangaza unakuta TRA wanakusanya chini ya billion 100 kwa ujumla huu ni upungufu wa zaidi ya shs billion 440 kwa mwaka, uzembe huu unaligharimu taifa kwa kiasi kikubwa mbaya zaidi haya ni makampuni ya kigeni yanaondoka na fedha zetu kwa hiyo ni kitu cha ajabu sana kuacha kiendelee kwani taifa linakosa mapato makubwa sana,
napenda nitoe wito kwa jamii ya watanzania kupigania upotevu huu mkubwa hili kukuza uchumi wa nchi yatu kwani tunaibiwaaaaaaaaaaaaaa
je watanzania hatuna wasomi hata wa kutathimini kodi
au kuna tatizo gani?
 
Unashtukia shuka asubuhi! Wizi ulianza tangu zamani haya unayoyaona wanayajua ila wanakaa kimya... MLUNGULA ndio matokeo yake!!
 
Correction VAT is 18% and not 20%. Na usemayo ni kweli lakini kumbuka VAT is not direct tax ambayo inatozwa directly kwenye income Vat is indirect tax ambayo inatakiwa kuchargiwa on sale. Na saler is not the one who is paying that tax but is an agent of the final consumer!! Kwa mashirika ya cm wanajitetea kuwa mauzo madogo na kwa kuwa bado haijapatikana mbinu ya kugundua exactly ni vocha ngapi zinazoweza kuuzwa per day ila ni kubase kwenye assumption tu kama ulivyokisia wewe hapo ndo tunapoibiwa!! Ila ki ukweli kampuni za simu zinahitajika kuangaliwa tofauti on Tax issue!!
 
Hii ni global issue. Makampuni ya simu ni fat heads. Always ni win win situation. Ndo maana management zao zina bonus za kufa nguruwe.
 
aah, mwana kujua kiasi cha vocha kilichotumika, ni rahisi saana,
kampuni zote zina 'control ya vocha zilizouzwa, ndio maana ukiingiza vocha uliotumia itakataa.kama tra wakiamua kua macho, wanaweza pata jumla ya vocha zote kwa kila mtandao,na kiasi gani liliuzwa- ubavu wa kudai takwimu sahihi wanao na ni kosa kubwa kudanganya juu ya mapato yako ili ukwepe kodi halisi.
natoa changamoto kwa watz wenzetu ktk vitengo vya mauzo wapo ambao watajua kiasi halisi kiliuzwa waende tra kupuliza filimbi [wapewe donge nono ila pia tra watawalindaje hao watu wasifukuzwe kwa kusema ukweli?]
ii nji yetu tajiri saana tu, tatizo tumelala-tukiamua kuamka nakwambia kijana wangu miaka 3 nji ii itakua nzuri kuishi-ila ulafi/ujuha/ubazazi tuamua kuacha.
kila kitu chema tunacho sie- uzalendo na kuheshimu kazi ndio hatuna.
 
ooh, akashube umenichafua ladha ya chakula sina-
vije useme 'always ni win win situation'
au unamaana win win wawini tu wao wageni na mabwanyenye?unakumbuka cmu za viselula zilivyoanza kuingia '85 bei ikiwa $300- 500 @ moja,
apo souz zilikua rand 150/180 zile kama mche {$30-60 @ moja},
sie na ushamba wetu tukajikamua kununua kuonyesha nasi tumo kumbe twaliwa- wametupiga hasa hawa usiseme ni kama wizi mchana kweupee.
tunalizwa sana na hatupati kitu kama tusipoamka usingizini leo na si kesho.
 
