Kampuni za ndege lawamani kuinyima mapato Swissport

kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,223
1,670
Baadhi ya kanuni zinazosimamia utoaji huduma kwenye viwanja vya ndege hazitekelezwi ipasavyo kutokana na kampuni zingine kukiuka masharti ya leseni zao, imeelezwa.

Kanuni hizo haziruhusu watu wanaotoa huduma ya usafiri wa anga kujihudumia wenyewe, lakini ziko baadhi ya kampuni zimekiuka masharti ya leseni zao na kujihudumia zenyewe.

Akizungumza Dar es Salaam jana wakati wa mkutano wa wadau ulioitishwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Swissport, Gaudence Temu alisema hali hiyo inawanyima mapato na kuhatarisha uhai wa kampuni zingine.

"Kwanini sheria zitumike kwa operators (waendeshaji) wengine na kwa wengine zisitumike… tunashauri sheria zifuatwe," alisema Temu.

Alisema kanuni zinaelekeza ndege zinazochukua abiria 19 kushuka chini, ndizo zinaruhusiwa kujihudumia zenyewe na kuruhusiwa kuingia mkataba na shirika lingine kupeana huduma lakini wapo ambao wanakwenda kinyume na kanuni hizo.

Akizungumzia madai hayo, Mwenyekiti wa bodi ya mamlaka hiyo, Mwatumu Malale alishauri watu wote wenye mapendekezo jinsi ya kuboresha utendaji kuyapeleke kwa maandishi ili yafanyiwe kazi.

Mkurugenzi wa Kampuni ya TanzanAir, Abdukadir Mohamed aliishauri mamlaka hiyo kuangalia uwezekano wa kuajiri vijana wa Tanzania ambao wamehitimu taaluma ya urubani.

"Wengi wana masaa machache, tuangalie jinsi tutawasaidia vijana wetu ili wapate uzoefu na hatimaye kuajiriwa," alisema Mohamed.

Katika hatua nyingine, mamlaka hiyo imepokea maombi 16 ya leseni kwa ajili ya huduma za usafiri wa anga, upakuaji na upakiaji mizigo na kutoa huduma ya chakula.


Source: Mwananchi
 
kwani hawa si ndio wanao tuhumiwa na wizi wa vtu katika mizigo ya abiria...?
 
Temu na wenzake ni wezi tu bora abaki kimya maana ataanikwa hadharani ufisadi wake
 
Temu ni noma..amekula sana hela katika hilo shirika. Wizi wa watu yeye haumii wala nini na yuko tayari kuondoka.
 
Swissport NI wezi na imejaa wafanyakazi wenye dharau na kejeli.tatizo la ukiritimba ,..fanyeni kazi msiogope mashindano
 
hivi hii kampuni si ndiyo inatuhumiwa kuajiri vibaka wanaiba mizigo ya wasafiri!!!!ningeshauri fagio la mh. Mwakyembe liende huko pia!!! yaani kampuni imejaa vibaka duuu!!!
 
Back
Top Bottom