Kampuni za mawasiliano zinaweza kusaidia vita hii | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kampuni za mawasiliano zinaweza kusaidia vita hii

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Yona F. Maro, Dec 7, 2009.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Dec 7, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  HAWA WANAWEZA KUSAIDIA VITA HII

  Katika pita zangu Leo jijini nimegundua kitu Fulani kitu chenyewe ni kwamba kuna baadhi ya waajiriwa wa kampuni za mawasiliano ya simu na internet wanashiriki kwa namna moja au nyingine katika kuuza na kusambaza programu .

  Sio hao tu hata baadhi ya wafanyakazi wa kampuni zinazoshugulika na masuala ya ICT wengine kwa kujua wale wazoefu na wengine kwa kutokujua wale ambao sio wazoefu haswa wanafunzi kwa sababu vyuoni mwao hawafundishwi mambo haya na wengine ni wale waliojifunza masuala haya wenyewe kwa utundu haswa ufundi na kuinstall programu hawa wengi wao hawajui kabisa .

  Ukitembea Kwenye maduka ya kampuni mfano za simu kama zantel Utakuta wale vijana wanaotakiwa kutoa msaada kwa wateja wao wanapoenda hapo wako na cd za Microsoft windows na programu zingine kwa ajili ya kuinstall Kwenye computer hizo vile vile Kwenye maduka hayo hakuna maelezo yoyote yanayoelezea huduma hizo wanazotoa kwa wateja wanaoenda kwa msaada wa mawasiliano ya internet .

  Nashauri wasimamizi wa kampuni hizi wawe ndio viongozi kwa kukataza na kukemea tabia za wafanyakazi wao kufanya shuguli hizi Kwenye offisi zao tena pale wanapotumia programu ambazo leseni zake zimeshatumika sehemu nyingine au ambazo zimekwisha muda wake ambazo zitaendelea kumletea shida mteja , kama wanaruhusu wafanyakazi wao kufanya hivyo ndani ya maduka yao basi waseme kabisa kwamba nao wanauza software na kutoa msaada kwa software hizo na wasema kabisa kwamba wana makubaliano Fulani na kampuni wanazouza programu hizo .

  Kwa ushauri wa bure tu kampuni hizi za mawasiliano zinaweza kuingia mkataba na zinazotengeneza baadhi ya programu zinazotumika sana na watu kwa ajili ya kupatiwa programu halali kwa bei nafuu kwa ajili ya wateja wao mbalimbali wanaohitaji hizo au hata nyingine wawe wanatoa bure tu .

  Kampuni hizi zinawateja wengi kwahiyo wakiingia mikataba na watengenezaji wa programu hizo kutakuwa na faida pande zote mbili nadhani inapendeza pale mteja anapokuwa anatafuta programu Fulani kwa ajili ya matumizi ya kawaida badala ya kutumia muda na fedha kutafuta madukani anaweza kuipata Kwenye tovuti ya kampuni yake ya mawasiliano , kama antivirus , adobe , office , drivers na zingine za kila siku .

  Nimeona Kwenye tovuti ya kampuni ya Sasatel wanatoa huduma ya drivers kwa wale ambao wanahitaji kwa ajili ya vifaa vyao pamoja na maelezo mengine kwa ajili ya vifaa hivyo , hii itasaidia sana wateja wao , kampuni zingine zinaweza kuiga mtindo huu haswa kampuni zilizojitanua maeneo mengi afrika ya mashariki .

  Kwani mtu akienda kununua modem yake dukani akaambiwa anapewa na programu ya kulinda computer yake dhidi ya virus na mengine Kwenye mtandao atakataa ? na hata kampuni husika itasaidia kupanua soko lake kwa wateja wake .

  Kwa kumalizia tu naomba kuwasihi viongozi wa kampuni hizi wawe waangalifu sana siku upekuzi unaweza kufanyika Kwenye maduka yao na wenye mali ikachafua jina la kampuni wafanyakazi na kudaiwa fidia kubwa kwa tabia hizi .

  Sehemu zote duniani jamii zinajitahidi kupambana na aina hii ya uhalifu hapa kwetu inaonyesha somo halijaingia sawasawa , kwa sababu hata zile kampuni zilizofanyiwa upekuzi mara ya mwisho na kukutwa na programu bandia mpaka leo bado zinapewa tenda na baadhi ya taasisi ya serikali nyingine zimebadilisha majina lakini ni wale wale .
   
 2. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #2
  Dec 7, 2009
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,947
  Likes Received: 1,506
  Trophy Points: 280
  Shy tafadhali acha porojo bwana mbona nawe unatembea na CD za software magumashi ?
   
 3. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #3
  Dec 8, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Una uhakika na unachosema ? Mara ya mwisho kuniona ni lini nikiwa na pack ya cd
   
Loading...