Will be back on this.......! sometimes, tukofikiri kuna kodi inakwepwa kunakuwa sio huko, na kule tusikodhania wanakwepa ndo ndiko ukwepaji mkubwa unatokea....will be back!
 
watu wa namna hii wanatakiwa Tanzania maana watanzania ni sisi na mali za Tanzania tumepewa sisi tufaidi pamoja na vizazi vijavyo. Lazima tuwajibike kuhoji na tusichoke wala kutishika. Kwani huwezi kuhama nyumba kwa sababu tu nyoka ameingia ndani ya nyumba. Hili ni shirika mojawapo kama kewli lakini yapo mengine mengi. Inasikitisha mno.
 
usiniambie kwamba tra hawana jinsi ya kuwabaini hawa watu wanavyokwepa kodi wakati kila baada ya miaka mitano unaona wanabadilisha majina ya kampuni bado watu awajiulizi kwann sidhani kama wanalipa kodi wakati ni wawekezaji wana grace period cha miaka mitano ikifika wanabadilisha jina wasema wamepata hasara ivyo wanauza sikuhazigandi wanazidikupeta
 
Correction VAT is 18% and not 20%. Na usemayo ni kweli lakini kumbuka VAT is not direct tax ambayo inatozwa directly kwenye income Vat is indirect tax ambayo inatakiwa kuchargiwa on sale. Na saler is not the one who is paying that tax but is an agent of the final consumer!! Kwa mashirika ya cm wanajitetea kuwa mauzo madogo na kwa kuwa bado haijapatikana mbinu ya kugundua exactly ni vocha ngapi zinazoweza kuuzwa per day ila ni kubase kwenye assumption tu kama ulivyokisia wewe hapo ndo tunapoibiwa!! Ila ki ukweli kampuni za simu zinahitajika kuangaliwa tofauti on Tax issue!!
labda kwa kusaidia wale jamaa wanapigwa Corporate tax. Lakini kumbuka hii ipo subject to profit na humo ndani yake ndiyo kuna issue za capital expenditures. Hapo ndiyo kazi inapoongezeka ni vigum saana kuona profit. Unaweza kuona haya makampuni yanawanunulia wafanyakazi wake magari ukadhani ohpss ni babkubwa kumbe upande wa pili tunayalipa siye wenyewe.
 
Its true, but Corporate ni 30% on profit, na mpaka ufikie profit available on tax kuna mengi sana unatakiwa kutoa na kuna vingine ambavyo ni allowable ambavyo unatakiwa kuvideduct ili kuavoid double taxation. Ndo mana taxpayers wengi wanadeclear loss on profit means hatozwi kodi but anakuwa carried forward!! Na mpaka kugundua anafanya froud ni mpaka maauditor waende!! Kodi kubwa iliyotakiwa kupatikana hapo ni on sales ambayo ni VAT!!
 
Definetly, I agree with you lakini kumbuka VAT hawachajiwa wenye kampuni bali watumiaji. Wenye kampuni they are regarded as collecting agents. Of which I dont real believe km kucheat kwenye VAT ni kubwa km Corporate maana hiyo wanaassess kwenye input na output km kunarefund kampuni inaweza kuclaim. Kimsingi shughuli kubwa ni kwenye Profit ambayo inalead into corporate tax. Hao jamaa, they are exaggerating expenses, in the end less or no or carried forward they are losses for the sake of claiming taxes in the coming year. Kinachoweza kusaidia haya makampuni (kulipa kodi itakiwayo) ni kuyafanya yawe listed, hapo itaondoa ukiritimba na kuongeza shareholders kwahiyo supervision itwakuwa widened. Pia nadhani wangecreate some sort of independence kwenye assessment ya financial statements zao for tax purposes. Maana if you have few individuals reviewing a particular company continously lazima tax itakuwa ndogo.
Note; Kwenye kulist wanatakiwa waandae mazingira na si kuwalazimisha
 
ooh, watz kupigwa tulipigika toka enzi,nakwambia kama tra wakiamua kufuatilia ni rahisi tuu mbona- ipo rikodi ktk @ kampuni ya kiselula ya na. za vocha wameuza na za kiasi gani[ndio maana ukijaribu kufoji kuingiza vocha iliotumika haikubaliki] na ivo kwa mtaji huo tra wafanya kazi yao kifanisi -si suala la kukisia watajua kodi inayopas
wa kulipwa ;kanuni iko kua mlipaji anatakiwa aipeleke menyewe kwa
watoza ushuru na akatamke hio ndio kima kamili-akidanganya akaipu nguza ni kosa kubwaaa na faini yake usiseme- uko markani ukiwa na kesi na IRS{idara ya kodi } ni balaa usiombee!huponi .
Tz tuna kila chema, tukiamua kujenga nji ii miaka 3 tu nakwambia dunia itagwaya uchumi wetu umekuaje, tatizo letu kubwa ni kua hatuusemi ukweli, tunaona viashiria kua nani anaharibu kazi mahali, badala ya kusema wazi na kukemea uozo/upuuzi huu tunabaki kuteta chini chini na kulaumu-ukisema ukweli mnoko,utasakamwa na kuundiwa kisa, maana
tunalindana- mtu wa mtu huyo,mtoto wetu huyo, aa mwache tu mbona wengine walifanya hayo hayo wakaachwa leo huyu kazidi nini?,izo ni chuki binafsi au unamwonea gere umekosa kua pale ungefanya nini cha ajabu_ kama ungepewa ile nafasi?[na kuna ukweli kiasi ktk hayo maana sie ni jamii ya wakwapuaji ukiwahi kwapua mapema ujiondokee- kwani nji ii ina wenyewe- wako wapi ?uridhi kwa vijana ni kua wajifunze kuvuna kabla hawajapanda kitu chochote-huu ni ujinga lazima kuukataa]adui wa watz ni sie wenyewe.
Lazima tuamke leo si kesho-na kuamua kuanza kuweka misingi jinsi ya kujenga taifa letu, nakwambia misaada ya wafadhili sio jibu-lazima sie tuthamini kazi,kwa vitendo na viongozi waaze wao kuonyesha dira kwa vitendo-inahitaji upya wa mawazo na dhamira ya kweli-
sio kampuni za simu tuu- dhulma ipo tele ktk uvunaji wa m/asili zetu - madini,misitu ,wanyama pori,mazao ya bahari- tukiamua tunaweza
=Botwana ,Namibia, Ghana ,ooh hata kadogoo Rwanda katuacha mbalii
tuamke usingizini,tukatae ubinafsi,tuseme kweli na tujali kazi inawezekana!
 
haa nimesikitishwa na kauli ya waziri kusema wanakusanya shillingi billion 206 wakati ukweli ni chini ya billion 100, akijibu swali bungeni wiki iliyopita alitoa takwimu nadhani zisio sahii
 
Wiki iliyopita Bunge limepitisha muswada wa sheria ambao unazitaka kampuni za simu kujiunga na soko la Hisa la Dar es Salaam.

Kuna haja ya kuwa na timu maalum ya kukagua mapato halisi ya kampuni za simu. Binafsi ningeenda mbali zaidi na kuweka utaratibu ambapo Voucher zote zinakuwa UNDER CUSTOM BONDED FACILITY.

Hii ni global issue. Makampuni ya simu ni fat heads. Always ni win win situation. Ndo maana management zao zina bonus za kufa nguruwe.

Umepewa ruhusa kutumia hiyo avatar hapa jamvini? Mimi nilifahamu huyo ni Invisible, Je unaweza kufafanua au ni one and the same? If the later is true no worries.
 
Nafurahi kusikia ya kuwa sasa kamati ya Bunge ya bwana zitto na deo Filikunjombe wameweza kulioni hili. sasa ni jukumu moja tu la kuzuia wizi wa makampuni ya Simu
 
Hii ni global issue. Makampuni ya simu ni fat heads. Always ni win win situation. Ndo maana management zao zina bonus za kufa nguruwe.

...Nimeipenda sana hii ya 'Kufa Nguruwe' Mkuu! Ni Kweli. Kwa nini Afe Binadamu...????? JF Kiboko.:yo::yo:
 
Back
Top Bottom